Nina wasiwasi na haya maamuzi ambayo Mungu aliyafanya, hapa alikosea

Nina wasiwasi na haya maamuzi ambayo Mungu aliyafanya, hapa alikosea

Nipe majibu ya kiutuuzima
Majibu yapo kwenye kitabu cha mwanzo tumia akili kutambua sababu za mambo ....kwenye kitabu cha mwanzo tunasikia mungu akisema "kutakuwa na uadui baina ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka"....kisha kwenye injili tunasikia mungu anasema "walio wangu watasikia sauti yangu hata mmoja hata achwa apotee " sasa hapa tunagundua kuwa kuna uzao wa shetani na huo uzao siyo majini tu hata baadhi ya wanadamu ni uzao wa shetani maana tunajua kuna binadamu watatupwa motoni pia. Hivyo kinacho endelea duniani ni kutimia yale maneno ya vita baina ya uzao wa nyoka na wamwanamke ...hivyo kuuliza kuwa kama Mungu yupo kwanini wanadamu wanauana wanatesana wanachukiana nk ni kutokujua maandiko. Kwa sababu uadui baina ya haki na batili kausema mungu mwenyewe kwenye vitabu vyenu kuwa utakuwepo siku zote za maisha ya mwanadamu.....ukitumia akili utajua kuwa siyo kila nafsi ya mwanadamu imepandwa na mungu bali shetani utia nafsi za uzao wake kwenye miili ambayo mungu ajatia nafsi ...ndiyo maana imeandikwa kuwa pando la mungu hakuna litakalo tupwa motoni bali watapatikana wote na kuokolewa asiwepo hata mmoja wa kutupwa motoni ...
 
Swala la kuabudu ni "myth" , Mungu au shetani ni fikra zako ..huwezi ukasema kati ya Mungu au shetani lazima aabudiwe mmojawapo, kuna ambaye haabudu yeyote yule hivyo conclusion yako siyo sahih

Swala la kuabudu ni "myth" , Mungu au shetani ni fikra zako ..huwezi ukasema kati ya Mungu au shetani lazima aabudiwe mmojawapo, kuna ambaye haabudu yeyote yule hivyo conclusion yako siyo sahihi
Ndugu, laiti kipindi hicho mama yako akiwa na ujauzito wako angelijua kuwa analeta duniani kiumbe ambaye atamkataa Mungu na uwepo wake basi huenda angekutupa chooni,
Inasikitisha sana asee, hivi nyie ndugu zetu mnaojitoa akili kusema hakuna Mungu hata Shetani anawacheka japo niyeye anayewapotosha.
Hamfikirii hata kujiuliza kuwa nyie ni nani, kabla ya hapo mlikuwa nani na baada ya hapo utakuwa nani?,
Viumbe vyoote alivyoviumba Mwenyezi Mungu akiwemo mimi na wewe bado tuu huoni hilo?,
Hujiulizi hvyo unavyoviona vimetokeaje?,
Hujiulizi kwann ndege anaweza kuruka angani akaenda kwa mbawa zake lakn wewe huwezi?, Kwann mamba anaweza kuishi kwenye maji lakn wew ukiwekwa mule ndani na nusu saa unakufa?, bado hujioni pumzi unayovuta na kuitoa imetoka wapi na nani kakuwekea hyo hewa?, Mungu kakuumba wewe binadamu na sio mende muda huu ungekuwa chooni unasubiri vinyesi ule ili uishi?, Huyo Mungu alokuumba wewe akakufanya kuwa bora na akakupa mamlaka ya kuwa mtawala na kiongozi wa viumbe wengine wote leo hii unamvimbishia kifua eti unam challenge?,
Sikia, huwezi, hutaweza na hautakaribia kuweza kumchallenge Mwenyezi Mungu na hata kama uungane na wenzako muwe wengi kuliko binadamu wote ulimwenguni hamtoweza kumchallenge Mungu, maana nyie ni viumbe dhaifu mnooo, binadamu hatuna dhamani yoyote sisi ila cgenye thamani kwetu ni ROHO alotuwekea Mwenyezi Mungu ambayo hakuna anayejua ipoje maana inatokana nayeye.
Sisi ni dhaifu mnoo, tena mnoo na usijaribu tena wala kufuata mkumbo kwa wenzako mnaojidai kila siku humu JF kumdhihaki na kumchallenge Mungu utadhani amekuwa babu yenu.
Halafu, kwann mje kuuliza maswali yenu huku ya kumchallenge Mungu?, nyie simushamfanya ni mtani wenu?, muulizeni hukohuko kwenye vikao vyenu.
Yeye ndie Muumba wa kila unachokiona na usichokiona, na yeye ni mpoole na mwenye hekima, anawavumilia huenda kuna siku mtajitambua na mtatubia kwake naye ni mwenye huruma atawasamehe. Ila ikiwa mtashupaza shingo zenu, yeye ni mkali na mwenye adhabu zisizovumilika, anakuangalieni na muda wowte akiamua atawaonyesha kuwa yeye ndo Jabbar.
 
Yuda hakumsaliti Yesu.
Aliyemsaliti Yesu ni mtu alikuwa anaitwa Yuda Ihariot,ambaye alikuwa amekasirika demu wake alichukiliwa na Yesu na kufanyiwa mlokoke.
Soma kitabu

And they called his name Emmanuel. I am sananda pdf.
 
Majibu yapo kwenye kitabu cha mwanzo tumia akili kutambua sababu za mambo ....kwenye kitabu cha mwanzo tunasikia mungu akisema "kutakuwa na uadui baina ya uzao wa mwanamke na uzao wa nyoka"....kisha kwenye injili tunasikia mungu anasema "walio wangu watasikia sauti yangu hata mmoja hata achwa apotee " sasa hapa tunagundua kuwa kuna uzao wa shetani na huo uzao siyo majini tu hata baadhi ya wanadamu ni uzao wa shetani maana tunajua kuna binadamu watatupwa motoni pia. Hivyo kinacho endelea duniani ni kutimia yale maneno ya vita baina ya uzao wa nyoka na wamwanamke ...hivyo kuuliza kuwa kama Mungu yupo kwanini wanadamu wanauana wanatesana wanachukiana nk ni kutokujua maandiko. Kwa sababu uadui baina ya haki na batili kausema mungu mwenyewe kwenye vitabu vyenu kuwa utakuwepo siku zote za maisha ya mwanadamu.....ukitumia akili utajua kuwa siyo kila nafsi ya mwanadamu imepandwa na mungu bali shetani utia nafsi za uzao wake kwenye miili ambayo mungu ajatia nafsi ...ndiyo maana imeandikwa kuwa pando la mungu hakuna litakalo tupwa motoni bali watapatikana wote na kuokolewa asiwepo hata mmoja wa kutupwa motoni ...
Kumbe Mgalatia upo ,mzee wa kujificha
 
Dah ukiwa Muislamu raha sanaaa

Tokeni huko kwenye fikra potofu njooni kwenye Nuru
Wote mmepotoka tu.. Tofauti ni lugha tu hapo. Watu mnaamini ukifa unafufuka tena alaf unaenda kupewa mabikra 72.. Inahitaji ujinga wa hali ya juu sana kuamini huu utopolo
 
Salaam Members!

Tumekuwa tukisikia toka kwa wafuasi wake kua Mungu ni mwema sana kwa watu wake hapa duniani.

Lakini Mungu huyu kuna maamuzi aliyafanya ambayo ni mengi na yanatia shaka kwanini aamue wachache wapate adhabu kwaajili ya wengine.

Nina mifano miwili:
  • Kitendo cha Mungu kumuumba Yuda Iskariote halafu baadaye Mungu huyo huyo anamtia hatiani kwa kumsaliti Yesu.
Biblia inasema Yesu kwa kuongozwa alimteua pia Yuda Iskariote kama mtume wake na mda huo Yesu anajua fika ninaye msaliti tayari na ataingia hatiani kwa kupitia mtego wa fedha.

Ina maana kweli Mungu alishindwa kufikiria njia mbadala ya mwanae kwenda msalabanii isipokua kumtenga Yuda ndiyo aje amsaliti baadaye?
Yuda aliingia kwenye dhambi huku Mungu ndiyo amesababisha hayo yote tena kwa makusudi kabisa.

Mungu amesema kuna moto wa milele, Mungu huyo ametengeneza mazingira ya Yuda kuingia kwenye dhambi na tayari hukumu iko wazi.
Yuda Iskariote amepata hukumu isiyostahili kwa mipango ya Mungu.

  • Kitendo cha Mungu kumfanya Farao kua na moyo mgumu kuwaachia wana wa Israel.
Mungu alikosea kumfanya Farao akatae kuwaachia wana wa Israel wa hiari huku akilenga zaidi maslahi yake binafsi hasa ya yeye kujulikana.
Unafanya jambo jema ndiyo watu wanakuelewa, lakini yeye anamuingiza kwenye makosa kwa makusudi kabisa akiwa anajua na anajua hukumu yake itakuaje halafu baadaye unaambiwa yeye ana upendo.

Hivi upendo wa Mungu unatoka wapi wakati anatengeneza mazingira yeye mwenyewe ya watu aliowaumba kufanya makosa ili tu yeye afaidike na makosa yao?

Kulikua na haja gani ya kumuumiza Farao na watu wa Misri kiujumla wakati angeweza tu kumfanya Farao awe na moyo mwepesi na kuwaachia Waisraeli wakaondoka?

Mungu aliua watu wa Misri ili watu wake kwa upendeleowa taifa la Israel lipate kufaidika, na wakati wote ni yeye amewaomba.
Cha ajabu, Mungu alikuja kuua watu wengi kwenye ile bahari tena kwa makusudi kabisa.

Kinachosikitisha zaidi ni wafuasi wa Mungu walishangilia na wamekua wakishangilia hivi kitendo vya kionevu kwa wengine na wakati ni binadamu wenzao.

Wafuasi wa Mungu hawana upendo.

Kuna mifano mingi sana kwenye Biblia hasa ya vita, Mungu anaandaa watumishi wake waende vitani na yeye anawaaminisha atawasaidia kuua adui zao.
Kweli Mungu anakosa njia mbadala za Amani za kutatua mgogoro kati ya jamii 2 au zaidi tofauti?

Maamuzi anayofanya Mungu kwa namna nyingine anapendelea, na huo ni ukweli.
Zipo njia mbadala za kutafuta suluhu ya jambo lakini siyo kumuumiza na kumtia hatiani mtu kwa hukumu kali toka kwa Muumba wake.
Mnafanta makosa halafu mnamsingizia Mungu. Kwanza Mungu gamumjui tuanzie hapo kwanza!
 
Wote mmepotoka tu.. Tofauti ni lugha tu hapo. Watu mnaamini ukifa unafufuka tena alaf unaenda kupewa mabikra 72.. Inahitaji ujinga wa hali ya juu sana kuamini huu utopolo
Iogope sana iyo siku unayoidharau
 
Back
Top Bottom