Biashara ya boda boda ni nzuri kama utaendesha mwenyewe,japo siku hizi imekua biashara ngumu kiasi maana abiria hawapandi mtu wasie mjua.
binafsi hata mimi sipandi tu boda boda ilimradi nimepanda,hivyo ili uanze ona matunda ya hii biashara itakubidi uchaji solar sana kijiweni wakati wenzio unawaona wanatoka na kuingia.
ukizoeleka biashara utapga sana ila hapo mpaka uzoeleke sasa (maji umeyaita mma)
Kwa mtaji huo nakushauri kitu ambacho vijana wengi wanakichukulia poa mno mwisho wake wanawaza mabiashara yasio na future ya kueleweka.
Binafsi siwezi fanya biashara ya boda,ila mkuu nakushauri kwa mtaji huo Hebu kaa chini tafuta location nzuri chukua frem kisha fungua DUKA LA MANGI.
duka la vitu vya majumbani tunapenda kusema dukani kwa mangi,Mkuu nakuhakikishia hili duka ukiweza litunisha mtaji kama ulionao ukajaza mazaga zaga yote na mkawa wawili (wewe na waifu) waifu mchana yote anatoka saa 8:00 usiku,wewe unaingia muda huo hadi majogoooo, BABA BABA BABA mchawi lazima uitwe braza.
Duka la mangi ni biashara bomba sana yenye Future inayoeleweka,unapokua na mtaji mkubwa biashara ya Mangi inakupa more income ila boda boda hata ujambe uharishe hutokaa hata siku 1 ulaze faida LAKI ng'ooo utachora chini.
DUKA LA MANGI uwezo wa kulaza faida zaidi ya 100k per day kila siku biashara ikija changanyia mwendo wa 360km/hr boss kama nakuona hivi utavyokuja nishukuru badae.
Achana na ma idea ya vijana sijui boda boda,sijui toyo,sijui bolt,nk (sidharau hizi idea zao) lakini future yahizo biashara zao ni inaonekana kabisa, binafsi mimi sasa hivi huwezi niambia nifungue biashara ambayo nikiiangalia baada ya 5yrs haitoweza nipa 500k per day, sifungui mimi biashara.
Biashara zenye COSTANT INCOME sizitaki na wala siziwezi,napenda duka la mangi maana the more the capital the more the income the more the customer,nk
DUKA la Mangi ni biashara ambayo kijana yeyote anaetafuta maisha na amedhamiria kupambana na ana mtaji basi simshauri mara mbili namwambia tu mara 1 Asijifikirie aifanye bila kusita sita.
Duka la mangi linauza vingi brooo,kuna mchele,unga,sabuni,wine zote,vinywaji vyote yani unakusanya unakusanya hadi ukija jumlisha faida unasema Asante BABA wewe ni mkuu.
Mama yangu alikua akimiliki duka la mangi ezi hizo,ilikua ukiingia dukani chini sakafuni kuna coin kama zote zimedondoka,huwa haziokotwi dukani kuna coin nikawa najiuliza kwann mama anaacha pesa chini? nikienda dukani kwake najifanya viatu vinanibana nikiwa pale nnje nakunywa soda navua viatu then natafuta namna yyte ile niingie dukani,napita kukanyaga maeneo yenye coin nazifinya na kidole cha mguu naziinua natia mfukoni...
Mpaka nitoke dukani mfukoni nishamake hadi buku, (buku enzi zetu wazee sio masihara)
Leo nimekua ndio naelewa kwanini duka la mangi lina pesa,kwann mama alikua haokoti coin zikidondoka,mkuu duka ya mangi ina pesa kuliko watu wafikiriavyo.
Nafanya biashara nyingi ila mwaka Huu biashara yangu kubwa ninayoenda ifungua ni DUKA LA MANGI brother penye asali washirikshe na wengine,ifanye hii biashara ina faida nyingi sana sana sana.