Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Nina mtaji wa Milioni 35 nataka kufanya biashara Kariakoo

Wakuu nimebangaiza nimefanikiwa kuweka Milioni 35 nataka kuingia katika biashara Kariakoo, nifanye biashara gani?
Tafuta mentor yaan mtu ambae yuko kwenye biashara fulan ambayo succsefull..mweleze ukwel..hata mdanganye kuwa hyo ndo the only cash u have. Nenda kwa unyenyekevu mwombe akuongoze kwenye biashara yake hyo hata umpe asilimia fulan kwenye faida yako utakayokuwa unapata..kwa muda flan labda miaka miwil then unaamuaga..atakufundisha na kukupitisha kote how yeye anatoboa..na utakua umefanya jema. Na pia usianze na hela yote anza na mtaj wa 10m...zingne piga fixed deposit...

Usipofanya hvo utakuja juta mkuu...

Wenzio tushashika pesa zaid ya hzo na zkapotea huko huko kwenye biashara sabab hatukua na mising tukaingia kichwa kichwa
 
Tenga tena milioni 5.
Ingia katika biashara ya ng'ombe huku kanda ya ziwa wapo wa bei poa hasa kipindi hiki cha mwanzo wa mwaka.

Ng'ombe nunua maximum wa laki 2.
Nunua ng'ombe 20.

Jumla Milioni 4.

Operational cost hio inabaki milioni 1, kuwaswaga toka mnadani, kuwachunga na kulisha pumba.

Baada ya wiki 1 unakuja kuwauza.

Andaa elfu 50 niache shughuli zangu nikupe darasa zaidi kuhusu karanga na biashara ya mifugo + kukupa connection
 
Kuna biashara naweza kukushauri kitaalamu ba kukuandikia mango wa biashara nikishirikiana na mawazo yako
Ila itabidi ulipie tsh. 800,000/= na lazima ukubali uje tukae pamoja tuandike kati ya siku 2 zisizozidi tatu
Hutojuta
Karibu!!!
 
Kuna biashara naweza kukushauri kitaalamu ba kukuandikia mango wa biashara nikishirikiana na mawazo yako
Ila itabidi ulipie tsh. 800,000/= na lazima ukubali uje tukae pamoja tuandike kati ya siku 2 zisizozidi tatu
Hutojuta
Karibu!!!
Kwani usijiandikie wewe huo mpango wa Biashara na ukaifanya wewe ili utoboe zaidi kuliko kutaka izo 800,000 z uyo jamaa
 
Nakupa tena ushauri
Usizike hela zote hizo kwenye biashara 1.

Anzisha biashara 3, gawanya lets milioni 21 kwa hizo 3.

Remember:
Otighe ghutola amabhulunge ghansi ghokighabho kemwe

(dont put all eggs in one basket)
 
Usinunue mazao na kuweka store nenda sokoni uwe unanunua nafaka kwa wakulima na wale wanaotoa vijiji, we uwe unauza kama wholesale
Ukiwa unanunua afu unaweka store ukisubili price kupanda hiyo sio biashara bali ni kamali cos posibility ya kushuka inakuwepo kubwa

Ushauli wangu: Fanya research ya nafaka unayotaka kuuza mfano mchele anzia wanakonunulia(kobolewa) inaweza ikawa Kahama, Mpanda, Mbeya n.k ili kujua season kwa mwaka ukimaliza tafuta store town hapa wanapouza nafaka agiza au uwe unaenda mwenyewe mwanzo hautakuwa unapata faida kubwa ila kadri muda unavyozidi kwenda faida utayona tena kubwa kubwa
Mwisho wasiku utapata wenyeji wa maeneo uliyochulia mzigo watakuwa wanajua wewe unataka mchele wa aina gani so itakuwa rahisi kwao kukutumia mzigo unao utaka au una mechi na soko lako

Nb: Ninapatikana Moshi (kiusa) jilani na panoni petro station nauza maharage na mchele kutoka kahama grade 1 kiroba 50kg 85000 kwa kilo 1700 na grade 2 kiroba 50kg 75000 kwa kilo 1500 na maharage price ya sokoni kwa jumla 2200 ya songea na 2300 kwa yanayotea sanya juu hapahapa moshi
Naomba contact zako mkuu
 
Nauboresha huu ushauri...maana hapa nod kuna hela.

Mkuu kwa pesa yako hiyo fanya hivi.
[emoji117]Tafuta mji ambao ndo unaanza kukua au umekua ila huduma za afya bado hazijakua.
[emoji117]Tafuta nyumba kubwa tu kwa miji kama hiyo kodi unaweza kukuta kwa mwezi nyumba nzima haizidi laki 3.
[emoji117]Baada ya kulipa kodi labda ya mwaka mzima sawa labda na milioni 3.6(hapa lipa kishika uchumba kwanza labda laki 2 kabla ya kulipa kodi).
[emoji117]Nenda manispaa onana na DMO,afanya mpango akakague jengo na mazingira akipitisha.
[emoji117]Fanya ukarabati utakao ambiwa nafikiri kwa nyumba iliyokamilika hautamaliza 5M
[emoji117]Hakikisha mazingira yanavutia,nunua na vifaa sio lazima ununue vipya kuna used kibao vilivyo na hali nzuri kwa gharama nafuu..weka huduma ya dispensary yenye RCH ndani yake...huduma ziwe nzuri na bei ya kawaida...ukiwa na uwezo weka na meno na nunua Ultrasound ya bei poa hata ya milioni 10.
[emoji117]Tafuta wafanyakazi wachache wenye uzoefu kisha kaa mwenye golini wanapolipia ndani ya mwaka utakua mtu mwingine na huduma zikiwa bomba bro utapiga hela mpaka basi.

Mfano mdogo nakupa Dawa kama Doxcy boksi linauzwa 6400 ambao kila boksi linakaa na blister 10 na kila blister moja ina vidonge kumi sawa na vidonge 100.Kwahiyo kwenye boksi moja unatoa dozi 10 dispensary ninayofanya kazi dozi moja wanauza elfu 4 hivyo kwa kila boksi unatoa elfu 40.Drip unazoziona bei ya jumla unanunua 850-1000 ila mtu utamuwekea kwa elfu 10 hapo ukitoa giving set na scalp vein faida yako ni 8000.

Bado sikwambii kwenye kitengo cha Dental jino kung'oa ni elfu 10 ,mng'oaji anaweza chukua elfu 3 ,ukitoa gharama ya ganzi na syringe unakuta unabaki na faida ya elfu 6,,,bado kwemye ultrasound na RCH bado kuna kesi za Kusafisha ,kutahiri nk.

Bro biashara ya afya inalipa hasa ukiwa mjanja na akili nyingi inalipa sana.

Nb:ukishindwa Dispensary basi funguo maabara ya kisasa au pharmacy ule maisha.

Ushauri bora sana huu.
 
Umepiga hesabu nyepesi Sana mkuu, kilemba cha kuachiwa fremu ya vyombo hakipungui M 15-20 kwa fremu za ndani, za nje hata hiyo35M yake haitoshi kilemba.
Lazima ulipe Kilemba cha kumvua mtu fremu? 😂😂😂 Dah ila biashara za kibongo bwana jau kweli! Hapo Bado hujaanza kusumbuliwa na wazee wa Tai za rangi ya karoti wale 😂😂😂
 
Back
Top Bottom