Sikia mkuu Watu wengi hawajui kuwa mafuta mengi mwilini sio tu suala la kula sana na kutofanya mazoezi. Kuna upande mwingine muhimu sana ambao watu wengi hawaujui —
hormones, hasa insulin.
Nikupe ushauri wangu.
Tatizo la kuongezeka kwa mafuta kwa mtu wa kilo 100 mara nyingi linahusiana na jinsi insulin inavyofanya kazi. Iko hivi Mwili unapata nishati kutoka kwenye:
- Glucose ya chakula unachokula
- Mafuta yaliyohifadhiwa mwilini (ndiyo yaliyojaa maeneo kama tumbo, kiuno, au kwenye ini)
Unapokula mara kwa mara kuanzia asubuhi hadi usiku chai, mkate, biskuti, karanga, juice, ugali, wali, na vitafunwa vya katikati insulin inabaki juu muda mrefu. Wakati insulin iko juu, mwili unatumia glucose ya chakula badala ya kutumia mafuta yake kama nishati. Hapo ndipo mtu anakaa na mafuta kugoma kuondoka. Hata ikifanya mazoezi vipi huwezi kupungua.
Hii ndiyo sababu mtu anaweza kula “kidogo” lakini mara nyingi sana na bado hapungui. Si kwamba anakula sana , ni kwamba insulin haiwi chini. Insulini inazuia mwili kutumiaafuta ya mwili ( stored fats ) kama chanzo Cha nishati.
Suluhisho liko kwenye
mpangilio wa kula. Lengo ni kuupa mwili muda wa kushusha insulin ili mwili uwe na nafasi ya kutumia mafuta yaliyohifadhiwa ambapo ndio njia ya mtu kupungua.
Fanya Hivi Sasa kuanzia Leo. Usisubiri kesho. Fanya maamuzi Magumu.
- Acha kabisa vitu vya sukari na matunda ya sukari Kwa kipindi Cha miezi 6
Sukari na matunda ya sukari hupandisha insulin haraka kuliko chakula kingine chochote. Namaanisha sukari ya chai, vinywaji vitamu, soda, juice zilizo na sukari, sweets, biskuti, cakes, chocolate tamu, energy drinks, n.k. Kwa mtu mwenye kilo 100, hii hatua moja inaweza kubadilisha mwili haraka.
- Kata unga na vyakula vya wanga laini
Unga wa ngano, mkate, chapati, mandazi, pasta, biskuti, na sabuni ya kila siku ya ugali mweupe na wali mweupe hupandisha insulin muda mrefu. Hii inablock mwili kutumia mafuta.
Badala yake, kwenye milo yako weka:
• protini (mayai, nyama, samaki, maharage)
• mboga
• mafuta mazuri (parachichi, mayai, karanga kiasi)
Hii combination itapunguza insulin spike na inakusaidia kukaa bila njaa kwa muda mrefu.
Kitu kingine muhimu
acha kula kula ovyo kati ya milo. Usiwe unakunywa chai saa 1, mkate saa 3, biskuti saa 4, juice saa 6, ugali mchana, halafu jioni tena mkate au soda. Hayo ndiyo hufanya insulin ibaki ON muda wote.
Hivyo basi
1. Acha kula asubuhi ... Kunywa Maji au Black coffee bila sukari au Herbal tea bila sukari... Kunywa Maji Hadi mchana.
2. Kula chakula cha mchana. Kijae protin na mafuta ( Fat) kama parachichi.. Na simple Carbs kama Ndizi , au carbs zenye mizizi kama viazi vitamu, mihogo nk. Mboga za majani na nyama.
3. UkimaliZa kula cha mchana usile kitu chochote ( don't snack). Kunywa maji Hadi usiku. Lala.
Kwa mwanzo ni ngumu sana. Ila utazoea.
Ukiona unashindwa. Kula mchana ... Halafu ikifika saa Moja kula Tena kidogo sana.
Kumbuka pia kutembea umbali hata wa kilomita 10 Kila siku. Sio lazima kukimbia just walk
Ingia Google check Japanese walk.
Utapungua Hadi utajikataa.
Ukishapungua Sasa unaweza kuwa unakula Kwa mpangilio mzuri huku ukizingatia mwili wako usionhezeke tena.
Jipe miezi sita for this challenge.
Anza Leo.
Hujachelewa.