Nina Swali fikirishi nahitaji kupata ufafanuzi kuhusu Wanyama Pori

Nina Swali fikirishi nahitaji kupata ufafanuzi kuhusu Wanyama Pori

Bueno

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2022
Posts
34,600
Reaction score
59,760
Wakuu, naomba kwa mwenye uelewa anisaidie kidogo kwenye hili. Naomba kueleweshwa kwa mfano Simba wengi namaanisha wengi wakaamua kutoka MBUGANI kwenye Hifadhi ya Wanyamapori wakaingia mjini watu wataokutana na Simba hao wanatakiwa kufanya nini ili wasidhurike?.

Naomba hili swali nijibiwe na mwenye uelewa nimeona km kuna Simba wengi sana wanaenda kuingia mjini ila sijui ni wapi. Na msiniseme km naumwa au naugua kichaa au nimeonaje. Naomba kwa mtu mwenye uelewa atufafanulie Simba wakiingia mjini watu wanatakiwa kufanya nini?

Namaanisha hivi ukikutana na Simba wengi sehemu ambayo hakuna nyumba hakuna mti hakuna kitu chochote cha kujibanza umekutana na kundi la Simba wengi hili hapa unatakiwa kufanya nini?
 
Lala chini kisha jikaushe km sukamu usitikisike hata ukiumwa na nyoka usishtuke, angalizo simba ana kawaida ya kukupiga kucha ili ahakikishe km umekufa kweli au unamuigizia maana simba hua hali mzoga km fisi
 
Unakodoa,simba ni mwindaji sio mviziaji
Mkuu hivi umeelewa swali? Simba wengi mbele yako umekutana nao hawa hapa utawakodolea wangapi na kuwaacha wangapi? Na utawakodolea kwa muda gani? Elewa ni kundi la Simba sio Simba mmoja
 
Majani yazidi kupigwa ban
Jibu swali mkuu huna jibu usisingizie majani, nahitaji watu wa wanyama pori km wapo humu watusaidie kujibu ili kujinusuru unapokutana na kundi la Simba unatakiwa ufanye nini? Au hata km kuna Wamasai wanaweza wakatusaidia hili swali
 
Any way swali lako kuwa ukikutana na Simba wengi na uko sehemu ambayo sio rahisi kujitetea ni sawa na swali mtoto akikuuliza hivi ukitupwa baharini na hujui kuogelea Baba Utakufa?
Ndio linafanana na hilo maana hilo pia linafikirisha, sasa jibu swali umekutana na kundi la Simba mbele yako utafanya nini ili kujinusuru usife?
 
Wakuu, naomba kwa mwenye uelewa anisaidie kidogo kwenye hili. Naomba kueleweshwa kwa mfano Simba wengi namaanisha wengi wakaamua kutoka MBUGANI kwenye Hifadhi ya Wanyamapori wakaingia mjini watu wataokutana na Simba hao wanatakiwa kufanya nini ili wasidhurike?.

Naomba hili swali nijibiwe na mwenye uelewa nimeona km kuna Simba wengi sana wanaenda kuingia mjini ila sijui ni wapi. Na msiniseme km naumwa au naugua kichaa au nimeonaje. Naomba kwa mtu mwenye uelewa atufafanulie Simba wakiingia mjini watu wanatakiwa kufanya nini?

Namaanisha hivi ukikutana na Simba wengi sehemu ambayo hakuna nyumba hakuna mti hakuna kitu chochote cha kujibanza umekutana na kundi la Simba wengi hili hapa unatakiwa kufanya nini?
Hapo huna la kufanya zaidi ya kuwaitia Yanga wamalizane nao chap. 😂
 
Hapo ni ishu ya confidence tu kama unaweza kaza moyo shusha chini kabisa hofu ili kupunguza kasi ya frequency zako.
Simba,nyoka upima kiwango chako cha hofu kupitia masafa ya mawimbi yako kama ni hatari kwao ili wakudhuru kama hatari hawana shida na wewe.
Thus watoto wachanga huwa hawadhuriki kwa sababu wao hawajui hatari kwa maana hawatoi mawimbi ya hofu.
Nje ya kusimama ukijiamini hakuna salama ingine.
Simba kama hana njaa na sio tishio kwake hana mpango na mtu.
 
Back
Top Bottom