Ninakubaliana na Rais, hiki ni kipindi cha kuimarisha Sekta Binafsi

Si unaona sasa fuata JF motto ‘ficha ......

Kumbe unajadili vitu hujui kama topic yenyewe inayohusu mambo ya taxation ni accounts.

Wewe unadhani kwa nini waajiriwa wa TRA wanaokwenda kukadiria wafanyabishara kodi ni wahasibu. Unadhani kodi inakadiriwa tu kwa utashi wa mtu.

Matatizo watu wanajitafutia kwa kutotunza kumbukumbu zao na kuto kuandaa accounts zao on time.

Halafu sasa kwenye hii mada sina upande wala sifanyi siasa nataka nijifunze tatizo lilipo haswa maana malalamiko ya kodi yamekuwa mengi.
 
Ni kweli kuna upungufu wa kumbukumbu na kutojua sheria za kodi zinapelekea wafanyabiashara kutozwa kodi na faini kwa kutotimiza wajibu wao na hii huwafanya kupata faini ambayo haiendani na kipato chao cha biashara hapo ndipo lilipo tatizo la wafanya biashara na pia upungufu wa sheria yenyewe kuzalisha faini na riba kubwa mno na ndiyo kilio kikubwa. Upande wa pili ni wafanya kazi wemyewe kubambikiza kodi na faini za uongo ili kushawishi rushwa kubwa mfano Kesi ya mfanyalazi wa TRA Mwanza-Mary Moyo mwezi uliopita aliyekamatwa na TAKUKURU kwa kumbambikia mfanya biashara kodi za uongo na kuomba mamilioni ya fedha. Hivyo kuna suala la elimu, sheria yenyewe,maadili kwa watumishi na mifumo.
 
aliyeiua hawezi kuifufua. Kifupi pombe hapendi mafanikio ya watu wengine. Ndio maana yangu aingie madarakani ameshindwa kulipa madeni ya ndani na kusababisha baadhi ya wafanyabishara kufilisika
 
Serikali yoyote makini dunia inakuwa na mfumo wa kuinua biashara yaani 'Business tool '
 

Suluhu la hili tatizo ni wenye makampuni/wawekezaji kujua sheria za na taratibu za kodi, na Watendaji wakuu wa makampuni kuzijua sheria na taratibu za kodi na kuzitekeleza kadri kadri ya taratibu za TRA. Wengi wetu tunafanya biashara lakini hatuna uelewa wa kodi. Na hata ikitokea TRA wanatuambia tulipe hizo kodi wanasema tuu lipa kiasi hiki ila hawatupatii maelezo/tasfiri/matokeo ya wanachotuambia.

Na kutekeleza hilo TRA wasiishie tuu kwenye kupokea reports, kukusanya kodi, na kutoa tax clearance. Wanatakiwa kukaa na kujitathmini kuhusu malalamiko ya wateja. Wafanye utafiti kujua gap lililopo kati yao na walipa kodi na kulifanyia kazi ili kujenga mazingira rafiki kati yao na pesa zinakotoka.

Sioni kwanini TRA ishindwe kupata suluhu katika kupunguza mateso na malalamiko ya wateja wanaowafanya wao kuwa walipo. Kumsaidia mlipa kodi kuelewa taratibu itawapa motisha watu wengi zaidi kuwekeza na kufanya kazi na TRA.

Idara ya huduma kwa mteja TRA mnafeli wapi?
Mkiweza kuvaa viatu vya walipa kodi mkawatendea haki watatimiza wajibu wao kiroho safi. Ila mkiwaacha waendelee kuumia kwa makosa madogomadogo wanayofanya kwa kutokuwa na uelewa wa kodi na kuwapa kodi kubwa na penalties mjue tuu mnachochea kuipunguzia nchi mapato
 
Umeandika point za msingi kabsa, mfano angalia GPSA inavyokimbizana na wafanyabiashara wa stationery mjini mpaka wamefunga hiyo biashara ili gpsa iweze kufanya biashara peke yake na serikali.
 
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
 
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
That is not the issue.

Kitu ambacho nimejifunza kodi inayolalamikiwa for the most imekadiriwa ni VAT na hiyo aitakiwi kuwa tatizo kwa mfanyabiashara because it should be passed to the final consumer.

If you are business input VAT can be claimed back and you have the responsibility to claim output VAT on behalf of TRA.

Kwa maana hiyo kitendo cha kutoa risiti isiyo sahihi ni upumbavu uliopindukia because VAT is traceable.


Halikadhalika kitendo cha TRA kuwaadhibu walaji it’s just pathetic it’s not their duty to ask if a trader is registered if they are the final consumers or their duty to know who is a registered and unregistered traders complicated to explain but from what I heard from TRA ☝️ their explanation is just pathetic. To explain how pathetic requires a report.

Kuna tatizo TRA kwenye matakwa ya VAT payer in terms of records starting with what a receipt needs to cover and what records a business needs to keep in order to trace registered VAT payers, kuna watu wananunua kariakoo for exportation kuwaadhibu ni ushamba kwa uzembe wao.

Kuna maswali ya tax estimates kwa wafanya biashara when they are filing for their quarterly tax returns what system is used accrual or capital (as yet its not clear, to me). Hayo mambo yanahitaji washaushauri (accountants) kuliko TRA kuzunguka nchi nzima kutoa elimu.

Na linapokuja swala la profit accounts ndio kabisa utegemei mfanya biashara aweze fanya accounts bila ya accountant kwa sababu awezi jua all of his allowed expenses kama VAT tu inamshinda ku file. If that is the case most are at the mercy of TRA officials, that’s not ideal.

Unajua Trump halipi Tax ndogo huko kwao kwa bahati mmbaya it’s the Law, similarly malalamiko yetu ya makampuni kutolipa kodi kwa miaka sio kwamba kweli wanakwepa kodi ni sheria zetu za copy and paste ambazo pengine atuzuelewi vizuri ndio zinawaofanya watu wanaotumia firms kama PWC au Dolloite kufanya accounts zao kutumia loopholes za hizo sheria kukwepa kodi (hao watu ni tatizo ata kwa mabeberu)
that is the case everywhere in the world.

Kwetu sisi wafanyabiashara na accountants it appears have limited knowledge on the law to make matters worst kila finance act inaleta mabadiliko and people don’t keep up but TRA staffs: there is a problem of taxation in Tanzania.
 
Mwenyewe ndio kaiua sekta binafsi kwenye awamu yake ya kwanza, kila tenda anapeleka Suma JKT, leo anasema anataka kuifufua nitamuamini vipi?
JK aliweka vizuri secta binafsi yeye akabadilisha nakumnanga miaka mitano imepita anarudia matapishi if that the case amuombe radhi JK maana alimnanga
 
Sidhani kama kodi za TRA hazilipiki bali tatizo biashara hakuna imefungwa kuanzia juu mpaka chini, unaporuhusu serikali ifanye biashara jua kuwa mamia kwa mamilioni watafunga biashara zao
Serikali inafanya biashara gani zinazoharibu biashara zao?
 
kujipanga ni chaka fulan hivi
 
Kwa kutumia utaalamu na uzoefu wako wa uchumi, tupe mifano halisi ya jinsi sekta ya binafsi iliweza kukuza uchumi kabla ya utawala wa huyo unayembeza.

Ukishindwa kufanya hivyo bila shaka yoyote wewe tindo unaleta swaga tu za kijiweni humu JF kama mlivyojiaminisha "NiYeyeee" angeshinda Uchaguzi Mkuu. Badala yake mmelishwa matango pori kuamini viongozi watashitakiwa na nchi itawekewa vikwazo vya kiuchumi.

Uamini usiamini, iwapo utatumia kichwa chako vizuri, miaka 5 ya utawala wa sasa, kama wewe ni mjasiriamali, una kampuni au umeajiriwa, kuna fursa tele za kujikwamua kiuchumi.
 

Nakurahisishia kabisa, rais juzi kahamishia kitengo cha uwekezaji kwenye ofisi yake,maelezo yake ilikuwa kuwa utendaji wa hicho kitengo unakwamisha uwekezaji. Hilo moja, unasema kuna fursa tele za kujikwamua, nieleze zile pesa zilizoporwa kwenye Bureau de change kwa mtutu wa bunduki na Jwtz zikipelekwa wapi? Katika mazingira hayo unatarajia muwekazaji yoyote serious kutokea? Urudi na maelezo ya hizo pesa za Bureau nikupe chai ya moto.
 

Katika moja ya bandiko zake Salary Slip nimemshauri, nawe nakushauri, mtumie majukwaa ya mitandao ya jamii kueleza Itikadi na Sera za vyama vyenu vya siasa badala ya kuomba dua Serikali ya CCM iharibikiwe.

Km hilo la Bureau de Change, wewe unajua kuwa zilikuwa zinatumika kutakatisha fedha. Kwa sasa baadhi ya Benki za biashara, km NMB, kama ulikuwa hujui, zimefungua ATM ambazo mtu anaweza kutoa fedha ya kigeni.

Kwamba kuna fedha iliporwa kwenye Bureau de Change, nawe unataka tuamini hivyo wakati hakuna madai yoyote mahamakani! Porojo tu za kijiweni kama zile zile wakati wa kampeni za uchaguzi - ati ushindi kweupe.

Kama hambadiliki kifikra mtabaki kuongozwa na udaku. Pole zenu wafuasi wa upinzani humu JF kwa upumbavu na ulofa wenu kifikra.
 

Nilijua huna jibu zaidi ya kuleta blabla, mimi sio katibu wa itikadi wa chama chochote cha siasa, hivyo sio wajibu wangu kueneza sera za chama chochote cha siasa. Kama unataka kujua sera za chama chochote cha siasa hapa hakuna ofisi ya chama chochote, nakushauri uende kwenye ofisi za chama husika ukachukue vitabu na vijarida vya sera zao. Vinginevyo unionyeshe mada yoyote uliyowahi kuanzisha ili ueneze sera za ccm.

Kama bureau De change walikuwa wanatakatisha pesa chafu, ilipaswa wapelekwe mahakamani kila mmoja ashitakiwe kutokana na ukubwa wa kosa lake. Hilo la kuporwa pesa za Bureau de change lilifanyika mchana kweupe, sijui unakataa nini. Kama umeporwa na Jwtz, ni mahakama ipi utaenda hapa nchini kushitaki. Hakuna mtu yeyote anayeweza kuagiza Jwtz wakaendeshe operation yoyote nchi hii za rais, je ni mahakama gani nchi hii inathubutu kwenda kinyume na maagizo ya rais, tena rais mwenyewe huyu asiye heshimu sheria? Nasema hivi hakuna muwekazaji yoyote wa maana anaweza kuwekeza hapa nchini chini ya serikali hii.

Hilo la kuomba serikali ya ccm iharibikiwe, naona umechomeka haya maneno ili yaweze kubeba maelezo yako dhaifu. Hatuko tayari kuiunga mkojo serikali yoyote ya wakandamizaji na wakiukaji wa haki za binadamu, wauaji na wezi wa kura. Huko Afrika kusini walikuwa na serikali halali, lakini tuliingilia mambo yao ya ndani kwakuwa serikali hiyo ya wazungu ilikuwa inawafanyia uonevu watu weusi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…