Nina wasiwasi kuna Bia za kuchakachua hapa mjini

Nina wasiwasi kuna Bia za kuchakachua hapa mjini

Ukinywa serengeti lite nyingi lazma utaharisha [emoji1787][emoji1787][emoji1787] huwa haziivi maana ndio bia inanyweka sana Dar.
Serengeti Light si za Wadada zile.
Wanaume watumie japo Casttle Light inafaa.
Kuliko Mdada anywe Serengeti Light na Mkaka nawe unywe Serengeti Light haipendezi kwakweli.
 
Kuna namna vyombo vinavyohusika vitupie jicho maana nchi hii kuna matapeli wengi sana na ndio maana magonjwa ya Figo , ini na Cancer

yamezidi kuongezeka sana
Duh 🙄
Hatari sana
 
Sina nia ya kuwatisha wanywaji wenzangu wa bia. Lakini nimekuwa ninafanya ulinganifu ninapokunywa bia nikiwa Kenya na nikiwa Tz. Mfano ladha ya Heineken ya Kenya ni tofauti .

Pia Heineken ya sehemu kama Serena hotel au Supermarket kubwa unakuta ina utofauti wa Ladha na hata harufu na Heineken zinazouzwa kwenye Baa za mitaaani.

Za mtaani asilimia kubwa zimetulia hazina vipovu vilivyochangamka, pia zina harufu na hata umwe vipi hucheuwi hata kidogo, lakini za Serena hotel na Big Supermarket ambazo zina ladha, zinatoa vipovu vilivyochangamka na ukinywa unacheua.

Kuna namna vyombo vinavyohusika vitupie jicho maana nchi hii kuna matapeli wengi sana na ndio maana magonjwa ya Figo , ini na Cancer

yamezidi kuongezeka sana
we unaongelea bia mbali kote huko,
watu wanachakachua mpaka maji ya kunywa juzi nmeenda sehemu nmekunywa maji ya kilimanjaro ya 500 ladha yake bora hata ya bombani maana kama yana vijichumvi
 
we unaongelea bia mbali kote huko,
watu wanachakachua mpaka maji ya kunywa juzi nmeenda sehemu nmekunywa maji ya kilimanjaro ya 500 ladha yake bora hata ya bombani maana kama yana vijichumvi
Nchi hii jamani. Bahati mbaya sana inaonyesha vyombo vinavyohusika na usalama wa vyakula na vinywaji havijalichukulia kwa uzito suala hili. Kuna uwezekano mkubwa watu wanapata maradhi ya Ini, Figo nk sababu hii.
 
Serengeti Light si za Wadada zile.
Wanaume watumie japo Casttle Light inafaa.
Kuliko Mdada anywe Serengeti Light na Mkaka nawe unywe Serengeti Light haipendezi kwakweli.
Hahahahah wadada bia zao ni Redds, Savanah, Desperado na Flying fish. Wine zao ni Saint Anna na Robertson.

Serengeti Lite ni Unisex beer ile.
 
Hii ni kweli kabisa. Na hasa heineken wanachakachua sana, hii kitu imenifanya niache kunywa bia kabisa.

Kuna siku nimenunua heineken naweka kwenye glass lkn huoni lile povu nilozoea, kuinywa sasa radha hamna kabisa. Wanatunywesha mambo ya ajabu sana siku hizi
Mimi ilinikuta kwenye St. Anna. Ilikuwa Sumbawanga, Ile kumimina kwenye glass ikaanza kufoka povu kama bia. Aisee niliacha kunywa zile wine.
 
Back
Top Bottom