Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 3,135
- 3,392
Ikiwa Mungu ni mjuzi wa yote, je, alijua kuwa moto utaangamiza California siku moja?
Kama alijua, kwa nini alishindwa kuzuia au kuhamasisha watu wake wanaomuomba kuepuka maafa hayo?
Kama Mungu anajua kila jambo linalotokea na litakalotokea, kwanini aliruhusu maafa kama hayo kutokea mpaka kwenye makanisa yake?
Je, hapendi kuabudiwa kama anavyodai?
Je, alijua kwamba wasio na hatia wataathirika, lakini aliona ni jambo lisilostahili kutoa taharifa kwa watu wake?
Ikiwa Mungu ni mjuzi wa yote, kwa nini alishindwa kuzuia moto wa California kabla haujaua au kuhamasisha watu wasio na hatia kuondoka?
Kama Mungu ni mwenye nguvu zote na mjuzi wa yote, kwanini ameruhusu janga kama hili kutokea ilihali aliweza kulitafutia solution nyingine mapema?
Je, ni ni sahihi yeye kuwapa mateso watu wasio na hatia ikiwa alikuwa na uwezo wa kuzuia?
Ikiwa Mungu alijua mapema kuhusu moto huo, kwanini aliruhusu watu wasio na hatia kuathirika?
Je, nguvu zake zote hazingemruhusu kuhamasisha au kuokoa watu wake kabla ya maafa?
Ikiwa Mungu ni mwenye huruma, asiye na hasira, na msamehevu, kwanini msamaha wake unaonekana kuwa na udhaifu? Infact, Anaendelea kumsamehe na kumwachilia Shetani ambaye ndiye chanzo cha uovu kisha analeta mateso kwa wanadamu wasio na hatia.
Kama Mungu ni mwenye huruma, kwanini anaruhusu Shetani kuendelea kutenda maovu na kuangamiza watu, huku akionekana kuwa na uwezo wa kumshinda au kumhukumu?
Kama Mungu ana uwezo wa kuangamiza uovu, kwa nini anaendelea kumruhusu Shetani kuleta maafa na uharibifu kwa binadamu?
Je, hii inahusianaje na sifa zake za Nguvu, Haki, Huruma na upendo?
Je, ni haki kuacha wengine kuteseka kwa makosa ya wengine?
Kama Mungu anahukumu na anahukumu maovu, kwanini haadhibu ipasavyo wale wanaozua madhara makubwa kwa jamii, kama wauza viungo au walio katika dhambi, wakati ana uwezo wa kuondoa uovu kwa haraka bali anachagua watu wa kuadhibu?
Infact hii story ya Mshana ni ya kubuni na haihusiani na tafiti za kisayansi kuhusu vyanzo vya moto.
Ikiwa si ya kubuni ninahitaji majibu kamili ya hayo maswali hapo juu.
What led to hotel fire disaster at Turkish ski resort?
Some survivors did not hear a fire alarm and there are claims of failures in the hotel's fire safety.
Moto mwingine umeua watu 79 huko Uturuki, juzi tu. Sijui nazo ni hasira za Mungu?!?!?!