Nina mtaji wa laki moja. Je nifanye nini ili niwe napata angalau elfu mbili kwa siku?

Nina mtaji wa laki moja. Je nifanye nini ili niwe napata angalau elfu mbili kwa siku?

Uza mifuko, kama upo sehemu iliyochangamka kama sokoni kariakoo. Unanunua kwa jumla unazengeazengea wanunuaji unakata nyuma yao wakinunua bidhaa unawasogezea mifuko. Ya 300,500,1000.
 
Habarini wana jf.

Nimepata mtaji laki moja.je nifanyej ili nipate elfu mbili mpk elfu tano per day.

@everyone
Fungua kijiwe cha kahawa kama upo mjini ,tafuta sekta au hata tembea kijiwe baada ya kijiwe,kutembeza mahitaji ya nyumbani,njegere,vitunguu, mbogamboga,au hata nyanya ama matunda .usijali Watu watasema je,ukishindwa tafuta mtaa ambao hawakujui.
 
Habarini wana jf.

Nimepata mtaji laki moja.je nifanyej ili nipate elfu mbili mpk elfu tano per day.

@everyone
Anzisha mikopo kwa riba. Utawakamata sana wamama wa marejesho..
Bila bondi x3 ya mkopo usitoe hela.

Uzuri wa hii biashara huwa wanaitana wenyewe

No need of marketing
 
Wazo la bure.
Nenda kachonge kale kajiko kadogo hivi ka kuchomea mishkaki.
After that nenda machinjioni, nunua kichwa.
Kicharange vizuri hukoai japo kilo 4 au 5 (sina uhakika hapo).
Nenda sokoni, nunua viungo mbalimbali. Njoo marinade hyo nyama. Kisha nunua zile vimbao vya mshkaki.
Ikifika jioni, tunga hyo nyama kwenye hzo vimidenge, nenda sehem yenye mkusanyiko kama stendi hivi.
Panga vimishkaki vyako. Uza 200 vitatu jero.
Hakikisha una kasufuria kadogo ambako unapikia pilipili humo ndani so kanakua kanachemka kwa pembeni.
Usisahau ka taa ka sola ka kuning'iniza hapo kwa juu. Kama hela imebaki nunua ka redio ka bluetooth af ueke flash inayosema mishkaki mitamu 200 mitatu jero.
I got a feeling utapata zaidi ya 2000 ya faida na huo mtaji utakua bado umebaki.

Biashara ikichangamka ongeza mishkaki ya mapumbu ya ng'ombe, mmoja jero.
Master piece 👊👊
 
Weka kijiwe cha kuchoma mahindi kuanzia saa 11 jioni. Mda mwingine jiongeze na mengine.
 
Wazo la bure.
Nenda kachonge kale kajiko kadogo hivi ka kuchomea mishkaki.
After that nenda machinjioni, nunua kichwa.
Kicharange vizuri hukoai japo kilo 4 au 5 (sina uhakika hapo).
Nenda sokoni, nunua viungo mbalimbali. Njoo marinade hyo nyama. Kisha nunua zile vimbao vya mshkaki.
Ikifika jioni, tunga hyo nyama kwenye hzo vimidenge, nenda sehem yenye mkusanyiko kama stendi hivi.
Panga vimishkaki vyako. Uza 200 vitatu jero.
Hakikisha una kasufuria kadogo ambako unapikia pilipili humo ndani so kanakua kanachemka kwa pembeni.
Usisahau ka taa ka sola ka kuning'iniza hapo kwa juu. Kama hela imebaki nunua ka redio ka bluetooth af ueke flash inayosema mishkaki mitamu 200 mitatu jero.
I got a feeling utapata zaidi ya 2000 ya faida na huo mtaji utakua bado umebaki.

Biashara ikichangamka ongeza mishkaki ya mapumbu ya ng'ombe, mmoja jero.
Imeenda hii
 
Mkuu kama uko dsm cha kwanza ondoa aibu ingia kariakoo kuna biashara nyingi ndogo ndogo unaweza kufanya

Kuna hii mikanda ya wanaume inayouzwa 3000, ambayo wamachinga wengi wanaitembeza sana k.koo ... ukifika ulizia chimbo wanaponunua kwa jumla, coz kwa jumla wananunua mkanda mmoja 1000, ukiweza kuuza hata mikanda mitano kwa siku hapo hapo k.koo hukosi 10000

Kuna nyingine ya kuzungusha maji ya kunywa na hiz soft drinks zingine .. pia unaweza kuifanya pia

Kwa mtazamo wangu hiz ni biashara nyepesi unazoweza kuanza nazo kama utakua dsm ...kama uko mkoani kwakweli ntashindwa kukushauri coz kila mkoa unatofautiana kwenye fursa
 
Sio poa yaani hapa kwenye kuumiza kichwa Kuna advantage sana sababu kama wazo ulilianzisha mwenyewe ni rahisi kumodify na kuongeza mambo ya msingi kuongeza faida tofauti na wazo la kucopy.
Swadakta kabisa kwenye wazo la kucopy mbeleni atakwama kisha atakuja kuandika uzi mwingine wa kulaumu kuwa alidanganywa

Sent from my SM-C7000 using JamiiForums mobile app
 
Piga aviator, Ila inabidi usome course kwanza ya masaa 48 ambayo ukimpata mwalimu mzuri utamlipa 20k, then utaunganishwa kwenye group la telegram uwe unapewa signals, hopefully utatoboa
 
Back
Top Bottom