Hismastersvoice
JF-Expert Member
- Jan 26, 2013
- 24,523
- 30,084
- Thread starter
- #41
Mkisha tepeshwa matako mnavimba unajiona umevunja ungo.Kwanza we kima unalaani kama nani nyau pori wewe!
Mkisha tepeshwa matako mnavimba unajiona umevunja ungo.Kwanza we kima unalaani kama nani nyau pori wewe!
Nataka nijue Mushi kafanya nini!Mbona nimeeleza ni swala la ardhi.
Inasemekana mzee Mushi ni marehemu.
Unataka! Ili iweje, mahakama ilimpa ushindi dhidi ya walalamikaji kabla hajafariki, hivyo wewe hauwezi kubadili chochote.Nataka nijue Mushi kafanya nini!
Mdau hapa ni muhtasari wa hii habariUna haraka Gani asubuhi yote hii hadi kushindwa kutoa briefing ya kinachogombaniwa. Mzee Mushi ndio nani? Alifanyaje?
Mdau hapa ni muhtasari wa hii habari
Wakuu kwa wale ambao hawajui ni nini hasa kimesababisha hii taharuki ya Mkuu wa Mkoa na amri yake ya ukamataji kutokana na kosa la mtoa mada kukimbilia haraka kupost habari hii juu juu bila kuelezea kiundani hapa chini ni kikokotoo na muktadha mzima wa suala hili tangu mwanzo ili kuweka kumbukumbu sawa na kuleta weledi jukwaani.
Mgogoro unahusu umiliki wa eneo la hekta 10 kule Madale Scout Wilaya ya Kinondoni ambapo tangu mwaka 2015 upande wa Kitwanga ulishinda kesi dhidi ya familia ya Mushi na kuanza kuwauzia wananchi viwanja lakini mwaka 2022 familia ya Mushi ilikata rufaa na kushinda rasmi hukumu halali ya Mahakama ikionekana kuwa ndio wamiliki halisi wa eneo hilo
Kufuatia ushindi huo familia ya Mushi ilitekeleza amri ya Mahakama mnamo Septemba 3 2026 kwa kuondoa kaya zaidi ya 15 za wananchi waliokuwa wamejenga katika eneo hilo jambo ambalo lilisababisha taharuki kubwa kijamii baada ya mali na vyombo vya wananchi hao kutupwa nje huku wengine wakikosa kabisa mahali pa kuishi
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila aliingilia kati kwa nia ya kufanya usuluhishi wa kiutu akitaka kuwakutanisha wanafamilia ya Mushi na wananchi waliofukuzwa ili kuona kama kuna uwezekano wa wananchi hao kununua maeneo hayo rasmi badala ya kuishi nje ambapo aliitisha mkutano wa pande zote mbili eneo la tukio mnamo Septemba 19 2026 lakini familia ya Mushi haikutokea kwenye mkutano huo
Kitendo cha kutofika kilimkasirisha Mkuu wa Mkoa ambapo alikitafsiri kama dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka ya Serikali na hapo ndipo alipoamuru Jeshi la Polisi kuwakamata wanafamilia hao na kuwaweka mahabusu hadi Jumatatu
Sakata hili kwa ujumla wake linaibua mjadala mzito na kudhihirisha mtazamo wa wachambuzi wengi kuwa wakuu wa mikoa nchini wamepewa madaraka kiasi kikubwa sana kisheria na kiutawala na mara nyingi wanayatumia vibaya kwani familia ya Mushi ina haki yote iliyotukuka kulinda na kutumia ardhi yao kulingana na amri halali ya Mahakama ya mwaka 2022
Kutumia nguvu ya dola kuwakamata na kuwaweka mahabusu raia walioshinda kesi mahakamani kwa kosa tu la kutofika kwenye kikao cha usuluhishi ambacho si cha kisheria na hakina ulazima wa kisheria ni mfano wa wazi wa jinsi madaraka makubwa ya wakuu wa mikoa yanavyoweza kuingilia uhuru wa mahakama na haki za msingi za raia
Kimsingi kama umeelezea sawa, kuna uvunjaji wa katiba na haki za binadamu katika agizo hili.Akiongea huko Madale mkuu wa mkoa ameliagiza jeshi la polisi liikamate familia yote ya mzee Mushi na kuwaweka kolokoloni! Ni lipi kosa la mke na watoto wa mzee Mushi wanahusika na kosa ambalo huenda lilitendwa na marehemu! Sidhani hata walalamikaji watafurahia kuona mke na watoto wa anayedhaniwa mtuhumiwa wanafungwa bila kupitia mahakamani kutokana na kosa linalohusu ardhi.
Ninawakaribisha Lucas Mwashambwa na Thlaatlaa kupongeza pia.
Ndugu mdau Mdogoee, kwanza chukua sekunde chache ukajifunze maana ya jina langu (Kijana Wa Ifoza) kabla ya kukimbilia ukabila wa Kaskazini. Hivyo asili yangu haina uhusiano na weledi wa hoja ninazoziweka hapa.Tatizo lako nawewe yumkin ni mtu wa Kaskazini
Mkuu wa Mkoa kivyovyote wewe ni Mwananchi wake uko ndani ya Mkoa wake
Yeye akikwita lazima uwende
labda uwe na Sababu za Msingi kugomea kwenda
Unaitwa na Mwenyekiti wa Usalama wa mkoa wako
Kwanini ugomee
Kwasasa kisheria ndani ya Mkoa wa Dar es Sallam
Kumepigwa Marufuku kutumia Mabaunsa
Familia ya Mushi imefanya kosa kutumia Mabaunsa kuvunja nyumba za watu 15
Ndiomana wamekimbia mkutano
Wamejua kile wamefanya ni kosa Kisheria ndani ya Mkoa huu ✍️
Uko sahihi kabisa mdau Kiranga. Hoja yako inagusa msingi mkubwa wa utawala wa sheria na haki za binadamu unaokiukwa hapa:Kimsingi kama umeelezea sawa, kuna uvunjaji wa katiba na haki za binadamu katika agizo hili.
Ndugu mdau Mdogoee, hakuna anayebisha kuwa mahakama haikuruhusu matumizi ya mabaunsa; hoja hapa ni kwamba ukiukwaji huo wa taratibu ulitakiwa kushughulikiwa kisheria mahakamani na siyo kwa Mkuu wa Mkoa kutoa amri haramu ya kukamata familia nzima jukwaani. Huwezi kunyoosha makosa ya mabaunsa kwa kutumia madaraka vibaya kinyume na Katiba, kwani kosa halisafishi kosa lingine.Mahakama haijawai kusema kutumike Mabaunsa kwenye kukamata Mali
yenye kuzozaniwa 👈
Mahakama inayo taratibu zake zenye kueleweka
Sio Mabaunsa ❌️
Ndugu mdau Mdogoee, kwanza chukua sekunde chache ukajifunze maana ya jina langu (Kijana Wa Ifoza) kabla ya kukimbilia ukabila wa Kaskazini. Hivyo asili yangu haina uhusiano na weledi wa hoja ninazoziweka hapa.
Hoja yako ina makosa makubwa ya msingi kiutawala, kikatiba, na kisheria:
1. Sheria Hailewi Makosa Mawili: Kama familia ya Mushi imekiuka taratibu kwa kutumia mabaunsa (jambo ambalo liko nje ya amri ya mahakama), mkuu wa mkoa alitakiwa kufuata mkondo wa sheria kuwashtaki kwa kosa hilo. Huwezi kusahihisha kosa la kutumia mabaunsa kwa kufanya kosa jingine la kisheria la kutumia madaraka vibaya (Abuse of Power).
2. Mamlaka ya Kukamata kwa Wakuu wa Mikoa Imewekewa Mipaka: Kisheria, amri ya kukamata raia inatakiwa itoke Mahakamani kupitia vyombo vya dola baada ya kuwepo kwa mashaka ya kijinai. Kifungu cha 7 cha Sheria ya Tawala za Mikoa [Cap. 97 R.E. 2002] kinampa Mkuu wa Mkoa mamlaka ya kuagiza ukamataji TU pale mtu anapotenda kosa la jinai mbele yake, au pale anapokuwa na sababu za msingi kuamini kuwa usalama na utulivu wa umma (Public Tranquillity) unakiukwa na hakuna njia nyingine ya kuzuia isipokuwa kumuweka ndani. Kutofika kwenye kikao cha hiyari cha usuluhishi siyo tishio la usalama wa mkoa wala siyo kosa la jinai.
3. Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama siyo Jaji: Cheo hiki kinampa mkuu wa mkoa mamlaka ya kusimamia ulinzi, siyo kuwa Hakimu wa kutatua migogoro ya ardhi ambayo Mahakama ilishatolea maamuzi tangu mwaka 2022. Wito wa RC ulikuwa wa usuluhishi (mediation) ambao kwa asili yake ni wa hiyari, siyo wito wa kimahakama (summons).
4. Ukiukwaji wa Katiba: Ibara ya 13(1) na 13(6)(a) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatamka wazi kuwa kila mtu ana haki ya kulindwa na kupata fursa ya kusikilizwa na chombo huru cha sheria (Mahakama). Mkuu wa Mkoa kujifanya jaji na kutoa adhabu ya mahabusu jukwaani ni kuingilia uhuru wa mahakama na kukiuka haki za kikatiba za raia. Tuache ushabiki Mdogoee, tufuate sheria.
Ndugu mdau Mdogoee, inaonekana aidha husomi kuelewa au unalazimisha ubishi kwa kuhamishia hoja kwenye ukabila na hisia za 'kulala nje' badala ya misingi ya sheria. Nakupa mfano huu rahisi: Kama mtu akimuua rafiki yako na unajua wazi kuwa ndiye muuaji, je, sheria inakuruhusu wewe kuchukua bunduki na kwenda kumuua yeye? Ukifanya hivyo, utakuwa umejibu uhalifu kwa uhalifu mwingine na utachukuliwa kama muuaji vilevile mbele ya sheria.Sawa yumkin kwenye ukanda unajitetea
lkn utetezi wako umeegemea zaidi pande ile y North ❗️
Lkn kwako kuvunjwa nyumba 15 kwanjia ilio kinyume cha Sheria kutumia Mabaunsa sio kosa la jinai???
Mkuu wa mkoa anaweza kukuswekwa ndani ❗️
ndani ya mkoa wake ili kutunza Amani yumkin yeye anazo taarifa za nyinyi familia ya Mushi kutaka kuvamiwa kuuwawa👈
Jamba wamefanya ni kubwa kwenye Jamii
familia 15 zinalala nje ya nyumba
Wewe ulale ndani
ya nyumba 👈
nyumba zenyewe za maana zimevunjwa❗️
Unajua mkuu wa mkoa kalenga nini kutoa agizo ilo mbele ya zile familia zenye kulala nje❗️
Ndugu mdau Mdogoee, hakuna anayebisha kuwa mahakama haikuruhusu matumizi ya mabaunsa; hoja hapa ni kwamba ukiukwaji huo wa taratibu ulitakiwa kushughulikiwa kisheria mahakamani na siyo kwa Mkuu wa Mkoa kutoa amri haramu ya kukamata familia nzima jukwaani. Huwezi kunyoosha makosa ya mabaunsa kwa kutumia madaraka vibaya kinyume na Katiba, kwani kosa halisafishi kosa lingine.
Paskal hivi kuna sheria huruhusu kuwekwa ndani kienyeji kisa familia kudai haki yao?Naunga mkono hoja.
p
Walivunja sheria ipi?Wakati Familia ya Mushi imevunja Sheria
Lkn Kijana wa Ifoza unapendekeza
Mkuu wa mkoa kufata
Sheria kuendea kwa Wavunja Sheria yani Familia ya Mushi
Kumbuka Familia 15 wanalala nje kipindi ichi cha hatari za mvua kubwa za El Nino✍️
Kosa la msingi ni lipi fafanua kosa kwanzaKufata Sheria ni msingi wa lazima
Familia ya Mushi imejiona yenyewe inanguvu za kila upande
Sasa Kufikia Serikali kuingilia kati manake
Moja ya lengo kufikishq ujumbe kwake Familia ya Mushi na wengine kwamba wanatakiwa
kufuata Sheria
SERIKALI ipo macho ikiona Unaopuyanya kibabe👈
jua Serikali watakuja mbele yako kukumbusha wewe ni sehemu ya raia wacha kuonea raia wenzio✍️