Nina wazo la kufanya hii 'project' kwa mwaka 2022

Kwa mwanzoni, nitaanza na vijana wawili wenye certificate; mmoja kilimo, mwingine mauzo; hawa kazi yao ni kuzunguka kwenye masoko na shambani. Kwa kila shamba kijijini, nitatafuta mzee mtu mzima moja ambaye atakuwa anaripoti kwangu kimawasiliano.
Hao wasomi utalia,
 
Bado utapigwa tu, achana na Watanzania wewe hizo kuna watu wamejaribu na wakalia,
 
Try to scale down your project blood! nasema hivi kwa maana imekuwa ngumu sana kupata one to one relationship kati ya plan and result

Mipangalio yako ni mizuri lakini kwa kuitazama kwa haraka hii inaonekana ni massive project ambayo itabidi iwe handled professionally and not primitively.

Kama uta scale down project yako, kwanza utakuwa na uwezo wa kuretreat pale mambo yakienda kinyume na matarajio.Pili, utakuwa na urahisi wa kurudi nyuma na kuredefine your project.

Mwisho kabisa, kila kitu kinawezekana but you need to be patient. Otherwise,all the best
 
Nitaanza na ekari 10 kwanza, kwa kilimo cha kiazi mviringo; nitatafuta binti aliyesomea certificate ya kilimo kwa ajili ya kutembelea mashambani na kusimamia. Nitatumia muda mwingi kupata mtu sahihi
 
Nitaanza na ekari 10 kwanza, kwa kilimo cha kiazi mviringo; nitatafuta binti aliyesomea certificate ya kilimo kwa ajili ya kutembelea mashambani na kusimamia. Nitatumia muda mwingi kupata mtu sahihi
Kwa ekari kumi ni kiwango kizuri na zao ulilochagua nadhani linaweza kuwa halina changamoto nyingi(japo sina ujuzi mkubwa katika kilimo)

Mwisho kabisa study market kwa uzuri maana wote wenye kulima linapifika jambo la nauza wapi na napata nini ndio umekuwa mtihani.

Market inabadilika kila sekunde unaweza kuwa umepata soko lako la uhakika gafla mambo yanakubadilikia.I mean, ujipange kwa rafu zote.
 
Sijui uwezo wako lakini..tambua kuchimba kisima kirefu sehemu nyingi Ni zaidi ya milioni 8..
Kuna kufunga sola za nguvu au generator na pump za maana kuvuta maji..
Kuna mdau kasema Ni project ya milioni 50 inawezekana kabisa..
Mimi naona utafanikiwa kama utafanikiwa kutatua chngamoto ya usimamizi..
 
Kuchimba kisima kirefu, itafuata baada ya kuona mafanikio katika majaribio ya ekari chache za mwanzo
 
Kila kitu kinawezekana mkuu kikubwa ni kutokata tamaa, mafanikio ya kweli yanapitiaga up down yote ni kujifunza zaidi, kikubwa kabda ya kuanza kuinvest ,nenda kafanye kuishi kwenye hizo project, tafuta connection ya watu wanaofanya hizo project, utajifunza kitu.

Tenda za usambazaji wa maji usisite kututafuta tukupe ushauri wa kitaalamu.
 
Gharama zenu za uchimbaji zikoje mkuu?
 
Gharama zenu za uchimbaji zikoje mkuu?
Gharama za uchimbaji inategemea na location utakayofanyia project mkuu, Ila kadri unavyooenda mbali na DSM ndivyo unaongeza gharama za uchimbaji, sasa kama ili kupunguza cost ,anza project yako mkoa wa Pwani na kingine na kwamba mahitaji yako pia yataathiri bei ya uchimbaji, mfano kuna jamaa mmoja kachukua ekari 300 , anayaanda sasa kwa kilimo, kwa ekari hizi ili apate maji ya kutosha amechimba kisima cha kipenyo cha inchi 8 na amechimba mita 200, kisima pekee yake ametumi milioni 45 complete,,
But standard kisima ni inchi 5 ambapo bei yetu kwa kila mita moja ni 90k kwa maeneo ya pwani.
Baada ya kuchimba kisima inatakiwa kuweka miundo mbinu ya kusambaza maji kwa kuweka reservoir point baada ya kila ekari kadhaa ili maji yaweze kumwagilia eneo kubwa la shamba lako, hapa lazima utandaze bomba za kutosha na tank tower.
Karibu.
 
Katika hizo mita 200, maji yanakuwa yanapanda yenyewe au mpaka yavutwe na pump
 
Backward integration. Well said
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…