Ninahitaji mwenyeji USA jimbo lolote ila Texas ni much preferable

Hivi Arizona ni jimbo au mkoa anyway Mr ma weed welcome much in Arizona,tuvute kitu cha chuga. [emoji849]
Haha asante mkuu nashukuru kwa wito ila huo ujana nilishastaafu zamani sana mkuu
 
Vizuri sana kwa kupenda maisha mazuri. Endelea na juhudi hizo inaonekana utaweza especially kama tayari una kipato cha kutosha kulipa visa fee na flight ticket. Nipo katika mchakato huo naamini soon nitafanikiwa.

Kama una fedha njia ya haraka ni kupata tourist visa ambayo fee yake si chini ya $700. Baada ya mwezi utakuwa nayo ila pia bank account yako isome salio la kama $9,000 na pia uwe na flight fee kama $3,000. Visa itakuwezesha kubaki USA kwa miezi isiyozidi 6.

Ukifika USA na uwe na mtu wa kushukia kusave fedha, nadhani ndilo unalotafuta sasa, good!

Ukiwa kule tafuta kazi ya kuajiriwa na mwajiri akupe work visa sponsorship, halafu apply visa adjustment kupata permanent residency. njia hii ni ngumu kama huna qualification za kutosha kupata ajira. Au njia nyingine oa (au pata tu mchumba) raia wa huko na it akusaidie kupata permanent residency ndani ya miezi 6 na uraia within 3 years. Njia za panya zipo na zina madhara yake.
 
Asante kwa darasa mkuu lakini pia asante kwa kuusoma na kuuelewa uzi wangu vizuri nadhani shughuli ya kutafuta visa ianze kwa kasi.
 
Asante kwa darasa mkuu lakini pia asante kwa kuusoma na kuuelewa uzi wangu vizuri nadhani shughuli ya kutafuta visa ianze kwa kasi.
Sawa hata mimi nipo kwenye issue ya kutafuta pa kushukia. Pia angalia uwezekano wa kushukia kwa watu wanaopokea wageni na kukaa nao kwenye nyumba zao au Mashamba yao. Hawa wanaweza wakakuchaji rate za kawaida, wakachaji rate kidogo au wengine wasikuchaji kabisa. Kuna websites zinaorodhesha watu hao (hosts) mfano WWOOF check World Wide Opportunities on Organic Farms | WWOOF. Hawa ni watu wenye mashamba(farms) na wana plans mbalimbali za kukaa na wageni kwa jinsi mtakavyo kubaliana wengine wanalipisha, wengine hawalipishi na hata wapo wengine wanakulipa kidogo na kukupatia chakula, accommodation,etc
 
Kuna mcheza kikapu timu ya ABC Army Basketball Club Enerico Agustino aka Mabange jee ndiye wewe?.
 
Ninapatikana John's Corner siyo mbali kutoka Camp David ni sehemu tulivu na ina baridi inayovumilika.
 
Ninapatikana John's Corner siyo mbali kutoka Camp David ni sehemu tulivu na ina baridi inayovumilika.
Nashukuru kukufahamu brother, John's Corner ipo TX? Utulivu na hali ya hewa nzuri ni jambo jema , , nitakutafuta unipe experience asante sana kaka.
 
Imekaa poa hiyo ngoja niifatilie kuna website pia inaitwa "workaway" hii pia ina host wengi wanaoprovide accomodation na food ila ni ya kulipia. Hiyo WWOOF haiitaji mtu awe na ujuzi kwenye kilimo?
 
Kwenye huu uzi wako nimeona matambo ni mengi zaidi kuliko ulichohitaji kukiwakilisha
 
Imekaa poa hiyo ngoja niifatilie kuna website pia inaitwa "workaway" hii pia ina host wengi wanaoprovide accomodation na food ila ni ya kulipia. Hiyo WWOOF haiitaji mtu awe na ujuzi kwenye kilimo?
Haihitaji ujuzi wowote ila upende kujifunza na kufanya kazi kwenye organic farms. Zipo website nyingi tu workaway pia ni nzuri sana. Ila itabidi ujiandikishe na kulipia ili uweze ktumia sites hizi kupata mwenyeji.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…