Nina wazo la kufanya hii 'project' kwa mwaka 2022

Kilimo kina changamoto nyingi sana, kuhusu soko mazingira yote nitayatumia; nita-email mazao yangu kwa nchi za jirani, fb, youtube na mitandao mengineyo
Nchi za Jirani na Wananuzi wakubwa hawanunui kwako sababu tu una mzigo / mali bali pia long term relationship kwamba wewe unaaminika, unaweza uka-deliver na mzigo wako sio wa kubabaisha (ndio maana madalali hawaishi wala hawataisha) people like dealing with people they know....

Kwahio kwanza anza kwa ku-cultivate soko kabla ya production..., Unaweza ukaanza kutafuta market wakati hauna shamba..., mwaka huu tu Mwanzoni kuna wakulima walikosa soko la mahindi na mchele ulikuwa haujapanda kwa miaka mitatu mfululizo ungeweza kutafuta mali na kuuza kwa hilo soko lako la nje
 
Nakubaliana na wazo lako, kupata mtu atakayejituma bila kuwa mbia ni changamoto
 
Nitafanyia utafiti mkuu, nitaanza na zao la viazi mviringo
 
Mwachie mke
 
Uwekezaji wa Kilimo Kwa mtanzania ambaye ni wakipato Cha kati ni mgumu
 
Kwa mwanzoni, nitaanza na vijana wawili wenye certificate; mmoja kilimo, mwingine mauzo; hawa kazi yao ni kuzunguka kwenye masoko na shambani. Kwa kila shamba kijijini, nitatafuta mzee mtu mzima moja ambaye atakuwa anaripoti kwangu kimawasiliano.

All the best Mkuu
Ukiendelea kwa muda ulete mrejesho
 
  • Mi nitakuwa napambana mjini pamoja na kujibana, huku fedha zangu zikiwa zinaenda kijijini kwenye kilimo.... yawezekanaukawa na wazo zuri sana, lakini hiyo👆 point ya hapo juu ni tayari kosa namba moja la kiufundi.
 
  • Mi nitakuwa napambana mjini pamoja na kujibana, huku fedha zangu zikiwa zinaenda kijijini kwenye kilimo.... yawezekanaukawa na wazo zuri sana, lakini hiyo[emoji115] point ya hapo juu ni tayari kosa namba moja la kiufundi.

Haya ndio yale mambo ya kilimo cha simu!
Wewe uko mjini kazi kupiga simu tu mwisho wa siku ni msiba!
 
Kama hauna milioni 50 kwa hiyo project yako unajidanganya
Nitaanza kidogo kidogo; kuna baadhi ya vijiji kukodi shamba haizidi 50,000/= Na kuna mikoa mingine shamba la ekari moja linauzwa 200,000 au chini ya hapo
 
Mkuu yote hiyo ni mipango mizuri.ukitaka ufanikiwe jibu rahisi na lazma wewe uwe front.habari ya kuambiwa dawa imeisha tuma ela.utakuja kulia vibaya tuulize sisi tuliokuwa huku
Nitajitahidi kuwa makini sana kwenye kutengeneza timu, pia kubuni mfumo wa kudhibiti hizo changamoto. Kwa asili ya mwanadamu, bila kuwekewa mfumo wa kumdhibiti lazima atasababisha hasara tu, ndio maana hata makazini kunakuwa na miongozo mingi, kanuni, ukaguzi n.k hiyo yote ni kumdhibiti binadamu.
 
Hao wafanya kazi utalia labda uweke Managment ya Wahindi,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…