Nina Tshs. 300,000, Naweza kuifanyia nini ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?

IZAMA

Member
Joined
Dec 29, 2014
Posts
81
Reaction score
15
Ndugu Wanajamvi,,
Poleni na majukumu.

Historia:

Mimi ni kijana umri 25. Nilimaliza kidato cha 4 mwaka 2010. Nikafaulu na kuchaguliwa kujiunga form 5 (2011) Azania boys. Comb: PCB. Mlezi aliyekuwa ananisomesha alifariki 2009 mwaka 1 kabla ya kumaliza o'level.

Kwa neema nikafanikiwa kuanza form 5. Hata hivyo nililazimika kuacha kutokana na kushindwa kulipa ada na michango mbalimbali ya shule. Hata hivyo nikajiapizia kuendelea na masomo.

Update: Hivi karibuni nimejaribu kufuatilia MUHAS nikaambiwa nafasi zipo za kujiunga kama nikitumia cheti cha form 4 kupitia diploma. Kilichonikatisha tamaa ni ada yao yaani Tshs. 1,114,400 kwa mwaka na kozi hiyo itachukua miaka 3. Maana yake 1,114,400 X 3 =3,343,200/- Chuo kinaanza mwezi July 2015

Cheti changu kipo hivi:
2010
Chem B pass
Biology C pass
Physics D pass
Maths C pass
Geo C pass
Kisw C pass
Eng C pass
Hist C pass
Civ C pass

OMBI:
Nina kiasi cha Tshs. 300,000. Je,naweza kuifanyia nini pesa hiyo ili mpaka July niwe nimepata ada ya Tshs. 1,114,400?

Kaka zangu, dada zangu Naomaba msaada wa mawazo. Jinsi gani nisiikose nafasi hii maana bahati hairudi. Asanteni sana kwa utu wenu!!
Wadhamini mnakaribishwa.
Tuwasiliane: izackmanase@gmail.com au
0768577654
 
Pole sana ndugu, kwa haraka nashindwa kufikri ni kitu gani unaweza fanya na hicho kiasi cha laki 3 kwa miezi takribani miwili ili upate 12,00,000/-, naomba wadau waje wakusaidie, ila usikate tamaa. Naamini kamwe ndoto yako haiweiz kupotea, inaweza kuchelewa tu, one day yes!
 
Anza kubet ila uwe na roho ngumu
 
Me nakushauri kidogo!

Nenda teaching kisha ajiriwa na gvnt utakapoajiriwa omba kusomeshwa na PSPF au mfuko wa kijamii utakaokuwa umejisajili! Kwa sababu utasomea medicine au coz yoyote ya sayansi ambayo una uhakika wa kuajuriwa na gvnt watakusomesha bila shida
na lastly utakuwa ume archieve malengo yako!

Sio lazima malengo yako yaende kwa njia nyepesi kama unavyotaka, sometimes inapitia mzunguko!
Hali kama yako ilinikuta nikaingia ualimu na sasa ni dokta.
 
Wa TZ bwana kijana mwenzetu anaomba msaada wa Mawazo tu,comment zinazotelewa hazifanani kabisa na utu.
Kama huna msaada unaonaje ukikaa kimya ukawaacha wenye kusaidia wakatoa ushauri. Kumbuka leo kwake kesho utakuwa wewe.

Mkuu usikate tamaa na pole kwa yaliyokupata,nimechukua contact zako ntakutafuta kwa maelezo zaidi.
 
Pole sana na Hongera kwa kuonesha kutokataa tamaa.
Ningekushauri ufuate Proper Channel kuomba Msaada.
Naamini wafadhili wa kukulipia ada utawapata, watu hawaaminiki nowdays,watu watajuaje kama wewe sio Tapeli?
Ungeanza na kwenda ITV could be the best step
 
Kuingiza laki 3 na kutoa million 1.2 kwa miezi 3 kwa biashara halali ni ngumu kidogo. Labda ufanye biashara ya kuongeza thamani ya bidhaa na sehemu kubwa ya mchakato huo ufanye kwa mkono yako. Kwa mfano ununue ngano usage mweyewe, ukate kuni mwenyewe, upike chapati wenyewe, uuze mwenyewe :glasses-nerdy:
 
Nimeguswa sana na maelezo yako. Lkn pia naona uwezo wako kiakili kutokana na ufasaha wako ktk mtiririko wa maelezo. Usichoke tutafika tu. Hebu tueleze zaidi, Nikwamba Baba na Mama na Ndugu wengine wote ha wapo au wapo lk uweze wa kukusaidia haupo?
 
Nimeguswa sana na maelezo yako. Lkn pia naona uwezo wako kiakili kutokana na ufasaha wako ktk mtiririko wa maelezo. Usichoke tutafika tu. Hebu tueleze zaidi, Nikwamba Baba na Mama na Ndugu wengine wote ha wapo au wapo lk uweze wa kukusaidia haupo?

Tuanzie ukoo wao wako wapi mpaka wanashindwa kumsaidia
 
dini yako tafadhal waweza kwenda kwa gwajima akufanyie maombi utapata tu wafadhili.
 
Nitafute nikupe mikeka uwe una beti utapata zaidi ya iyo ela nje nje
 
pole kaka ningekuwa na uwezo ningekulipia hata nusu ya ada. ebu jaribu kuwatafuta matajiri kama 3 wa hapa bongo wakusaidie.
 
copy AshaDii ana PhD ya kutembeza bakuli.
 
Last edited by a moderator:
Nimevutiwa sana na huyu jamaa hasa kwa uwezo, juhudi na kutokukata tamaa.
Binafsi ninaona kuna issue mbili, yaani issue ya kupata Ada mwaka huu lakini issue ya kupata ada kwa mwaka wa
Pili na watatu plus pesa ya kujikimu wakati wote akiwa chuoni. It is a big challenge.

Binafsi ninaweza kukusaidia kwa ushauri madhubuti, lakini kama ukiweza kufafanua haya maswali
1/Kwa sasa unafanya nini kimaisha?
2/Una miliki kitu gani cha thamani?
3/Una familia(mke au mtoto)?
4/Uko karibu kiasi gani na jamii inayokuzunguka(marafiki, jamaa, taasisi za kiimani, kisiasa au kiuchumi)?
5/Umewezaje kupata hizo laki tatu?
6/Una ujuzi gani wa kimaisha?
7/Toka umalize shule mpaka sasa umekuwa unafanya nini?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…