Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
Kauli mbiu ni kufanya uzalishaji vijijini, na kuleta mauzo mjini. Kwa yeyote atakayependa wazo langu, anaruhusiwa kulitekeleza; elimu haina mwisho.
Nitaanza hivi:-
Nawakaribisha kwa mawazo.
NB: Kuhusu wafanyakazi, nitawatengenezea mpango kazi wa kila siku, na kila siku jioni lazima wafanye presentation; ambaye atakuwa hajafanya chochote, ataenguliwa.
Nitaanza hivi:-
- Nitafungua kampuni yenye jina 'Equation x agricultural adventure'
- Nitatafuta binti wa kazi mpambanaji kweli kweli mwenye cheti cha kilimo
- Nitampiga semina ya wiki moja, ili aweze kuelewa ndoto zangu
- Nitampa safari ya kutembelea vijiji 10 vyenye ardhi ya rutuba katika mikoa 2, kwa kuanzia.
- Nitaingia mkataba wa miaka 2 au 5 kwa kukodi mashamba kwa kila kijiji nitakapofanikisha
- Itakuwa vizuri kama nitapata kuanzia ekari 5 kwa shamba
- Sehemu ambayo mkataba utaanzia miaka 5, nitapambana nichimbe kisima ili kilimo cha umwagiliaji kiwe rahisi.
- Wafanyakazi wa shambani watakuwa wanakijiji, pamoja na mtaalamu mmoja atakayekuwa anawazungukia.
- Nitalima zao la muda mfupi ambalo tayari soko lake nimeshaliona.
- Mi nitakuwa napambana mjini pamoja na kujibana, huku fedha zangu zikiwa zinaenda kijijini kwenye kilimo
- Baada ya mavuno, mazao yataletwa mjini kwa mauzo; nitatafuta kijana wa cheti cha mauzo.
- Mafanikio yakiwa vizuri, nitaongeza wigo kwa kuongeza mikoa mingine.
- Naimani, huu mradi utanilipa
Nawakaribisha kwa mawazo.
NB: Kuhusu wafanyakazi, nitawatengenezea mpango kazi wa kila siku, na kila siku jioni lazima wafanye presentation; ambaye atakuwa hajafanya chochote, ataenguliwa.