Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Wakuu nimebangaiza nimefanikiwa kuweka Milioni 35 nataka kuingia katika biashara Kariakoo, nifanye biashara gani?
Tafuta mentor yaan mtu ambae yuko kwenye biashara fulan ambayo succsefull..mweleze ukwel..hata mdanganye kuwa hyo ndo the only cash u have. Nenda kwa unyenyekevu mwombe akuongoze kwenye biashara yake hyo hata umpe asilimia fulan kwenye faida yako utakayokuwa unapata..kwa muda flan labda miaka miwil then unaamuaga..atakufundisha na kukupitisha kote how yeye anatoboa..na utakua umefanya jema. Na pia usianze na hela yote anza na mtaj wa 10m...zingne piga fixed deposit...

Usipofanya hvo utakuja juta mkuu...

Wenzio tushashika pesa zaid ya hzo na zkapotea huko huko kwenye biashara sabab hatukua na mising tukaingia kichwa kichwa
 
Tenga tena milioni 5.
Ingia katika biashara ya ng'ombe huku kanda ya ziwa wapo wa bei poa hasa kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

Ng'ombe nunua maximum wa laki 2.
Nunua ng'ombe 20.

Jumla Milioni 4.

Operational cost hio inabaki milioni 1, kuwaswaga toka mnadani, kuwachunga na kulisha pumba.

Baada ya wiki 1 unakuja kuwauza.

Andaa elfu 50 niache shughuli zangu nikupe darasa zaidi kuhusu karanga na biashara ya mifugo + kukupa connection
 
Kuna biashara naweza kukushauri kitaalamu ba kukuandikia mango wa biashara nikishirikiana na mawazo yako
Ila itabidi ulipie tsh. 800,000/= na lazima ukubali uje tukae pamoja tuandike kati ya siku 2 zisizozidi tatu
Hutojuta
Karibu!!!
 
Kuna biashara naweza kukushauri kitaalamu ba kukuandikia mango wa biashara nikishirikiana na mawazo yako
Ila itabidi ulipie tsh. 800,000/= na lazima ukubali uje tukae pamoja tuandike kati ya siku 2 zisizozidi tatu
Hutojuta
Karibu!!!
Kwani usijiandikie wewe huo mpango wa Biashara na ukaifanya wewe ili utoboe zaidi kuliko kutaka izo 800,000 z uyo jamaa
 
Nakupa tena ushauri
Usizike hela zote hizo kwenye biashara 1.

Anzisha biashara 3, gawanya lets milioni 21 kwa hizo 3.

Remember:
Otighe ghutola amabhulunge ghansi ghokighabho kemwe

(dont put all eggs in one basket)
 
Naomba contact zako mkuu
 

Ushauri bora sana huu.
 
Umepiga hesabu nyepesi Sana mkuu, kilemba cha kuachiwa fremu ya vyombo hakipungui M 15-20 kwa fremu za ndani, za nje hata hiyo35M yake haitoshi kilemba.
Lazima ulipe Kilemba cha kumvua mtu fremu? πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚ Dah ila biashara za kibongo bwana jau kweli! Hapo Bado hujaanza kusumbuliwa na wazee wa Tai za rangi ya karoti wale πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…