Nina serious clients wanaohitaji huduma kukosa ofisi kumekuwa "red flag" inayonikosesha pesa naombeni msaada wadau

We mwenyewe kazi huna unagongea mpaka elf 25, alafu unataka utafutie watu kazi! Kweli maajabu hayawezi kuisha!
Ndugu naamini hujasoma vizur uzi wangu ama pengine umesoma ila hujaelewa Mungu akusaidie kichwa cha wepesi wa kuelewa.
 
Mkuu as I told you tuombe Mambo yaende vizuri JF kuna baadhi ya watu ni wajinga watajiribu kukatisha tamaa Ila kwa Nilivyokusikiliza una potential kubwa utafika mbali Sana na upo smart Sana .
Asante sana Dr. Kwel kuna watu wanakatisha tamaa but Mungu ni mwema kuna watu kama wew pia wanao nitia moyo hivyo I still have faith and I won't loose hope, once again Thank you very much Doctor.
 
Madam Jane upo sahihi yani ninafanyaga survey na huwa najitosa sana hasa posta yani hata jana nilienda nilikutana na kihoja dada angu handler wa jengo ni kampuni flani sitohitaja ila baada ya mazungumzo nao walikubali rent ya mwezi mmoja ila kimbembe nikuwa wanahitaji nilipe security deposit sio one month but ya 3 months nikasema duu ndo utaratibu gan huu kwahyo miez 4 hapo. Lakin pia dada angu offisi is one thing bado meza na viti ( furniture) hata kama ni vya cello Lakin still namaanisha kuna another cost on top of cost. Sinauwezo wa kunyanganya na kuiba Dada angu pamoja nakuwa ni kwel Dunia haina Huruma kwa watafutaji, uwezo wangu ni huu wa kutafuta wadau na walengwa kwenye platform kama hii ya JF kuingia kwenye makubaliano ya kutunufaisha sote ama nje ya hapo kama pangekuwa na watoa mikopo kwa bisashara zinazojiestablish nazani ningekuwa wa kwanza kwenye folen maana ningelala nje ya ofisi yao.ila still Asante kwa comment yako nzuri yakutia moyo.
Bro sio rahisi mtu kukupa ofisi bure, japokua wapo wenye ofisi kubwa na yenye vyumba visivyotumika wanavyoweza kukuhifadhi uendelee na biashara yako ila ukweli ni kwamba hata kama ni wewe si rahisi kufanya hivyo sababu vipi ikitokea umechukua pesa za watu ukatokomea kusipo julikana nani atakamatwa kwa wizi kama sio alie kuazima ofisi?

Hapa ndo watu wengi wanaogopa na wanashindwa kukwambia.

Mfano wewe unafanya biashara ya kutafutia watu kazi abroad,vipi mbona wewe Huna kazi kwanini usijitafutie kazi huko abroad?

Lazima anaetaka kukusaidia ajiulize haya maswali na kuishia kupata wasiwasi.

Najua hii ni idea nzuri na inaweza kua inafanya kazi vizuri lakini nachoweza kukushauri better ukatafuta shughuli ya kufanya upate angalau kipato uweze kusave hata atleast kwa mwaka mzima then ndo uje urent ofisi na vifaa vyako vya ofisi upambane na idea yako hii ukiwa na mtaji wako atleast wa kuendesha ofisi hata kwa miezi 6.
 
Ni kwel kaka pengine upo sio rahisi Lakin kama nilivyojieleza hapo sihitaji charity wala bure, bali ni makubaliano ya kibiashara ya pande mbili zote kunufaika na yenye kulindwa kisheria.
 
Upo sawa ila ni vizuri kuanzisha ofisi yako,haya nayaongea nikiwa na experience nayo kwani unachopitia wote tunaoanzia scratch tumepitia.

Unaweza ukashare ofisi na mtu kwa mkataba fulani wa malipo ukapambana ila siku atakapo ona unafanya vizuri anaweza kukutimua na aka fungua biashara kama yako na wateja wako wote wakija pale watahudumiw kama ni wewe.

Maumivu ya kuanzisha kitu chako ni muhimu kwa mjasiamali kwani yatakusaidia vitu vingi sana huko mbeleni.

Hakuna mjasiamali aliefanikiwa kutoka scratch ambae hakufaulu ili zoezi la kusave kipato kwa ajili ya kujikusanyia mtaji wa kuanza anachowaza kwenda kukifanya.

Jitafutie mtaji ufungue ofisi yako kaka,ofisi za watu zina kila kero na manyanyaso kweli kweli.
 
Upo sawa ila ni vizuri kuanzisha ofisi yako,haya nayaongea nikiwa na experience nayo kwani unachopitia wote tunaoanzia scratch tumepitia.

Unaweza ukashare ofisi na mtu kwa mkataba fulani wa malipo ukapambana ila siku atakapo ona unafanya vizuri anaweza kukutimua na aka fungua biashara kama yako na wateja wako wote wakija pale watahudumiw kama ni wewe.

Maumivu ya kuanzisha kitu chako ni muhimu kwa mjasiamali kwani yatakusaidia vitu vingi sana huko mbeleni.

Jitafutie mtaji ufungue ofisi yako kaka,ofisi za watu zina kila kero na manyanyaso kweli kweli.
Mtoa mada zingatia hili sana tu tena kwa mapana zaidi.
 
Asante Kiongozi. Shughuli nayo fanya ni agency recruitment for job seekers abroad na admission & Scholarship abroad agency facilitator sijui nimeeleweka mkuu ?
Ndugu fanya hivi mtafute huyo mama mpe ukweli na mpe offer ya kumfanyia hio kazi na malipo afanye pale atakapo fanikiwa huyo mwanawe. Hela atakayo lipa ndio itakuwa mwanzo wa utafutaji wa ofisi yako. Pia kuwa serious kwenye mavazi na maongezi kuna watu wana kusoma kwa muonekano au maneno yako.
 
kwamba humu ndani utapata msaada usiweke akilini sana.
Naona unatumia mpaka emoji za kucheka “😂😂” nakuwoon!
 
Upo sahihi sana kiongozi na ctually nilifanya hivyo aliniambia kibusara tuu kuwa mchakato wa kumpeleka mtoto wake Germany tuu una include kufungua block account inayo hitaji ku deposit 36M hivyo pesa itakuwa changamoto kwa muda huu na kuwa yeye no government employee kuwa angekuwa ni business person ana office pengine tungekaa chini tuone tunafabyaje..nashukuru kwa ushauri na busara zako kiongozi.
 
😂😂😂😂 Sasa ulitaka niweke emoji za kulia kiongozi mchimba chumvi 😂😂😂. Kuna watu wanastahajabisa hii dunia.
 
Kutokana na maelezo yako hapo juu unahitaji nini hasa
1.Pesa ukodi ofisi? Msaada au ukopeshwe??
2. Unahitaji mtu mwenye ofisi akusaidie kwa mda ufanye shughuli zako?

Kama ni mkopo wa pesa unakitu gani cha kuaminiwa?
Kama ni ofisi kuna uhakika gani hautochukua pesa za watu ukaingia mitini mwenye ofisi akabaki na madeni?

Kama kweli hauna makando kando njoo Dm,
 
Upo sahihi sana kiongozi na ctually nilifanya hivyo aliniambia kibusara tuu kuwa mchakato wa kumpeleka mtoto wake Germany tuu una include kufungua block account inayo hitaji ku deposit 36M hivyo pesa itakuwa changamoto kwa muda huu na kuwa yeye no government employee kuwa angekuwa ni business person ana office pengine tungekaa chini tuone tunafabyaje..nashukuru kwa ushauri na busara zako kiongozi.
Tafuta vijana wanao taka kwenda Ulaya waambie unafanya safari malipo nusu mwanzo akipata visa ana malizia. Mwanzo wa kutafuta usitaka wateja wakubwa wenye mafanikio, Bali tafuta wale ndio kwanza wanajitafuta hawa wenye kujitafuta watakupa changamoto nyingi sana. Lakini ndizo hizo changamoto zao zitakifanya kufikia mafanikio yako. Hakuna alie fanikiwa bila kutoa sadaka atakae kudhulumu fanya ndio sadaka yenyewe mkuu. Usikubali kutumia ofisi na mtu mwengine kwenye biashara watu wana kopiana kwenye kutafuta hela.
 
Kiongozi nashukuru sana kwa wazo lako lenye tija mkuu nitalizingatia ili.
 
kuna ka stoo haka tumekageuza ofisi, ila hakuna dirisha kwa hiyo usiwe unakula maharage......

Back
Top Bottom