Nina Tsh 150,000 tu, nifanye nini ndani ya siku kumi na tano nipate Tsh 3,000,000?

Milioni 2 inatosha migodi ya wapi hii
 
Sembe itakua unaisikia tu mkuu nenda Arusha uone walioanza na maduka ya Sembe na sasa hivi wanapeleka mzigo Nairobi kitu chochote ukikifanya kwa umakini utafanikiwa unaponda biashara nzuri na makini kwa biashara ya ujanja ujanja dakika mbili unatapeliwa..
 
achana na huyo kenge mkuu, nina bro wangu alianza biashara ya duka la jumla kwa 10m kwa sasa kwa sasa turn over yake kwa mwaka ni over 300m, hyo biashara ya dhahabu naijua ndani nje akawadanganye kenge wenzake
 
Huyu jamaa hata nashindwa kumjibu, kazi za kununua dhahabu ni ngumu sana, kwanza unaweza ukawa na pesa machimboni na usipate dhahabu kabisa


Ndo maana Makota wengi wanawakopesha sana watu wenye makarasha ili ikitokea anakua na dhahabu anampa priority yeye kuinunua


Faida kwa Kila gram haiwezi kupishana elfu kumi Toka mgodini mpaka sokoni, sana sana hua inakua elfu 5 mpaka 6 kwa Kila gram, hivo lets say mtu ukiwa na mtaji wa kama Milioni 10 ukifanikiwa kupata mzigo wote unaenda kulamba kwenye laki 4 ivi, sio rahisi kivile


Na hapo ujue kuichoma dhahabu vizuri, ukizubaa ukienda jikoni Kule unakuta pesa yako inapungua, hakuna kazi rahisi mazee ingieni field ndo mtaelewa


Hivi kweli kazi za mgodini zilivyokua ngumu kuanzia mchama(muwekezaji), watenda kazi, mafundi wa Kila idara,wachorongaji,wenye makarasha na wanafanya biashara zao maeneo ya mgodi n.k alafu ukute eti ukinunua dhahabu mgodini ukienda sokoni unapata elfu 50 kwa Kila gram, nani kwanza angeuza dhahabu yake porini tena?? Na hio dhahabu si ingekua inagombaniwa kwa ngumi kabisa??


Biashara ya kununua dhahabu In reality tegemea faida ya elf 6 mpaka 8 kwa Kila gram
 
Umejificha kwenye kivuli Cha 'machimbo yasio rasmi'... Ila kwenye migodi yote tunayoijua hicho ulichoandika hakina uhalisia kabisa
 
Acha ubishi wewe kitaita sasahivi 1 g ni 200k
 
Nishamjibu mwenzio akashindwa hoja na wewe nishakujibu lete hapa ushahidi wa machimboni dhahabu kuwa 200k.
Na sokoni utauzaje ilhali bei ya mwisho ni 190k!!??
Nasubiri jibu.
Kitaita bei yake ni 200k na loliondo ni 180k per gram lete porojo zingine
 
Hapo ni lazima ufanye kigu high risk ambacho matokeo yake yatakua ni kupata io milion tatu au kupoteza io 150k yako. Na hamna kingine zaidi ya kucheza kamari
 
Basi wewe unaongea porojo
 
Umejificha kwenye kivuli Cha 'machimbo yasio rasmi'... Ila kwenye migodi yote tunayoijua hicho ulichoandika hakina uhalisia kabisa
Thibitisho wewe penye uhalisia.
Nasubiri majibu hapa.
 
Hizo hapo sasa ili ujue sisi hatupigi mdomo nililipwa 390 piga hesabu. ni shingapi kwa kila gram
 

Attachments

  • IMG_20240525_153825_913.jpg
    2.6 MB · Views: 11
Nani alisema ni biashara rahisi!?
Kwa akili zako unadhani unavyofanya biashara wewe ndicho wanavyofanya wengine!?
Kama umeshindwa wewe na wengine basi msijumuishe na watu wengine man.
Kama kwako ni ngumu kupata basi haifikirii na kwa wengine ni vivyo hivyo.
Nikae nidanganye kwa faida ya nani!?
Labda ni wewe unatengeneza faida ya 6k ila wenzako kuanzia mimi katika kila gram moja faida ndogo nilounda ni 25k mpaka nasimamia hii biashara.
Mbinu unaotumia wewe sizo atakazotumia mwingine.
Hivyo tusiitane uongo ilhali hujui ni nafanyaje na wewe umefanyaje.
 
Kitaita bei yake ni 200k na loliondo ni 180k per gram lete porojo zingine
Sijawahi kufika huko.
Mwisho wangu mimi Gairo.
Hiyo dhahabu ya 200k kwa gram sokoni unaiuzaje ilhali BEI ELEKEZI ni ile nilokutumia kule juu ambayo karat 22 ni 190k??
Aya tueleze unauza soko gani hiyo!?
Kama sio wewe ndio unaleta porojo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…