Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Kubadilisha kadi kama ulifungulia tawi la nje ya mkoa utasikia mhudumu anakwambia tutakata charge tsh 30,000![emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849][emoji849]
 
[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]na vipi kuhusu Standard Chartered?
Wazuri sana kwenye customer care, online banking na security ila makato yao ni hatari tupu. Mimi niko nao kwa sababu ya urahisi wa kutuma na kupokea pesa kutoka au kwenda nje ya nchi pia wana security nzuri kwenye akaunti hivyo si rahisi kuibiwa pesa.
 
Hii benk ya hovyohovyo Sana,waliniboa hadi hisa nilizokuwa namiliki nikaziuza.
 
Hizi bank kubwa zina wateja wengi. Kuna wakati naona kama hawajiongezi tena sababu wanajua hatuna options nyingi. Nenda Mwanga Bank...it comes out strong now
 
Hahaa, unakuta mtu akishapata mshara wake akitoa matumizi yake yote balance inabaki 50K, nae anakuambia anasave.
Miaka nenda rudi account haijawai gusa 2M
Account Inashindwa Na Kibubu
 
Equity bank nawakubali kuliko bank zote nchini...naomba tu waongeze matawi na atm ziwe nyingi...wataisoma namba inavoshuka wao watapitisha mishahara lkn hawatakuw na saving ya mtu ..
 
Vipi kuhusu Standard Chartered?
Standard chartered is the best, i do anything as a champ.connected with my tigo pesa and mpesa,i am satisfied for real: Even Absa is the best.chagua brand unayoipenda tu na ujoin,
standard chartered unafungua a feekaunti bure na kadi unaletewa bure na cheque book unapata ukitaka(kwa gharama), Absa kufungua akaunti unaanzia 20000tshs.(kadi unapewa na cheque book applicable kwa gharama) but sometimes cheque book inategemea na aina ya ac.uliochagua mf.personal saving/personal current ac.
Maintanance fees zinarange 5000 hadi 9500 kwa mwezi depends on aina ya ac.uliyofungua. pia unaweza ukaopt. Wazime kabisa online pursase ili hata mtu akiiba kadi yako hawezi kufanya online purchase.pos unaweza fanya kwa sababu inahitaji pin.ni salama.
Equity nao wako vizuri na prepaid card wanazo bila kuwa na akaunti na hawana makato. Except for withdraw
 
Nen
Njoo standard chartered ununuliwe mkopo na ela unapewa uwe malaika. Hadi 150m.
 
Equity iko poa
Nimeshaona matawi yao posta, mwenge, mbagala, temeke, k/koo na maeneo ya pale quality center, na bado gharama za kutoa hela kwa wakala wao bado zipo chini kuliko mitandao ya simu
 
Ni vile hatuwekezi muda wetu kidogo kufanya research. Tunanunua huduma kwa mkumbo au kusikia.

Standard Chartered, Stanbic, ABSA wapo vizuri sana. Na wapo transparent sana kwenye cost za huduma zao. Huwezi kuta unjustified transactions.

Ila hizi benki zinazopitisha matrilioni ya serikali kaa nazo mbali. Hata ukiondoka wewe hawajawahi kuwaza kama ni wa muhimu kivile.

Nakumbuka wakati natumia fnb, nikideposit mpunga, customer care ananipigia kuniuliza kama nilikutana na changamoto yeyote wakati naweka hela. Nikitaka kudeposit cheque, nawapigia kuwauliza baadhi ya maswali. Ishatokea nilichelewa kidogo bank, nikawapigia wasifunge branch yao ya pale sinza, wakanisubiri. Ila nilichelewa kama 10 mins. Hawa jamaa wapo top kwenye customer care.

Ukitaka ufurahie huduma nzuri, weka pesa kwenye benki ambazo taasisi za kimataifa zinaweka au wahindi wanaweka. Stanchart, Absa, Stanbic, DTB n.k
 
Niliwahama crdb mwaka 2012, card yangu ilimezwa atm ya udsm, nikaenda idai, wakaniambia kwakuwa nilifungua acc mcity, basi nipeleke complaint yangu huko.

Nikafunga acc saa ileile nikasepa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…