Ninalaani agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutaka familia yote ya mzee Mushi ikamatwe

Ninalaani agizo la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kutaka familia yote ya mzee Mushi ikamatwe

Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, raia wake familia zaidi ya 15 zinalala.nje wapo watoto, wazee, wagonjwa asiingilie kati? Yule mchaga amehonga mahakamani ananyanyasa raia kwa pesa zake hana hata utu,, km anaweza kumdharau na kumpuuza mkuu wa mkoa atamsikiliza nani nchi hii? Atamsikiliza mwenyekiti wa mtaa? Anataka aishije nchi hii? We huwajui wachaga wakipataga pesa, yule ni wa kufukuzwa arudi kwao Moshi
We jamaa una chuki na wachaga. Je umejuaje huyo mchaga amehonga mahakama? Heshimuni wachaga sana na wahindi ambao ndo wanawainulia uchumi wenu
 
Kuvamia nyumba na Mabaunsa ni kinyume cha Sheria

Mahakama kwenye hukumu yao hawajasema wavamiwe na Mabaunsa❗️

kubomoa nyumba zao na wahuni wahuni wasiotambulika
kisheria 👈

mbaya zaidi MKUU wa Mkoa alitoa Amri kwenye mkoa wake kusitumike Mabaunsa kwenye migogoro ya aina ile ✍️
Ardhi ni pamoja na chochote kilichopo juu yake. Yani mtu ardhi yake hataki nyumba mnampangia asibomoe?? Hapo kisheria hadi hizo nyumba hapo ni Mali ya Mushi. Mi nawachukia sana wavamizi, wanavamiaga ardhi za watu kisha wanajenga, likiwakuta wanatafuta sympathy..subiri siku ardhi yako ikivamiwa ndio utaujua utamu wake.. Na nikwambie haki ya mtu haipoteagi tena ikiwa ni ya kimahakama ndio balaa kabisa....sahiz we mwache yule Rc aingize siasa zake, siku akiwa hayupo ofisini hiyo haki itatekelezwa tuuu.

Halafu ukikaza hukumu ni dalali wa mahakama ndie anaepewa kazi na mahakama.. kama kuna uharibifu wowote katika utekelezaji haliwahusu kina Mushi bali ni hao madalali wa mahakama ambao wapo kisheria na mabaunsa ni hao madalal wamewaleta
 
Kwaiyo utaelewa
Pamoja na Sheria ilikuwa upande wa MUSHI lkn namna kaenda kwenye eneo usika
Iyo familia ya Mushi imevunja taratibu kadhaa

Ndiomana mkuu wa Mkoa imebidi kufika kwe tukio kuwasadia familia 15 wameonewa✍️
Jifunzeni sheria, familia ya Mushi ina kosa gani? Ukikaza hukumu dalali anaetafutwa ni wa mahakama, kwa hiyo mkosaji hapo ni dalali wa mahakama ambae yupo kisheria
 
Ndugu Mdogoee, nakuelewa vizuri sana. Hoja yako ya sasa ni kwamba kukamatwa kwao kulilenga 'kurejesha amani' na 'kuadhibu dharau' ya kutohudhuria kikao cha Mkuu wa Mkoa. Huu ni mtazamo mzuri wa kijamii, lakini kisheria na kiutawala una mapungufu makubwa sana:*
  1. Mipaka ya Kisheria ya Mkuu wa Mkoa (Cap 97): Ni kweli Sheria ya Tawala za Mikoa (Regional Administration Act, Cap 97) inampa Mkuu wa Mkoa au Wilaya mamlaka ya kuagiza ukamataji. Lakini sheria hiyo hiyo Kifungu cha 7 (kwa RC) na Kifungu cha 15 (kwa DC) inaweka masharti magumu: Mtu anaweza kukamatwa tu ikiwa ametenda kosa la jinai mbele yake, au ikiwa kuna tishio la wazi la uvunjifu wa amani ambalo haliwezi kuzuilika kwa njia nyingine yoyote isipokuwa kumweka ndani. Kugomea kikao cha hiyari cha Mkuu wa Mkoa hakuingii kwenye vigezo hivi vya kisheria.
  2. Kikao cha RC siyo Wito wa Mahakama: Mkuu wa Mkoa hana mamlaka ya Kimahakama (Judicial Powers). Ndio maana mtu anapogomea wito wa Mahakama anashtakiwa kwa 'Dharau kwa Mahakama' (Contempt of Court). Hakuna kosa la kisheria nchini linaloitwa 'Dharau kwa Mkuu wa Mkoa' linalompa mamlaka ya kukamata raia kwa dharau ya kutoingia kwenye usuluhishi.
  3. Adhabu ya Pamoja (Collective Punishment): Hata kama kiongozi wa familia hiyo angekuwa amekosea kisheria, sheria hairuhusu kukamata familia nzima (wakiwemo watu wasiohusika na maamuzi ya kesi) kwa kosa au dharau ya mtu mmoja. Kila mtu anawajibika kwa makosa yake binafsi mbele ya sheria.
Hitimisho la Mjadala wetu:
Lengo la kurudisha amani na kusaidia familia 15 zilizolala nje ni jambo jema kabisa na sote tunaliunga mkono. Lakini katika nchi inayofuata utawala wa sheria, njia inayotumika kupata haki ni muhimu sawa na hiyo haki yenyewe. Huwezi kutumia kosa la kiutawala au la mihemko kusafisha kosa la kukiuka Katiba na haki za msingi za raia.
Kutokana na mwelekeo wa hoja zako, unaonekana kuhalalisha ukiukwaji huu wa sheria kwa sababu tu umeratibiwa dhidi ya familia inayotoka Kanda ya Kaskazini—jambo linaloashiria chembechembe za ubaguzi wa kikanda. Hata hivyo, historia inatufundisha kuwa unywaji wa sumu ya dhuluma hauchagui kabila wala kanda; kuna siku mfumo huu ukizoea kuvunja sheria unaweza kugeuka dhidi yako au watu wako wa karibu.
Kumbuka huko nyuma, mwanasiasa kama Humphrey Polepole alikuwa mstari wa mbele kutetea matumizi ya nguvu kubwa ya dola na ukandamizaji wa haki wakati watu walipokuwa wakipotea na kulalamika, akiamini yuko upande salama. Leo hii, mabadiliko ya gurudumu la utawala yamefanya familia yake nayo ilalamike kama zilivyolalamika familia za kina Ben Saanane na Azory Gwanda. Ukisharuhusu viongozi kuwa madikteta kwa kigezo cha kushughulikia 'watu usiowapenda', unajenga janga ambalo siku likiwafika watu wako wa karibu ndipo utafumbua macho. Sheria ipo kulinda kila raia, bila kujali anatoka wapi. Naishia hapa, kila la heri!

Mimi Nimekuekea sehemu tatu Sababu tatu
Moja ya Kwanza yumkin ni Usalama wa familia yenyewe ya Mushi
Lkn iyo kwako umeitupa!

Jambo la pili unasema sababu ikiwa kuna jinai imetendeka❗️

Lkn ili nilikujibu pia uko juu🖕
Kwako Kuvunjwa nyumba 15
na Mabaunsa sio jinai tosha???
 
Kwa kuongezea, kitwanga alipata ushindi mahakaman, bila kuzingatia kwamba mushi anakata rufaa, yeye aliamua kuuza, kabla ya muda wa kukata rufaa. Mushi aliendelea kuwataadharisha wanunuzi hiyo sehemu ina mgogoro, lkn hawakuskia
Mdau hapa ni muhtasari wa hii habari

Wakuu kwa wale ambao hawajui ni nini hasa kimesababisha hii taharuki ya Mkuu wa Mkoa na amri yake ya ukamataji kutokana na kosa la mtoa mada kukimbilia haraka kupost habari hii juu juu bila kuelezea kiundani hapa chini ni kikokotoo na muktadha mzima wa suala hili tangu mwanzo ili kuweka kumbukumbu sawa na kuleta weledi jukwaani.
Mgogoro unahusu umiliki wa eneo la hekta 10 kule Madale Scout Wilaya ya Kinondoni ambapo tangu mwaka 2015 upande wa Kitwanga ulishinda kesi dhidi ya familia ya Mushi na kuanza kuwauzia wananchi viwanja lakini mwaka 2022 familia ya Mushi ilikata rufaa na kushinda rasmi hukumu halali ya Mahakama ikionekana kuwa ndio wamiliki halisi wa eneo hilo
Kufuatia ushindi huo familia ya Mushi ilitekeleza amri ya Mahakama mnamo Septemba 3 2026 kwa kuondoa kaya zaidi ya 15 za wananchi waliokuwa wamejenga katika eneo hilo jambo ambalo lilisababisha taharuki kubwa kijamii baada ya mali na vyombo vya wananchi hao kutupwa nje huku wengine wakikosa kabisa mahali pa kuishi

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Albert Chalamila aliingilia kati kwa nia ya kufanya usuluhishi wa kiutu akitaka kuwakutanisha wanafamilia ya Mushi na wananchi waliofukuzwa ili kuona kama kuna uwezekano wa wananchi hao kununua maeneo hayo rasmi badala ya kuishi nje ambapo aliitisha mkutano wa pande zote mbili eneo la tukio mnamo Septemba 19 2026 lakini familia ya Mushi haikutokea kwenye mkutano huo
Kitendo cha kutofika kilimkasirisha Mkuu wa Mkoa ambapo alikitafsiri kama dharau na utovu wa nidhamu kwa mamlaka ya Serikali na hapo ndipo alipoamuru Jeshi la Polisi kuwakamata wanafamilia hao na kuwaweka mahabusu hadi Jumatatu
Sakata hili kwa ujumla wake linaibua mjadala mzito na kudhihirisha mtazamo wa wachambuzi wengi kuwa wakuu wa mikoa nchini wamepewa madaraka kiasi kikubwa sana kisheria na kiutawala na mara nyingi wanayatumia vibaya kwani familia ya Mushi ina haki yote iliyotukuka kulinda na kutumia ardhi yao kulingana na amri halali ya Mahakama ya mwaka 2022
Kutumia nguvu ya dola kuwakamata na kuwaweka mahabusu raia walioshinda kesi mahakamani kwa kosa tu la kutofika kwenye kikao cha usuluhishi ambacho si cha kisheria na hakina ulazima wa kisheria ni mfano wa wazi wa jinsi madaraka makubwa ya wakuu wa mikoa yanavyoweza kuingilia uhuru wa mahakama na haki za msingi za raia



 
Tatizo lako nawewe yumkin ni mtu wa Kaskazini

Mkuu wa Mkoa kivyovyote wewe ni Mwananchi wake uko ndani ya Mkoa wake

Yeye akikwita lazima uwende
labda uwe na Sababu za Msingi kugomea kwenda

Unaitwa na Mwenyekiti wa Usalama wa mkoa wako
Kwanini ugomee

Kwasasa kisheria ndani ya Mkoa wa Dar es Sallam
Kumepigwa Marufuku kutumia Mabaunsa

Familia ya Mushi imefanya kosa kutumia Mabaunsa kuvunja nyumba za watu 15

Ndiomana wamekimbia mkutano
Wamejua kile wamefanya ni kosa Kisheria ndani ya Mkoa huu ✍️
Sasa ukishakaza hukumu anateuliwa dalali wa mahakama kufanya kazi, kwahiyo mwenye kosa hapo( kama lipo) sio Mushi baali ni madalali wa mahakama ndo mwenye kosa
 
Jifunzeni sheria, familia ya Mushi ina kosa gani? Ukikaza hukumu dalali anaetafutwa ni wa mahakama, kwa hiyo mkosaji hapo ni dalali wa mahakama ambae yupo kisheria

Kwaiyo kwako ni Dalal wa Mahakama sawa yupo kisheria lkn katoa wapi pesa za kuwalipa Mabaunsa wengi kiasi kile???

Kama sio Familia ya Mushi ndio imewakodi Mabaunsa ❗️
kwanini hawakuja
kwenye tukio japo kusalimiana na Wananchi wenzake ✍️
 
Sasa ukishakaza hukumu anateuliwa dalali wa mahakama kufanya kazi, kwahiyo mwenye kosa hapo( kama lipo) sio Mushi baali ni madalali wa mahakama ndo mwenye kosa

Dalali wanafaamika wa Mahakama kamwe hawawezi kukodi Mabaunsa izo pesa wamepewa nanani kufanya ukodishaji wa Mabaunsa‼️❓️
 
Mkuu wa mkoa ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa, raia wake familia zaidi ya 15 zinalala.nje wapo watoto, wazee, wagonjwa asiingilie kati? Yule mchaga amehonga mahakamani ananyanyasa raia kwa pesa zake hana hata utu,, km anaweza kumdharau na kumpuuza mkuu wa mkoa atamsikiliza nani nchi hii? Atamsikiliza mwenyekiti wa mtaa? Anataka aishije nchi hii? We huwajui wachaga wakipataga pesa, yule ni wa kufukuzwa arudi kwao Moshi
Kabla hataa ya kusema amehonga mahakamani na kunyanyasa raia kwa pesa zake, turudi nyuma kidogo...hilo eneo amelipataje? Aliamua tu kuwaondoa hao watu au alinunua hilo eneo? 🤣
 
Gentleman,
nasisitiza kiungwana kabisa kwamba, wale wote ambao mkuu wa mkoa amaagiza polisi kuwatia nguvuni wajisalimishe kwa hiyari zao mapema iwezekanavyo regardless ya status zao kuepuka usumbufu.

Maagizo ya kimamlaka na kisheria hayana hizo porojo. Tii sheria bila shuruti na itapendeza zaidi, otherwise subiri fedheha na public sympathy ikiwa zina manufaa 🐒
Samahani Mkuu, kosa la Mzee Mushi ni lipi hasa?
 
Familia ya Mushi ilipaswa kufaamu process ya kufuata Sheria kwenda kutwaa Mali yao

Sio kukodi Wahuni kwenda kuvamia Wananchi wenye Familia nyingi kiasi kile

Kwasasa Yumkin wakapoteza Haki yao

Mkuu wa mkoa
Hashindwi kutoa msukumo Kisheria kwa Wananchi wengi kupewa Haki ya kuishi kwenye eneo lao Walimojenga
Mgogoro unamiaka 20 kwasasa
Vipi Familia ya Mushi ikose UTU kwa Watanzania wenzetu
Tena wengi wao
Wachaga wenzake ✍️
 
mahakama iko wapi hapo gentleman? :1Head:
Rc ana mamlaka ya kuhoji hukumu halali? Nilimsikiliza kuna mambo angenyamaza zake tu...ye anafikia hatua ya kumtaja jaji mkuu kwamba ni msikivu atafatwa, Rc ni mwalimu by proffesion, hajui mahakama ni muhimili unaojitegemea? Hii issue italeta mjadala mpana sana, na asipoangalia inweza ikamfungisha virago. Asituchafulie sifa ya serikali yetu na mihimili mingine inayojitegemea
 
Ikumbukwe kwenye Mgogoro wa nyumba pale Msasani

Mkuu wa mkoa alitoa Amri ndani ya mkoa wake kusitumike tena Mabaunsa kwenye Matukio ya aina ile 👈

Kama ni Mahakama imetoa hukumu basi taratibu zifuate zile zile za
kisheria sio kukodi Mabaunsa kwenda kufanya Matukio
ya vile kubomoa nyumba za watu au kutoa watu nje ya
nyumba zao Marufuku ✍️
Wavamizi hua wanafanywaje? Kisheria hizo nyumba sio zao tena...ardhi ikiwa Mali yako ni pamoja na kilicho juu yake..hizo nyumba ni za Mushi ataamua azivunje ama aziache
 
Elezea Mushi kafanyaje!?,kwanini huwa mnaleta thread kama vile kila mtu anamjua huyo Mushi na familia yake walichofanya!?,kama kuna thread ilitangulia weka link watu wasome ndo watoe maoni yao.
Huko insta,tiktok na kwingineko mnaendaga kutazama matako tu?
 
Back
Top Bottom