Ninahama CRDB; ni benki gani inayoweza kuwa mbadala bora kwa Dar es Salaam?

Hii Benki imejaa wezi kama mtandao wa Vodacom.
 
nibora na salama hela zako kubaki nazo nyumbani. tafuta chobingo moja nzuri zitupie huko.Stori za makato utaziskia kwa akina Usokwe na wenzake tu
 
Kirefu cha FNB,,?, Je hadi huku nyalikungu wapo?, Maana wamenivutia sana
 
Equaty bank ni nzuri changamoto kwa mikoa mingi Wana tawi moja tuu makao makuu ya mkoa na baadhi ya mikoa hamna kabisa tawi ata mawakala hamna pia Ila Nina account yao na wapo vizuri Sana.
Equity wanasaidia mtu kuwa na nidhamu ya fedha, ATM zao ni za kuhesabu, branch pia, ukienda kwa wakala wengi hawana float.....so ukitaka hela ni lazima uende branch though wanatakiwa waboreshe huduma, waongeze ATM, kuhusu wakala sielewi kwanini wakala wengi wa Equity ukienda wanakwambia hawana float
 
Nmb chachap iko poa sana, haina makato yoyote yaani unaweka bure unatoa bure(ATM) ila tu ni account ya kuweka hela ndogo
 
Vipi kuhusu MKOMBOZI!??

Mimi hawa CRDB nasubiri mkopo uishe tu nitawapotea hawataamini.

CRDB, VODACOM na CCM (ya akina JK, Nape na Makamna) ni WAHUNI na MAJAMBAZI na ADUI wakubwa kwa walalahoi hapa Bongo.
 
Niliwahama crdb mwaka 2012, card yangu ilimezwa atm ya udsm, nikaenda idai, wakaniambia kwakuwa nilifungua acc mcity, basi nipeleke complaint yangu huko.

Nikafunga acc saa ileile nikasepa.
Wapuuzi sana, huduma mbovu kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…