Nina ndoto ya kufikisha miaka 100 ya kuwa hai duniani

Habari Wadau ๐Ÿ˜ณ

Mimi nina miaka 27 na ninataka nife nikiwa na umri wa miaka 100 hivi ๐Ÿ˜

Yaani niishi hadi mwaka 2100๐Ÿ˜

Nifanye nini ili nitimize ndoto hiyo ukiachana na kuomba Mungu !!!

Waefeso 6:2-3​

โ€œWaheshimu Baba na mama yako,โ€ hii ndiyo amri ya kwanza ambayo imeongezewa ahadi, yaani, โ€œUpate fanaka na kuishi miaka mingi duniani.โ€
Amri ya tano inasema, โ€œWaheshimu baba yako na mama yako, siku zako zipate kuwa nyingi katika nchi upewayo na Bwana, Mungu wakoโ€ ( Kutoka 20:12 )
 
Habari Wadau ๐Ÿ˜ณ

Mimi nina miaka 27 na ninataka nife nikiwa na umri wa miaka 100 hivi ๐Ÿ˜

Yaani niishi hadi mwaka 2100๐Ÿ˜

Nifanye nini ili nitimize ndoto hiyo ukiachana na kuomba Mungu !!!
Hakikisha unakula chakula asliia nakujishughulisha mfano kulima, (mjini inabidi ufukuze upepo), halafu usichimbe chimbe migodi
 
Inawezekana kabisa. Ali Hassan Mwinyi alifikisha 98.

Jitahidi, pamoja na masuala mengine ya msingi kama mazoezi, ule angalau apple mbili kila wiki, utakuja kunishukuru.

1. Dhibiti kabisa kiwango cha uzito wako (maana yake uzingatie sana mlo wako). Watu wengi wanaanza kwanza kufa tumboni kabla ya kufa nafsini. Sijui unanielewa?

2. Akili yako isiwe na msongo kupitiliza na wala isikae bila kazi yoyote (kumbuka kwamba msongo ni mzuri kama haujavuka wastani wake.)

3. Jijenge kiroho, kimwili, kitaaluma, kijamii, kiuchumi na kimkakati.

4. Jihadhari na pollutions - noise, light pollution, dust/air, media, psychological, etc.

5. Jiulize kila siku sababu ya kuishi - unategemea kuacha alama gani duniani? Ukipewa miaka 100, mwingine akapewa 30, kuna tofauti? Usiishi ili tu uishie baadaye, bali ishi ili uishi daima. Sijui unanielewa?
 
Kwa member wote wa jf hakuna atakayetoboa mwaka 2100

Amri hiyo inawahusu waisraeli wa kale .Katika nchi ya Israel ya kale "mtu yeyote akimtukana baba yake, akimtukana mama yake alipaswa kuuwawa"


Sisi ni wakristo ni tofauti na waisraeli wa kale
 
Kwa kuwa kifo ni lazima, kinatokea kwa njia mbalimbali kama ajali, ugonjwa, kuuawa, kurogwa na nyingine nyingi. Usikiwazie sana. Usikiweke kichwani mwako kitu ambacho LAZIMA KITOKEE kwa muda wowote.

Unachotakiwa kufanya (sio kitakachozuia ufe) furahia maisha. Panga mipango yako ya maisha, kula vizuri, jali afya yako, furahia kuishi, epuka vinavyokuumiza, epuka kila unachoona kina hatarisha uhai wako n.k LAKINI ZAIDI SANA MTANGULIZE MUNGU KWENYE MAISHA UNAYOISHI.
 
Hakika nimeelewa!

Ila vipi kupigana na wanadamu wenzangu wenye roho mbaya?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ