Ninajua kila mtu anajua kinachoendelea kule Los Angeles ila sijui ni wangapi wanajua chanzo cha ule moto unaouangamiza mji wa uzuri wa Dunia

Kinachotokea ni trailer bado movie haijaanza 😃 ipo siku watu watalia na kusaga meno
 
Ni kwa vile watu hawasomi vitabu ,nabii E.G white aliandika 1906 kuhusu kuungua kwa los angels na Chicago kama maasi yataongezeka. Na kama watu hawatamrudia Mungu. Lakini kwa vile shetani amepofusha fahamu zao ndio maana wakaanza kumdhihaki Mungu. Lakini wamevuna kile walichopanda kwa kutomheshimu Mungu wa Mbinguni.
 
Hakuna watu wapumbavu duniani kwa sasa kama Nikki Glaser yaani badala ya kuomba Msamaha kwa Mungu yeye aningia mtandaoni anaomba msamaha watu!? Deni lake linakuja!
 


Iko hivi .
Kama kuna binadamu wenye akili na maarifa basi ni wazi kuwa kuna viumbe wengine wenye akili zaidi . Binadamu hawezi kuumba kisichokuwepo kabisa . Yaani aamke asubuhi asema pawe na nyumba halafu iwepo katika mpangilio mzuri na wa kisayansi. Hapana.
Ni lazima tukubali na tumsifu huyu aliyetoweka hapa duniani na kutupa nafsi zenye kujua jambo zuri na baya na pia kufurahia uzuri wa dunia . Huyo ni wazi kuwa sisi kwa ujinga wetu na udogo wetu na maarifa yetu madogo sana maana tumeumbwa tu hatuwezi kamwe kumjua kwa asilimia hata 5 ya muumba wa aya mavitu yote yanayoonekana na yasiyoonekana . Unajua hata roboti limetangenezwa na binadamu lakini halina uwezo wa kufikia mahali pa kusema kuwa linaljua binadamu na linamkosoa na kujipangia linavyotaka lenyewe . Ukiona hivyo basi Binadamu ataliharibu na litakua halina faida kwake .

Binadamu wa leo ni mtu mdogo sana anayehitaji uangalizi na ulinzi mkubwa ili aweze kukabiliana na mazingira yaliyopo . Huyu ni modern man . Bibilia ipo wazi kuwa aliwekwa kwenye Eno tofauti na eneo la leo . Ile bustani mpaka leo haijulikani ilipo. Lakini ni wazi kuwa hii duniani haikuwa kwa ajili yetu maana mazingira ya viumbe waliokuwepo ilikua ni tofauti.

Kuna upotoshaji kuwa biblia ilibadilishwa . Huo ni upotoshaji wa makusudi. Katika kitu wenzetu wazungu walichojaliwa ni kuwa na watu halisi wenye kusimama kwenye ukweli hata kufa . Bibilia ilikua haifai kabisa kwa watawala wa dunia karne zote mpaka leo.

Ni rahisi kuona nchi inatawaliwa kwa misingi ya Dini lakini sio kwa misingi ya bibilia . Hivyo juhudi kubwa ya watawala mpaka leo ni kuidhoofisha biblia. Uliopondoa Bibilia basi umeondoa utawala wa Mungu duniani . Yaani dunia itakua inatawaliwa au inajitawala bila kufuata kanuni za Mungu . Na kanuni za Mungu zipo wazi kwa viumbe vyote. I
Binadamu wanaimani tofauti kwa sababu ya kupotoka ndio maana Mungu alikua anawatuma manabii ili kurejea kwenye imani ya Mungu aliyeumba . Kuna dhana kuwa vitu vimetokea tu kama bahati nasibu kulingana na nguvu za asili .😂😂😂Sasa hizo nguvu za asili ni nani ? Wanaona aibu kusema huyo ndiye Mungu aliyeweka hizo nguvu za asili na huo ndio ukuu wake .

Kuna dhana kuwa Mwanamke kwa sababu amepewa akili ya ziada katika saikolojia ya malezi basi yeye ndiye anayepaswa kuabudiwa . Hiyo ni dhana potofu. Mungu ndiye aliyeumba hivyo na ameumba hivyo makusudi ili malengo yake yatimie .
Hakuna mwanasayansi anayetengeneza kitu bila malengo .
Hebu fikiri kuku anayetototo vifaranga 30 na anavilisha chakula na kuvilinda mpaka vinakuwa . Je ,mwanadamu anauwezo huo ? Hata bilionea na Genus Musk au Billget hana uwezo huo . Je,kuku ana akili kuliko binadamu ? 😂😂😂😂😂😂Zamani tulikua tunaambiwa kuwa kuku ndiye kiumbe pale nyumbani mwenye ubongo mdogo sana .

Lakini pia kuna kiumbe anaitwa nyuki . Anatengeneza asali kwa maarifa makubwa sana . Mpaka leo hajawahi kuingia kwenye biashara ya kuuza asili na kujipatia fedha na kisha kujenge himaya yake yenye majumba na magari ili amshibiti binadamu mharibifu. Kwa sababu ndivyo alivyoumbwa. Mwanamke na mwanaume ni watu wawili tofauti sana . Kamwe hawawezi kufanana kwa sababu hawakuumbwa wakiwa wanafanana kitabia na kihisia. Hivi maumivu anayopata mwanamke wakati wa kujifungua angekuwa mwanaume angejaribu hata kufanya tendo analojua litampatia mimba nyingine 😂😂😂😂?
Yaani tungejua tunafanana dunia ingeisha mapema sana . Ndio maana ya kuletwa Mwanamke tusiyeganana kitabia na kihisia . Mwanamke akapewa saikolojia na akili ya ziada katika kulea na kumfundisha mtoto tangu akiwa mchanga .
Mama amepewa akili ya kumtambua na kumlea mtoto ambaye ndiye , huyo atakuja kuwa mwanaume na mwanamke mwingine wa baadae.

Mwanaume anafananishwa na Mungu kwa sababu ya hulka zake ,tabia zake za kuwa mlezi na mlinzi wa familia . Mwanaume anajitolea saa nyingine bila sababu. Mfano mwanaume anaweza kumpenda sana mama mkwe ,baba mkwe , Mashuleni,watoto wa kufikia,marafiki wa mke wake lakini tabia na hulka hiyo wanawake hawana kabisa . Mwanaume anapenda kuheshimiwa tu na kuwa ndio watawala tabia ya Kimungu .

Lakini pia watu wanapotosha sana kuhusu Ukristo . Ukristo sio dini za matbiko na ibada . Ukristo ni ufalme wa Mungu duniani ndio maana ukristo unapata upinzani mkubwa sana toka kwa watawala na vyama vya siri kwa sababu ya kutaka kuitawala dunia. Watawala wa dunia kamwe hawangeuweza ukristo kama sio kutumia mabavu na hata kuua ili tu kutawala .
Himaya ya Kirumi ilihofia sana ukristo ndio maana ikaubeba na kuutumia kuhadaa ulimwengu lakini ni wazi kama ukristo katika ukweli wake bila kutumia vitusho ,mauji na nguvu dunia nzima ingemfuata Kristo Masihi na ukristo ndio ungetawala dunia nzima kwa haki bila kutumia upanga wala mapanga . Lakini kwa sababu ya tamaa za watu waovu ,ukristo unapigwa vita sana kwa sababu ni ufalme wa Mungu duniani . Wakristo kazi yao ni moja tu kuutangaza ufalme wa Mungu duniani kote .Yaani dunia itawaliwe katika misingi ya amani ,upendo na ukweli .
Hiyo ndio dhana iliyomleta Kristo na ukristo duniania.

Fremason na Iluminant wanafanikisha sana kutumia silaha za ukristo kuutawala na kuuteka ulimwengu lakini katika uharibifu. Hii njia ionekanayo kuwa ni ya uzima lakini mwisho wake ni upotevun( dunia kupotea ) .
 
huyo ni mr.Ropo ropo
 

Ni upuuzi tupu.

Janga la moto huko LA kiini chake hasa ni mabadiliko ya Tabia-nchi (Climate change) Wala siyo hicho ulichoeleza.

Je, unataka kusema kwamba ajali ya kuporomoka kwa matope ya Mlima Hanang kule Manyara ni kutokana na sababu kwamba Watu wa huko walikuwa wanafanya Sana maasi dhidi ya Mungu? Je, unataka kusema kwamba Watu wa huko Hanang walikuwa wanafanya Sana vitendo vya ushoga na usagaji ndio maana Mungu aliamua kuuporomosha Mlima Hanang ili kuwaadhibu watu hao? Is it???
 
Picha zinaonesha majani makavu na hakuna hiyo baridi unayoisema.
Baridi haifanyi majani kuwa mabichi. Ila wakati wa baridi na hasa mwaka huu ambapo baridi imekuwa kali mno na haijapata kuonekana theluji nyingi sana Ulaya na America, mimi imenishangaza kuona moto mkubwa wa kihistoria ukiwaka huko Los Angeles. Kwa kawaida kuna mioto inawaka maeneo hayo hasa kaskazini mwa California karibu na Yosemite National parks kila mwaka lakini ni majira ya joto kali kuanzia July-October na sio majira ya baridi kama sasa.
 
Hana uwezo wa kutofautisha mwenye kosa na asiye na kosa?
Maana akileta adhabu inaangamiza viumbe vingi vidogo na vikubwa. Moto unaangamiza mpaka mayai ya ndege, nyoka, kenge n.k.uwezo

Uwezo anao na hayo ameyafanya sana na anaendelea kuyafanya.

Anapoleta jambo kama adhabu huwa alichagui na hapo Kuna hekima zake.

Hao ambao hawana hatia kufa kwao kwenye hiyo adhabu ndio muda wao ulifika humo, lakini kwa wenye hatia wapo ambao waliona hayo maovu yakotendeka lakini wakayafumbia macho nao pia hubebwa na hiyo adhabu.
 
Alisema moto utatokea mwaka gani?
Hahaaa acheni chai zenu. Moto hapo ushatokea mara nyingi yeye alimaanisha huu wa 2025?
 
Internet na simu umegundua wewe? una matatizo ya akili wewe si bure
Sijagundua Mimi, Sasa ndio nini yaani ? Jenga hoja. Shida yenu inakuja pale mnapowaona Wazungu ni wajuzi wa kila kitu, wakati ukweli Wazungu ni watu wa kuangalia fursa.

Mfano mchakato mzima wa Sayansi wa mwanzo sio mzungu, lakini sababu nyinyi hamfatilii haya mambo mnaaminishwa kuwa ni mzungu. Soma historia ya kadhia ya mnayoita "Scientific Method", utajua nafasi ya wazungu Iko wapi.

Sasa hoja yako Iko wapi ? Kwani huwezi kuwa mgunduzi wa simu na ukawa mjinga kwenye mambo mengine ya msingi ?

Sasa jengeni hoja kulingana na mada husika.
 
Unataka uthibitisho wa aina gani kwa kitu ambacho hakipo?

Sababu unajua hakipo unatakiwa utuambie na ututhibitishie, umejuaje hilo na ushahidi utupe.

Sasa kama huwa unaandika ilimradi ufurahishe nafsi yako, hapa sio mahala pake.

Hakikisha unajokidai u akijua.

Kingine swali nalifanya Lowe rahisi, unajuaje kama kitu fulani hakipo ? Je hutanguliwa na kutokuwepo kwake au kuwepo kwake kisha kikawa hakipo ? Maana kitu ambacho hakijawahi kuwepo ni muhali kukidiriki. Kwako hili limewezakana vipi ?

Sasa ulete hoja na sio utoto.
 
Mabadiliko ya Tabia-nchi siyo Kitu Cha uhalisia? Are you mentally stable?

Is it true that a Climate change is not a real thing???

Sio tu Climate Change, nakuongezea mpaka Global Warming, naposema sio jambo halisia ni kwa vile linavyoelezewa na hao Wazungu na kutaka sababu zinazo pelekea hilo. Ndio maana nasema wazungu ni WAJINGA na waongo isipokuwa wale wazungu ambao wamerehemewa na Allah wakawa wakweli na wenye elimu.

Wewe si unaambiwa kwamba Kuna Mabadiliko ya Tabia nchi au Kuna Global Warning, Sasa naongelea zile sababu wanazuoni zisema wao ndio za uongo na uzandiki.
 
Ili ukidiriki kimoja wapo aweze kuunguza na kuangamiza mji mzima no matter kuna werevu au wajinga?

Naam, sababu hata hao werevu pia huwa Kuna uzembe wameufanya.
No wonder watu wenye fikra kama zako ni rahisi kuwaambia waende kuua watu in the name of God....

Kwangu ni si rahisi sababu jambo la kupigana kwa ajili ya Allah ni ibada, kina masharti na nguzo, endapo viwili vikitimia na nikaamrishwa kufanya hivyo nitafanga ila sio kiholela holela.
Ila mtu kama mimi siwezi kufanya baya lolote au kushangilia baya lolote no matter ninaambiwa limetoka kwa nani;

Wewe unajuaje kama jambo hili ni baya na hili ni suri ? Yaani kipimo chako ni nini ?
Baya ni baya hata kama unaamini limetoka kwa Mungu au vinginevyo...

Kwa kipimo gani unachotumia wewe mpaka ukasema baya ni baya ? Tuambie hili, ili tuonyeshe ujinga wako ulipo.

Kingine unapo mjadili Mungu hakikisha unamjua sio kama mnavyofanya nyinyi kumjadili msiwe mjua, huu ni upumbavu na ujinga ulio pea na kukomaa kabisa.

Karibu kwenye mjadala, sasa.
 
Sasa wewe unatuandikia mambo ya ajabu ajabu eti unadai hii dunia Ni ya kike😄 Sasa kwa Nini tusiku nyok*

Unajua fika kwa vyovyote maelezo yako hayawezi kulinganishwa na yale ya biblia lkn bado uko bize kupotosha watu. Nenda andaa nondo zakutosha Kisha njoo humu ueleweke. Wewe hoja zako zimekaa kwa mtindo wa upingaji biblia pasipo hoja za kina.

Mwanamke kwenye biblia ameelezewa vizuri Kuna mama maria amebarikiwa kuliko wanawake wote au humuoni? Maisha yasingekuwa na maana endapo wote tungekuwa sawa. Lkn pia uonavyo ndivyo ilivyo vinginevyo ungebadili hata kidogo punguani wewe.
 
hata mchome juzi alisema hata malaika wakija kuisaidia mc algiers watafungwa na Yanga, kilchoendelea kila mtu anakijua
 
Acha wivu eti haya maisha magumu yameletwa na mabeberu na maisha mazuri yameletwa na mwafrica? Kwani hakuna waafrica wenye maisha mazuri? Uhalisia tu unatuonesha kwamba hata akili tunatofautiana iweje tulingane wote? Lkn bado hujachelewa unauwezo wakuleta badiliko kubwa lkn sio kwa hoja hizi hapana.

Mlimkosa yesu ndo sababu hamueleweki.
Alafu kumbe hata biblia hujasoma vizuri unakurupuka ooh! Mwanamke amedharauliwa.

Neno la Mungu Ni uzima. Wewe endelea kudharau uone, Wala kwa Sasa hata uendelee kusoma biblia huwezi kupona coz umeiseti akili kwamtindo wa kupinga na hakuna mahali pengine utakuja kumwona Mungu tofauti na kwenye imani, ilimpendeza kuishi humo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…