Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

tatizo wanakata bila kusema, sikuhyo walinikata, nikaachana nao mara moja

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Bank ilinitia hasara iyo nakumbuka wakati nipo shule wizi umeshamiri nikawaambia rafiki zangu hela tuhamishie kwenye account yangu ya CRDB basi kila jumapili anayependa kanisani anaenda kuweka pesa Basi pesa ziliwekwa hadi ikafika kama laki 2 na 80 pesa za hao jamaa wawili na pesa yangu laki 1 tulipo maliza shule nipo na jamaa tukaenda kwa wakala makato makubwa nikasema niende ATM pesa niliyoikuta [emoji24][emoji24][emoji24][emoji24]
 
Maendeleo Bank
 
Bank zote TZ zinafanana. Bahati mbaya huna namna.
CRDB wamezidi jamani, kuna siku nilikuwa na shida na sh laki moja, mtu kanitumia bank, kwenda kutoa nikaambulia elfu 75....niliumia sana
 
crdb ilikua bank bora sana Kimei kaondoka na crdb yake hii ya sasa majanga
 
Sababu ni kuwa watu hawajielewi,
 
Mkuu fungua blockhain wallet au exchanges kama Binace,trust wallet ,Huobi global etc......weka hela zako interm of stable currencies kama USDT
 

Alafu huu ujinga wa CRDB kudanganya watu kwamba kutuma hela CRDB kwenda CRDB ni bure waache kabisa. Wanakata vizuri tuu
Kuna muda meseji haziji kabisa kwa miamala. Na ikija wanakuambia tu umetuma kiasi fulani hawakupi salio.
Bank hovyo sana hili.
 
Halafu utawasikia mwisho wa mwaka wanatangaza faida ya mabilioni!! Kumbe wizi mtupu!! Ni manyang'anyi yanayovaa tai na suti.
CRDB wamezidi jamani, kuna siku nilikuwa na shida na sh laki moja, mtu kanitumia bank, kwenda kutoa nikaambulia elfu 75....niliumia sana
 
Naam watu wanasahau. Kwenye miaka ya 2000 mwanzoni nilipata katenda ka $. Nikafungua akaunti ya $ hapo CRDB kwa Kimei. Kila nikitoa pesa zangu na wao wanatoa, eti ni chaji za kutoa. Nikafunga, nikahamia benki nyingine. Lakini sasa karibu benki zote zimeiga huu wizi wa mchana. Hakuna sehemu ya kukimbilia. Zinatofautiana tu kiasi cha makato.
Hata wakati wa Kimei ilikuwa hovyo tu. Tena ilivyoanza pata tenda za serikali kama nmb ndo ikafia huko.
 
Ajabu kweli. Hata kama uchumi wa nchi unatelemka wao wanaropiti faida ya mabilioni! Mabilioni ya wizi wa makato. Faida yao yai reflect hali halisi ya uchumi wa nchi.
Mabank ya Kitanzania sijui yanafanyaje biashara yani makato ni makubwa kama una ka hela ka ngama ni bora uweke chini ya godoro tu.

Ndiomaana yanapata super profit kila msimu.
 
Aisee kama sina dharura na haraka huwa naingia kutoa ndani dirishani kwa teller angalau makato ni nafuu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…