Ninamzidishia baba 500K kila nikitoa hela

hata haukosei mwaya maana ile ya mama ni yake na ile ya baba itatumika nyumbani so ile unayomuongezea inakua yake tu


ila hela zote hizo unatoa wapi mwenzetu ni freemason au 😂
Kweli tunahitaji kujua,au ni Mwigulu
 
Well done; keep it up. Hiyo 500k unayompa mshua mbele za bimkubwa ujue huaga inakwisha mapema sana cause bimkubwa lazima huaga anaiomba kwa matumizi ya nyumbani, hiyo nyingine ndio inayo mlinda mzee wako akiwa na rafiki zake. Kuna na mwingine nae anafanyaga hivo hivo kwa baba yake. Kiasi fulani anampa mbele ya mama yake while nyingine anampa wakiwa chamber
 
Huko ni kujionyesha tu miosho Yani..kwani Kuna ambaye alikwmbia unakosea humu
 
We zidisha hata mara kumi ukiondoka anampa mke wake zote....
Halaf anampa mke wake huku anamchongea:
"huyu mtoto mjinga sana, yani anataka kututenganisha mimi na wewe, hajui kwamba sisi kitatunga kifo tu??"
Halaf ka mama kake kanajibu:
" haka katoto nimekanyonyesha miezi 9 nimekaachisha halaf hakajui kuwa wewe bado nakunyonyesha mpaka leo?, kajinga sana, heb nipe kwanza hizo 800k halaf kesho mwambie tunadaiwa 700k"😂😂
 
Mtume Muhammad SAW amesema unapowasaidia wazazi wako mama yako unampa mara 3 ya kile unachompa baba yako lakini kwa heshima ya baba unampa yeye mwanzo.

Ni kweli wanaume wana majukumu mengi kuliko wanawake lakini kwa upande wa mama aliteseka zaidi na malezi kwa kukesha kuliko baba ndio mama anapewa kipaumbele.

But hongera sana kuwasaidia wazazi baraka zake Mungu zikufikie wewe na kizazi chako.
 
Amin nakwambia binadam yeyote yule ni mnafiki siku ukikoswa hizo pesa. Za kuwapa ndo hutaelewa kuwa duniani kuna watu na viatu
 
Shida inakuwa pale unapompa pembeni hii inakuwa km mchongo flan hv kwanini usimpe mbele ya mama hata km ni zaidi maana yeye ndo kichwa pale,au wewe na baba ako mnamuogopa mama enu?
, au mama anashida flan ndo unaamua kumficha?
Je unmuamini kiasi gan mzee km ashiliki vema ktk ujenzi wa familia?
MWISHO.hizo pesa unatoa wap mpaka zingne mmpe baba kifichoni au na wewe unamichongo flan ya makandokando?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…