Equation x
JF-Expert Member
- Sep 3, 2017
- 33,679
- 49,841
- Thread starter
- #61
Kwa uzoefu wenu, ni mita ngapi zinafaa kupata maji mengi kwa ajili ya umwagiliajiImefungwa pump ya horse power 5.5 ,
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Kwa uzoefu wenu, ni mita ngapi zinafaa kupata maji mengi kwa ajili ya umwagiliajiImefungwa pump ya horse power 5.5 ,
Kabda ya kuchimba tunafanyaga underground water survey , itaonyesha depth ya maji, ila kwa experiance kwa pwani ya morogoro road inaanzia mita 100 hadi 160 , kwa pwani ya kilwa road kwenda kusini water table inaanzia mita 70 nakuendelea.Kwa uzoefu wenu, ni mita ngapi zinafaa kupata maji mengi kwa ajili ya umwagiliaji
Nimekupata mkuuKabda ya kuchimba tunafanyaga underground water survey , itaonyesha depth ya maji, ila kwa experiance kwa pwani ya morogoro road inaanzia mita 100 hadi 160 , kwa pwani ya kilwa road kwenda kusini water table inaanzia mita 70 nakuendelea.
Kwani kuzeeka kwenye ajira ni dhambi,nilipoona uzi wako nilidhani unajitambua kumbe sivyo-katikabhii dunia lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu kila MTU akijiajiri unadhani wewe na hizo projects zako utafanikiwaje???Inawezekana mkuu, kuna rafiki yangu nimekutana naye anafanya hii kazi; anawekeza m3 anapata hata zaidi ya mara 2. Jifunze kuwa karibu na waliofanikiwa, upate ujuzi. Ukiwa na marafiki wengi walioajiriwa hawatakusaidia kitu, zaidi za kukuambia kila kitu hakiwezekani, ndio maana wanazeeka kwenye kuajiriwa.
Nakubaliana na hoja yako; entrepreneurs vs employeesKwani kuzeeka kwenye ajira ni dhambi,nilipoona uzi wako nilidhani unajitambua kumbe sivyo-katikabhii dunia lazima kuwe na mgawanyo wa majukumu kila MTU akijiajiri unadhani wewe na hizo projects zako utafanikiwaje???
Wakati wewe unajiajiri kumbuka kuna waajira lukuki wanafanya mambo au vitu Vinci kwa manufaa yako na jamii yako.Kuna watu wanafundisha ndugu zako,kuna watu wnatibu ndugu zako,kuna waajiriwa wankulinda huku wewe ukiwa umelalal na hiyo miradi yako,kuna watu wanafikiria namna ya kujenga barabara utakazo pitisha mazao ya hiyo miradi yako,kuna watu wanatengeneza Sera we na ndugu zako mpate dawa,umeme &maji,kuna watu wanakaa na kutengeneza sheria mbalimbali zenye manufaa kwako na ndugu zako.
Ili hao vijana wako na mdada wawe comited wape share hata ya nguvu kazi tu wajisikie nao ni wamiliki.Kwa mwanzoni, nitaanza na vijana wawili wenye certificate; mmoja kilimo, mwingine mauzo; hawa kazi yao ni kuzunguka kwenye masoko na shambani. Kwa kila shamba kijijini, nitatafuta mzee mtu mzima moja ambaye atakuwa anaripoti kwangu kimawasiliano.
Hawajui wabongo huyu😅Hao wafanya kazi utalia labda uweke Managment ya Wahindi,
Tatizo la wabongo ni roho ya kwanini tu hata umlipe Million 100 bado atataka akupige kwa sababu cha kwanza anajiuliza kwani we anakuingizia bei gani? Akipiga hesabu anakuingizia billion1 mfano atawaza kwanini we umpe 100 tu hapo ndipo hujuma zinaanza!Ili hao vijana wako na mdada wawe comited wape share hata ya nguvu kazi tu wajisikie nao ni wamiliki.
Hii mbinu inatumiwa ba HUAWEI company, kila mfanyakazi mwenye tija alipewa hisa zake na kuwa mmiliki, nafikiri watanzania tukiiga hii mbinu tutapunguza changamoto ya uvivu na uaminifu.
mkoani hiyo haifiki kwa mm napokaa huwa ni 100 feet huko pwani wanachimba chini Sana coz wanatafuta fresh water ambayo ipo chini SanaKatika hizo mita 200, maji yanakuwa yanapanda yenyewe au mpaka yavutwe na pump
Utaanza kukwamishwa na wafanya kazi, Utawapata hao wasomi watasafirinkwenda vijijini nauri juu yako pesa ya kula njiani na wakiwa huko, guest house pa kulala,kumbuka wanajiita wasomi hawali mihogo Wala hawajui kujibana, hawataki kwenda porini. Wewe upo dar unaelekeza kwa simu na wao wapo pale center wanaelekeza vibarua shambani kwa simu. Unakuja kushtuka palizi halikufanyika vizuri, wamepanda kwa kutupa tupa ,dawa wameweka nusu ili wakupige Cha juu, nk watumishi kwa Tanzania Bado Sana wanatukwamishaNi kweli mkuu,nikipata nguvu kazi sahihi, kazi itafanyika mkuu
Ulipitia changamoto zipi mkuu, ili tujifunze?Kilimo kwa Tanzania hii Lima ili upate chakula lakini ki biashara hadi sumri aliyeacha mabasi akajitosa mazima Bado tu kinamsumbua.
Mwaka jana nimejipinda nikawekeza million tatu (3m) nimetoa Laki tatu hapo sijahesabu gharama ya muda wangu. Ilifika mahala nikataka kuyaacha mazao yafie shambani lakini nikapambana ili shule ifike mwisho nipate ushuhuda
Nimejifunza kitu ... do you mean kama ndo unaaza kupromoti mtandaoni peketake haitishi ..lazma uwe unafahamika na kuaminika cyoNchi za Jirani na Wananuzi wakubwa hawanunui kwako sababu tu una mzigo / mali bali pia long term relationship kwamba wewe unaaminika, unaweza uka-deliver na mzigo wako sio wa kubabaisha (ndio maana madalali hawaishi wala hawataisha) people like dealing with people they know....
Kwahio kwanza anza kwa ku-cultivate soko kabla ya production..., Unaweza ukaanza kutafuta market wakati hauna shamba..., mwaka huu tu Mwanzoni kuna wakulima walikosa soko la mahindi na mchele ulikuwa haujapanda kwa miaka mitatu mfululizo ungeweza kutafuta mali na kuuza kwa hilo soko lako la nje
Hata safari ndefu huanza kwa hatua moja..., mafanikio utakayopata mwaka huu yatakuwa hafifu kulingana na utakayokuwa umepata mwaka kesho ikiwa kila kitu kitaenda sawa..., Ukiuzia watu mwaka huu bidhaa na zikawa nzuri mwaka kesho watachukua zaidi na kuambiana fulani mzigo ni mzuri (unajenga jina na mahusiano)Nimejifunza kitu ... do you mean kama ndo unaaza kupromoti mtandaoni peketake haitishi ..lazma uwe unafahamika na kuaminika cyo
Amka kumekucha ila kama ndoto haitotimia usisite kurudi kulala Ili uote upyaKauli mbiu ni kufanya uzalishaji vijijini, na kuleta mauzo mjini. Kwa yeyote atakayependa wazo langu, anaruhusiwa kulitekeleza; elimu haina mwisho.
Nitaanza hivi:-
- Nitafungua kampuni yenye jina 'Equation x agricultural adventure'
- Nitatafuta binti wa kazi mpambanaji kweli kweli mwenye cheti cha kilimo
- Nitampiga semina ya wiki moja, ili aweze kuelewa ndoto zangu
- Nitampa safari ya kutembelea vijiji 10 vyenye ardhi ya rutuba katika mikoa 2, kwa kuanzia.
- Nitaingia mkataba wa miaka 2 au 5 kwa kukodi mashamba kwa kila kijiji nitakapofanikisha
- Itakuwa vizuri kama nitapata kuanzia ekari 5 kwa shamba
- Sehemu ambayo mkataba utaanzia miaka 5, nitapambana nichimbe kisima ili kilimo cha umwagiliaji kiwe rahisi.
- Wafanyakazi wa shambani watakuwa wanakijiji, pamoja na mtaalamu mmoja atakayekuwa anawazungukia.
- Nitalima zao la muda mfupi ambalo tayari soko lake nimeshaliona.
- Mi nitakuwa napambana mjini pamoja na kujibana, huku fedha zangu zikiwa zinaenda kijijini kwenye kilimo
- Baada ya mavuno, mazao yataletwa mjini kwa mauzo; nitatafuta kijana wa cheti cha mauzo.
- Mafanikio yakiwa vizuri, nitaongeza wigo kwa kuongeza mikoa mingine.
- Naimani, huu mradi utanilipa
Nawakaribisha kwa mawazo.
NB: Kuhusu wafanyakazi, nitawatengenezea mpango kazi wa kila siku, na kila siku jioni lazima wafanye presentation; ambaye atakuwa hajafanya chochote, ataenguliwa.