Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Unataka kurogwa?
 
Umewahi kujenga nini maishani kwako? Kampuni, duka,shamba, NGO, nk?
Au, unatafuta ajira?
Kama hujawahi, kujenga chochote maishani, huna elimu mzito(kama nyerere),
Hapo mtaani kwenu unaongoza nini? Unafahqmika kwa lipi? Umetatua nini?
Au, bado unasumbyliwa na bando,pango, na pesa ya kuhonga demu!?
 
Ahsante kwa kushiriki
 
NINI KIFANYIKE ILI KUONDOA HIZI SQUATER
  • Kupima nchi nzima
  • Ni sheria kujenga kwa kufuata utaratibu ulioweka na ni kosa kujenga hovyo hovyo pasipokufuata utaratibu mfano guest hazitajengwa hovyo hovyo, bar hazitafunguliwa hovyo hovyo n.k
  • Vifaa vya ujenzi vitakua viwe bei ya chini sana mfano cement inatakiwa iwe elfu tatu kwa mfuko, kazi ya serekali ni kuhakikisha vifaa vya ujenzi vinakua bei rahisi sana
 
Viwanda vya kutengeneza aluminium na copper wire coil vitakua mkoa wa songwe ambao ni karibu na maligjafi inapotokea zambia na drc congo
 
Rasilimali za congo zinatakiwa kutumika Tanzania kama malighafi za viwanda
 
Kiongozi mzuri ni yule anayejua kutengeneza fedha/mapato kupitia njia sahihi
Kiongozi ambaye hajui kutengeneza vyanzo vipya vya mapato ataitumbukiza nchi kwenye madeni na misaada ya kidhalilishaji

Mimi Dennis R Yesse ninauwezo wa kutengeneza vyanzo vipya vya mapato
 
Polymer base materials kama Polyethylene, Polypropylene, Polyvinyl Chloride, Polyethylene Terephthalate, na Polystyrene, Polyurethane zitakua zinazalishwa hapa nchini kwa bei ya chini zaidi ya soko la dunia na sio kua-imported kama ilivyo sasa
 
Miji yote Tanzania inatakiwa ipimwe kuwe na public garden kila baada ya makazi ya watu elfu 10-20, kuwe sehemu za michezo, kuwe na shule zenye miundombinu mizuri, kuwe na hospital zenye miundombinu mizuri na misafi, kuwe na pavement sehemu za makazi ya watu ili kusiwe na vumbi kama ilivyo sasa

Miji yetu nayo iwe mizuri na sio mibaya kama ilivyo sasa
 
Kujenga oil refinery itakayokua na uwezo wa kuzalisha mapipa million 10 na zaidi kwa siku na kuzalisha petrochemical ambazo ni moja ya msingi wa viwanda
 
Viwanda vinahitaji miundombinu bila ya kuwa na miundombinu ya viwanda ni vigumu sana kwa nchi za afrika kuwa na viwanda sababu hakuna miundombinu ya viwanda ambayo huvutia waekezaji.

SEREKALI LAZIMA IJENGE MIUNDOMBINU YA VIWANDA HAKUNA NJIA YA MKATO
  • Kosa kubwa sana kwa nchi za kiafrika ni kutokujenga na kumiliki miundombinu ya viwanda- ni hatari sana miundombinu ya viwanda kumilikiwa na wageni au waekezaji binafsi hawa ni rahisi sana kuihujumu.
  • Si sawa kwa serekali kuandaa tu sera na kukaa ofisini huku wakisubiri waekezaji mambo sio marahisi hivyo muwekezaji unatakiwa umuelezee ni jinsi gani ni nafuu kuzalisha bidhaa Tanzania na sio nchi nyingine kimahesubu na sio kinadharia.
  • Nchi za gulf zimefanikiwa sababu miundombinu ya viwanda ya kuzalisha mafuta wanamiliki serekali na sio wageni au watu binafsi.
  • Nchi za western viwanda vinazidi kupungua kwa speed kubwa sababu miundombinu ya viwanda waliwaachia sekta binafsi na hata serekali zao zimejaribu kuwapa subsidy ila zimewafaidisha wamiliki wa stock wa hizo kampuni.

Nikiwa rais ntafanya mambo yafuatayo kama sehemu ya kujenga miundombinu ya viwanda- serekali itajenga viwanda vifuatavyo na kuvumiliki​

  1. Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata bauxite kutoka zambia na congo ambayo itatoa pure aluminium ya bei nafuu zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini zaidi ya wale wa nje kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za aluminium.
  2. Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata raw copper kutoka zambia na congo na kuwa pure copper cathode za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za copper.
  3. Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata iron ore, cooking coal (coke) na limestone na kuwa pig iron za bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza bidhaa mbalimbali za steel.
  4. Kujenga kiwanda kikubwa cha kuchakata cotton, wool, na kuwa yarn zenye ubora na bei bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza fabrics za aina mbalimbali.
  5. Kujenga kiwanda kikubwa cha kutengeneza silicon wafer zenye ubora wa hali ya juu, na zitakua na bei ya chini zaidi kwenye soko la dunia, watauziwa wawekezaji wa ndani bei yao itakua chini, wa nje itakua juu kidogo kwa ajili ya kutengeneza chips na semiconductor mbalimbali.
  6. Kutengeneza oil refinery kubwa ya kuchakata crude oil ambayo itazalisha bidhaa mbalimbali watakaouziwa waekezaji kwa ajili ya kuzalisha bidhaa mbalimbali.
  7. Kutengeneza kiwanda cha kuchakata gold (smelting na refining) kwa bei nafuu sana, na gold yeyote inayozalishwa Tanzania haitashafirishwa kama malighafi tena nje ya nchi kwa ajili ya kufanyiwa smelting na refining.
Ukiwa na miundombinu hiyo saba ni rahisi sana kuvutia wawekezaji na kuifanya Tanzania kuwa nchi ya viwanda

MIRADI ENDELEVU
  • kuongeza megawatts za umeme maradufu na huu utakua mradi endelevu
 
Ninakusikitikia sana kijana naona hujipendi kwa figisu za wanasiasa wa nchi hii nakuhakikishia hata ukuu wa wilaya hutaupata.Kwa mambo ya siasa ya nchi hii usipende kuweka wazi wishes zako.
 
Mawazo mazuri tatizo siasa
 
Ninakusikitikia sana kijana naona hujipendi kwa figisu za wanasiasa wa nchi hii nakuhakikishia hata ukuu wa wilaya hutaupata.Kwa mambo ya siasa ya nchi hii usipende kuweka wazi wishes zako.
Mimi sihitaji ukuu wa wilaya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…