Ndugu mdau Mdogoee, inaonekana aidha husomi kuelewa au unalazimisha ubishi kwa kuhamishia hoja kwenye ukabila na hisia za 'kulala nje' badala ya misingi ya sheria. Nakupa mfano huu rahisi: Kama mtu akimuua rafiki yako na unajua wazi kuwa ndiye muuaji, je, sheria inakuruhusu wewe kuchukua bunduki na kwenda kumuua yeye? Ukifanya hivyo, utakuwa umejibu uhalifu kwa uhalifu mwingine na utachukuliwa kama muuaji vilevile mbele ya sheria.
Nirudie tena kwa faida ya uelewa wako: Kama familia ya Mushi walikosea kutumia mabaunsa, Mkuu wa Mkoa alitakiwa kuagiza washtakiwe mahakamani kwa kosa hilo la kijinai. Lakini kuitumia nguvu ya dola kukamata familia nzima kinyume cha sheria kwa kosa la 'kugomea kikao cha hiyari' ni sawa na kujibu kosa kwa kufanya kosa jingine kubwa zaidi la kiutawala na kikatiba. Kosa halisafishi kosa lingine hata siku moja. Kitu gani huelewi hapa?