Nina mtaji wa laki moja. Je nifanye nini ili niwe napata angalau elfu mbili kwa siku?

Wazo la bure.
Nenda kachonge kale kajiko kadogo hivi ka kuchomea mishkaki.
After that nenda machinjioni, nunua kichwa.
Kicharange vizuri hukoai japo kilo 4 au 5 (sina uhakika hapo).
Nenda sokoni, nunua viungo mbalimbali. Njoo marinade hyo nyama. Kisha nunua zile vimbao vya mshkaki.
Ikifika jioni, tunga hyo nyama kwenye hzo vimidenge, nenda sehem yenye mkusanyiko kama stendi hivi.
Panga vimishkaki vyako. Uza 200 vitatu jero.
Hakikisha una kasufuria kadogo ambako unapikia pilipili humo ndani so kanakua kanachemka kwa pembeni.
Usisahau ka taa ka sola ka kuning'iniza hapo kwa juu. Kama hela imebaki nunua ka redio ka bluetooth af ueke flash inayosema mishkaki mitamu 200 mitatu jero.
I got a feeling utapata zaidi ya 2000 ya faida na huo mtaji utakua bado umebaki.

Biashara ikichangamka ongeza mishkaki ya mapumbu ya ng'ombe, mmoja jero.
Hii biashara ya nyamanyama za mbuzi
kuna faida kubwa mno afanye utafiti vzr,
ikimshinda aingie kwenye matunda nako atalala hata na msimbazi
 
Umeandika kama motivesheno spika
Binadamu sisi ni wavivu sana WA kufikiria ujue ..
Ngoja nikupe practical example ya jibu langu .
Mtaji 100,000/=
Makazi ninayoishi : Karibu na stand ya mabasi
Watu wengi maeneo hay ni ( abiria , wapiga debe)
Swali la kujiuliza ni moja tu nifanye kitu Gani kuwaboreshea Hawa watu shughuli zao au kazi zao kulingana na tabia zao?

1.Abiria ( kundi hili wanapenda vinywaji, vyakula, na vitu ambavyo ni simple sana . Sasa hapa nikianza na idea ya kuuza maji Tafuta deri na mabarafu unaweka maji yanakuwa baridiiii Caton moja ya maji unainunua 9000 zipo chupa 12 ukiuza buku buku unatoka na 12000 faida 3000 .. Uza soda za kopo pia faida ni 2000 -3000 kwa Caton moja. Hapo unahitaji Caton 4 tu thamani ya elfu 40000 kutengeneza faida ya tsh 10000.

2. Wapiga debe (wengi wa Hawa watu wanatumia vinywaji vikali chukua chupa kubwa break down weka kwenye ujazi wa kawaida uza kwa Bei rafiki , wanapenda sigara nk.)
Hapa mpaka jua linazama uko hoi ila pia una maokoto
 
Haya ndio maneno sasa, ukiona mpaka mtu kaja humu ndani kuomba msaada ujue akili yake ishafika mwisho kuona fursa.
 
Sio poa yaani hapa kwenye kuumiza kichwa Kuna advantage sana sababu kama wazo ulilianzisha mwenyewe ni rahisi kumodify na kuongeza mambo ya msingi kuongeza faida tofauti na wazo la kucopy.
 
Back
Top Bottom