Nina shilingi milioni 64, niwekeze kwenye biashara gani kati ya hizi?

Asante kwa wazo.
64m napata Fuso la kuanzia? Na je, Fuso moja inaweza nipa return nzuri ya kuonekana? Unaweza nipa insights zaidi?
Usijaribu biashara hii kichaa, utamnufaisha dereva.

Wekeza UTT mfuko wa wekeza maisha kwa miaka kumi. Kila mwaka utapata interest ya 30% ukiwa umekaa bila kufanya kazi. UTT hautojuta.
 
ebu nisaidie milion 1 ntakushukuru sana sana TheCrocodile said
 
Nunua eneo kubwa nje ya mji kama Nala au michese....chimba kisima...M15 inakutosha kabisa na apo umenunua na jenereta incase umeme ukikatika......haya chimba bwawa la samaki(mawili ili ufuge samaki aina mbili na kambale wakiwemo)....weka drip irrigation...jenga kijumba kidogo cha msimamizi..hapo roughly itafika M30....chukua M8 nenda kwa doctor bajaji hapo chukua TVS mpya ...hii itakusaidia kama passive income ili usilie lie njaa..na pia usiguse kiasi kilichobaki kwenye m64 ....kumbuka utakua umebaki na M16, imetulia..hii mpaka ifike miez ,6 utakua umepata akili ya wapi uiwekeze

NB: kwakua umekiri wazi hujawah fanya biashara..wewe huhitaji biashara za kuumiza kichwa kwakua pia usimamizi wako utakua mdogo...

Ukipata hela yeyote kwenye sources zako anza biashara ya kujenga Nyumba za kupangisha au nunua government bonds
 
Shika namba 1 na namba 4
 
Tv huwa zinakodishwa kwenye kumbi za sherehe au yale matukio makubwa yanayojumuisha watu wengi kwenye kumbi maalumu. Kwa hapa mjini watu ambao wanafanya kazi za kurekodi video kwenye matukio huwa wanakodi hivyo vifaa.
Tatizo haielekei kuwa long run business na vigumu kufanya profit projection na hata kupima growth yake. I wish the man should not buy this idea!
 
Ngoja nkuambie, sijui km umeshaambiwa..kimbia haraka na 50m kawekeze UTT ama zile Bonds za serikali utanishukuru.

hyo ingine chagua wazo moja hapo lisilo na mtaji mkubwa na anza na 5m. Tuliza akili yako kabisa.
Fafanua kidogo, wazo hili mkuu

Sent from my SO-01J using JamiiForums mobile app
 
Wazo namba 1 ni zuri zaid. Ila Kuna muda utahitaji kwenda vijijini kutafuta mbuzi ww mwenyewe, Je, muda wako utaruhusu hilo moja la kufikilia.

Sehem ya michezo ya watoto ni nzuri pia Ila uwe mvumilivu kweny pesa tako ya mtaji kurudi.

Me nafikilia uendelee kufikilia zaid na zaid na chochote utachofikilia fikilia pia changamoto zake na mazingira yako ya kazi yataruhusu ww kuangalia biashara yako muda ambao unaweza itajika pia kazini.

Kingine kikubwa zaid kama umeoa na unamwamini mkeo..
Tenga million Kumi mfungulie duka liwe na nafaka na vitu vingine vya muhimu, pia miamala, na gas.
Alfu mwambie hii biashara sio ya kwake ni ya familia kila week uwe unaenda kupiga hesabu.
Biashara ikikua unamtafutia msaidizi.

Huku ww unaendelea kufanya saving kutoka kweny mshahara wako.
 
Tatizo haielekei kuwa long run business na vigumu kufanya profit projection na hata kupima growth yake. I wish the man should not buy this idea!
Fursa ni fursa tu. Ukiweza kutengeneza hela nyingi ndani ta miaka miwili unahamia kwenye fursa nyingine. Mpaka miukumbi yote iweze kuwa na tv zake zitakuwa zimepatikana fursa nyingine. Ila kwa sasa Pesa ipo.
 
Mkuu endelea kusave ifike 150m utengeneze Petro station..kwanza kwasasa tafuta eneo potential Kisha lifanyie urasimishaji andaa 10m kwa ajili ya consultant expert Hadi upate hati akushugulikie hatu zote

Sent from my Infinix X656 using JamiiForums mobile app
 
Kama hauna shida ya utajiri wa haraka kanunue hati fungani za serikali wakati unaendelea kujitafakari biashara ya kufanya.
Chukua walau ya miaka 5 yenye riba ya 8.6% kwa mwaka.
Hii ni sahihi kabisa, kwa namna alivyojieleza aweke kwenye Govt bond za miaka 20 or 25 atapata return ya kuanzia 12% kwa mwaka, ama aweke UTT liquid fund pia wakati anafikiria vizuri biashara ya kufanya. Active biz inaweza kuwa risk kwake kwa kuwa itahitaji usimamizi wa karibu sana.
 
Uzuri wa hizi anaweza kuchukua hela yake wakati wowote akiwa amepata biashara nzuri ya kufanya.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…