Nina nia ya kuwa Rais wa Tanzania

Unahitajika kuwa na Roho kama ya Jiwe, otherwise ni walewale wanaokuja kupiga Sera , wakishapewa viti wanaweka mipango pembeni, wanaangalia pa kupigia pesa .

Mipango hata Mama anayo, ukihudhuria vikao vyake utaisikia hiyo mipango inavyopangwa, Angalia sasa utekelezaji "F" ila maneno Mengi .

JPM akikwambia Namtimua fulani, naleta Soko, Flyover, SGR, Mradi wa umeme, kinachofuata ni vitendo ... By anymeans hata Mikopo ya Kausha damu .

Je umeshachukua hatua gani mpaka sasa itayoweza kukusogeza kwenye kugombea Uraisi?
 
Hataki kuambiwa ukweli huyu mwache aendelee kushusha notes labda rais anaweza akamuona ana kauzalendo akamvuta hata kakitengo ndani ya TIC au wizara ya viwanda akahojiwe atafanyaje hayo bila kushirikisha private sector..
 
nimechukua maoni yako ntaifanyia kazi nagombea mwakani
 
Kwani ni kosa mtu kuonyesha nia yake
Changamoto ya watanzania ni waoga sana nauhakika hata wewe siku mtoto wako akikuambia anatakakua flani lazima utamfokea

Jamii ya kitanzania na kiafrika ni kosa kubwa kuwa na ndoto na ndo kitu watawala wanachopenda
 
Kwani ni kosa mtu kuonyesha nia yake
Changamoto ya watanzania ni waoga sana nauhakika hata wewe siku mtoto wako akikuambia anatakua flani lazima utamfokea

Jamii ya kitanzania na kiafrika ni kosa kubwa kuwa na ndoto na ndo kitu watawala wanachopenda
Sasa wewe umeonyesha tu nia ila njia za kufikia hutaki tukushauri ..hata ebu tueleze njia zako utafikaje pale kwenye urais??maana kwa sasa mgombea binafsi hatakiwi
 
Watu wengine kushindwa jambo flani halikuzuii wewe kulifikiria na kulifanya

Changamoto kubwa ya waafrika ni uoga na kukata tamaa au jambo mtu akiona hawezi kufanya atahakikisha kila anayetaka kufanya anamkatisha tamaa
 
Sasa wewe umeonyesha tu nia ila njia za kufikia hutaki tukushauri ..hata ebu tueleze njia zako utafikaje pale kwenye urais??maana kwa sasa mgombea binafsi hatakiwi
Hakuna ajuaye kesho au mwakani nini kitatokea au baada ya miaka 5 nini kitatokea na hakuna lisilowezekana chini ya dunia

Usiogope kufeli sababu ni sehemu ya maisha ya binadamu kikubwa hujavunja sheria ya nchi
 
Wazo zuri tatizo ni jamii tuliyo nayo hadi mafuvu yarudishiwe akili, ni jamii ya bora liende ama kanyaga twende tuseme bendera fuata upepo, jamii ambayo ikilishwa fikra chanya na hasi haiwezi kupambanua, wanao pewa dhamana baadhi ni wajinga wengine wamekubali kuongoza taifa kwa unyumbu wa kisiasa,

Unyumbu wa kisiasa ni tabia ya wanaopewa dhamana kuahirisha kufikiri kwa nafsi kwasababu ya kujipendekeza, kulitumikia kundi fulani kwa masilahi binafsi na uoga kwa viongozi wao bila utii, (unafiki), a.k.a kujizima data tuseme kuahirisha kufikiri kizalendo, kwasasa uchawa
 
Mimi baada ya kuona hali ya viongozi wetu walivyoo hawana mpango wowote wa kuwatoa wananchi kwenye umaskini niliona nikosa kubwa sana kwa sisi vijana kuendelea kukaa nyuma ni hatari sababu viongozi waliopo wanapigania maslai ya familia zao

Mfano nchi inaweza tumia tsh billion 100 tu kutengeneza refining ya gold na makinikia yakawa hayapelekwi kufanyiwa refining nje ya nchi serikali itakuambia haiwezi lakin kila mwaka wanatenga tsh billion 300 kununua magari ya kifahari sasa ukiangalia hapo siuna ona kuna tatizo kubwa
 
Ni kweli una malengo mazuri ila nakukumbusha ukomo wa uongozi ni miaka 5
 
Watu wengine kushindwa jambo flani halikuzuii wewe kulifikiria na kulifanya

Changamoto kubwa ya waafrika ni uoga na kukata tamaa au jambo mtu akiona hawezi kufanya atahakikisha kila anayetaka kufanya anamkatisha tamaa
Waafrika sio waoga, Acha kua mtu wa excuses , kwani Jiwe alikua Mu-asia, Wale wakenya walioandamana ni wa US?


Kukata tamaa kwa wananchi kunatokana na viongozi kushindwa kusimamia ahadi walizotoa na kuangalia namna ya kutupiga tu punde wakipata nafasi, mfano wa ahadi ni hizo ulizoorodhesha mwishowe wanachangia ugumu wa Maisha kwa percent kubwa!!


Halafu usiruke maswali hujajibu hili swali "Umechukua hatua zipi mpaka sasa zinazokusaidia wewe kufikia Lengo la kua Raisi na je ni Yepi unayoyafanya ambayo hata waliokuzunguka wanakuona wewe unafaa kua kiongozi ?
 
Tunatatizo kubwa linalohusu uongozi Tanzania, ndiyo maana nimetumia neno wajinga, na nikweli wengi wanaopewa dhamana ni wajinga wanafanya maamuzi ya hovyo, darasani, (in entrepreneurship) tunajifunza kwamba asilimia 80 ya mafanikio kwenye biashara yana mtegemea mjasiriamali na aslimia 20 ni mjasiriamali na yanayo mzunguka, (the entrepreneur and his her environments), lakini hii aslimia 20 ina nguvu hata ya kuua biashara , endapo jamii itaendelea kunyamaza

Silence surrenders public responsibilities
 
Hongera kwa nia nzuri.

Maswali yangu kwako kupima uwezo wako!

1. Utafanikishaje ujenzi wa viwanda laki 1 ndani ya miaka 10 tu?

2. Utafanikishaje sekta zisizo rasmi kuajiliwa kwenye viwanda wakati hawana ujuzi wa kufanya kazi kwenye viwanda?
Mimi nimemwelewa sana huyo kijana pamoja na andiko lake;Kusudio la andiko lake ni hili hapa:
1:Ukweli Wala Hana Nia kabisa ya kugombea urais , kwakuwa hata Katina inataka angalau awe na umri wa miaka 40
2:Baada ya kumaliza masomo yake pale Mzumbe Kuna mwanga flani kaupata kuhusu viwanda kitu ambacho ni kizuri ingawa sina hakika kama kafanyia tafiti hayo yote aliyoandika,ila uchambuzi wake ni mzuri
3:Anafahamu fika hata wasaa huo wa kupendekezwa au kuchukua fomu kwake ni jambo gumu, ila anatamani hao watu wanaopewa au watakaochaguliwa kuongoza hii nchi waone hizo fursa za kiuchumi upande wa viwanda
4:Anajua fika nchi hii Ina wabunge,mawaziri, makatibu wakuu, wadau Mbali Mbali hata raia wa kawaida kwani hawapiganii hizo fursa? Lakini kwanini pia nchi inaachwa iongozwe Kwa misingi hii iliyopo na mifumo iliyopo ya kiuchumi kisiasa na kijamii?
Anatamani Hali hiyo iungwe mkono na kupiganiwa inadilike.
 
Ndoto nzuri,Mungu akusaidie na mikakati pia mizuri nimeona.Sema nini hujagusia Maslahi ya Viongozi wastaafu 😂,Hao jamaa kama hujagusia maslahi yao sahau wanaftina balaa
 
Wewe ni mtu na nusu.
Anza kuwaza kisiasa kwanza ili uonekane na kuvumbuliwa na wapigakura
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…