Nina wasiwasi na haya maamuzi ambayo Mungu aliyafanya, hapa alikosea

The Humble Dreamer

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
8,011
Reaction score
11,447
Salaam Members!

Tumekuwa tukisikia toka kwa wafuasi wake kua Mungu ni mwema sana kwa watu wake hapa duniani.

Lakini Mungu huyu kuna maamuzi aliyafanya ambayo ni mengi na yanatia shaka kwanini aamue wachache wapate adhabu kwaajili ya wengine.

Nina mifano miwili:
  • Kitendo cha Mungu kumuumba Yuda Iskariote halafu baadaye Mungu huyo huyo anamtia hatiani kwa kumsaliti Yesu.
Biblia inasema Yesu kwa kuongozwa alimteua pia Yuda Iskariote kama mtume wake na mda huo Yesu anajua fika ninaye msaliti tayari na ataingia hatiani kwa kupitia mtego wa fedha.

Ina maana kweli Mungu alishindwa kufikiria njia mbadala ya mwanae kwenda msalabanii isipokua kumtenga Yuda ndiyo aje amsaliti baadaye?
Yuda aliingia kwenye dhambi huku Mungu ndiyo amesababisha hayo yote tena kwa makusudi kabisa.

Mungu amesema kuna moto wa milele, Mungu huyo ametengeneza mazingira ya Yuda kuingia kwenye dhambi na tayari hukumu iko wazi.
Yuda Iskariote amepata hukumu isiyostahili kwa mipango ya Mungu.

  • Kitendo cha Mungu kumfanya Farao kua na moyo mgumu kuwaachia wana wa Israel.
Mungu alikosea kumfanya Farao akatae kuwaachia wana wa Israel wa hiari huku akilenga zaidi maslahi yake binafsi hasa ya yeye kujulikana.
Unafanya jambo jema ndiyo watu wanakuelewa, lakini yeye anamuingiza kwenye makosa kwa makusudi kabisa akiwa anajua na anajua hukumu yake itakuaje halafu baadaye unaambiwa yeye ana upendo.

Hivi upendo wa Mungu unatoka wapi wakati anatengeneza mazingira yeye mwenyewe ya watu aliowaumba kufanya makosa ili tu yeye afaidike na makosa yao?

Kulikua na haja gani ya kumuumiza Farao na watu wa Misri kiujumla wakati angeweza tu kumfanya Farao awe na moyo mwepesi na kuwaachia Waisraeli wakaondoka?

Mungu aliua watu wa Misri ili watu wake kwa upendeleowa taifa la Israel lipate kufaidika, na wakati wote ni yeye amewaomba.
Cha ajabu, Mungu alikuja kuua watu wengi kwenye ile bahari tena kwa makusudi kabisa.

Kinachosikitisha zaidi ni wafuasi wa Mungu walishangilia na wamekua wakishangilia hivi kitendo vya kionevu kwa wengine na wakati ni binadamu wenzao.

Wafuasi wa Mungu hawana upendo.

Kuna mifano mingi sana kwenye Biblia hasa ya vita, Mungu anaandaa watumishi wake waende vitani na yeye anawaaminisha atawasaidia kuua adui zao.
Kweli Mungu anakosa njia mbadala za Amani za kutatua mgogoro kati ya jamii 2 au zaidi tofauti?

Maamuzi anayofanya Mungu kwa namna nyingine anapendelea, na huo ni ukweli.
Zipo njia mbadala za kutafuta suluhu ya jambo lakini siyo kumuumiza na kumtia hatiani mtu kwa hukumu kali toka kwa Muumba wake.
 
mkuu ungefanya pia kupitia ule uzi wa makosa kumi aliyofanya mungu. naona wewe umeweka machache.
 
Afadhari akili zinaanza kuwapata na mnahoji!, vitu kama hivi wengine ndo vilitushinda na ndio maana siamini hilo likitabu na dini husika!, endeeleni kusoma na mfikiri vyema yapo mambo mengi sana mtagundua na mtajua dini ni ujinga wa karne!.
 
Kuna jambo Moja unafurahisha sana, Kipimo cha "Right & Wrong" wewe unakijua? Kwa maana nyingine ni sawa na kuhoji 'hapa Mungu ametembea kilomita nyingi sana' wakati huo hauna wala haujui kama kuna kitu kinaitwa 'Ruler'. Mungu ndiye SI units ya 'Wema na utakatifu' yeye ndiye anayeijua mipango yake ambayo kwa akili zake wewe mwanadamu hauwezi kudadavua hata theluthi ya maamuzi yake! Sembuse kuhoji kuhusu utendaji wake?😀 Akili zake hazichunguziki, huenda limits ya mwanadamu kufikiri ni katika 3D ila Mungu ni infinityD. Kwa maana hiyo unapohoji unahoji katika context gani?
 
muumba akasei, ndege imeanguka huko india walio fariki tunasema muumba kawapenda zaidi na aliye pona nae anamshukuru muumba kwa wema wake
 
Dah ukiwa Muislamu raha sanaaa

Tokeni huko kwenye fikra potofu njooni kwenye Nuru
 
Mungu ndiye SI units ya 'Wema na utakatifu' yeye ndiye anayeijua mipango yake ambayo kwa akili zake wewe mwanadamu hauwezi kudadavua hata theluthi ya maamuzi yake
Tatizo lako linaanzia hapa kwa kumtetea Mungu kua ni mwema tu, kwanini inazuiwa kuhojiwa upande wake wa pili anapokosea?
Wewe kwa Ajili yako hiyo, kila maamuzi anayofanya Mungu ni sahihi kwa msingi upi hasa ukizingatia yeye ni wa haki kama alivyonadiwa kwenye vitabu vyake?
 
MUNGU HAYUPO NA HAJAWAHI KUWEPO WEWE NI KIHEREHERE CHAKO TU KUAMINI UJINGA
 
Tatizo lako linaanzia hapa kwa kumtetea Mungu kua ni mwema tu, kwanini inazuiwa kuhojiwa upande wake wa pili anapokosea?
Wewe kwa Ajili yako hiyo, kila maamuzi anayofanya Mungu ni sahihi kwa msingi upi hasa ukizingatia yeye ni wa haki kama alivyonadiwa kwenye vitabu vyake?
Nadhani bado haujanielewa. Tatizo ni hiyo akili unayotumia kuhojia, ni akili hii hii ambayo haiwezi hata kuumba DNA au kuumba uhai hata wa sisimizi? Au unatumia akili gani kuhoji? Your brain thinking & reasoning is extremely limited. Reasoning za MUNGU ni beyond our understanding.Unaposema anakosea ni kwa reference ipi? Yeye ndiye SI Unit ya right/wrong, Neno "kosa" yeye ndiye anayejua definition yake, Wewe unahoji katika scale gani? God's scale au human scale?
 
Back
Top Bottom