Ninaomba mchanganuo wa biashara rahisi... Wanangu hawajalipiwa karo na maisha hayaendi. Nina 500,000 tu ndugu zangu, nifanye nini?

Ninaomba mchanganuo wa biashara rahisi... Wanangu hawajalipiwa karo na maisha hayaendi. Nina 500,000 tu ndugu zangu, nifanye nini?

Biashara imekuwa ngumu sana, wengi wanabeba chakula kwenda kazini. Hata biashara ya mama ntilie imekuwa ngumu sana
Kweli kabisa Maisha ya Tanzania yamekuwa pata pote, kunamtu kagrab kihuni ofisi ya umma anajinasibu anajenga nchi
 
Kwa haraka haraka nitaweka hivi:-
  1. Ufuta 1kg@5000
  2. karanga 1debe@20,000
  3. sukari 5kg@2500
  4. kahawa 10pkt@ 1000
  5. Benchi za mbao 4@15000 (ukiweka viti vya plastic wateja hawataki)
  6. Tangawizi 1000
  7. Maji ndoo 500
  8. Birika 20000
  9. Chupa ya chai 2@15000
  10. Mkaa 1debe@10000
Tumia nguvu zako kutengeneza na kucheka na wateja

Acha kuona watu ni wajinga mkuu! Karanga debe ziwe Tsh 20,000?,
Sukari kg 5 itakuwaje Tsh 2,500?
Kahawa pkt zitakuwaje Tsh 1,000 Badala ya Tsh 1,500 or 2,000?

Elewa pia kuna changamoto za biashara.

Maelezo yako ni ya mtu aliyefunga hesabu kabla ya kazi wakati kuna hesabu baada ya kazi.
 
Acha kuona watu ni wajinga mkuu! Karanga debe ziwe Tsh 20,000?,
Sukari kg 5 itakuwaje Tsh 2,500?
Kahawa pkt zitakuwaje Tsh 1,000 Badala ya Tsh 1,500 or 2,000?

Elewa pia kuna changamoto za biashara.

Maelezo yako ni ya mtu aliyefunga hesabu kabla ya kazi wakati kuna hesabu baada ya kazi.
Hulazimishwi kuelewa,ndio maana matajiri ni wachache.Wote wangekuwa wanaelewa matajiri wangekuwa wengi kuliko masikini.
 
Sawa mkuu, Ni idea nzuri natamani ningekuwa dar. Huku nilipo hiyo idea haitalipa kivile
mKUU umeanza uoga Haitolipa kivile usi iweke unapotaka kuji jibu swali..Hapo majibu ni mawali tu ITALIPA au HAITOLIPA kama haitalipa SAWA nakubali usifanye ila kama Haitalipa kivile ina mana italipa ila n kdg BASI hapo hapo Biashara yoyote inayolipa hata kama ni KIDOGO hiyo ndio BIASHARA.

Biashara isiyolipa hata kidogo hiyo ndio SIKUSHAURI...

NOTE: MFANYABIASHARA HANA BIASHARA MOJA (kidogo cha huku + kidogo cha kule = POCHI NENE)
 
mKUU umeanza uoga Haitolipa kivile usi iweke unapotaka kuji jibu swali..Hapo majibu ni mawali tu ITALIPA au HAITOLIPA kama haitalipa SAWA nakubali usifanye ila kama Haitalipa kivile ina mana italipa ila n kdg BASI hapo hapo Biashara yoyote inayolipa hata kama ni KIDOGO hiyo ndio BIASHARA.

Biashara isiyolipa hata kidogo hiyo ndio SIKUSHAURI...

NOTE: MFANYABIASHARA HANA BIASHARA MOJA (kidogo cha huku + kidogo cha kule = POCHI NENE)
Sawa mkuu
 
Unapochhagua kuwa Mfanyabiashara basi Fanya biashara ZOTE usikae kwenye Biashara MOJA usione aibu kisa una DUKA LA COMPUTER ukaacha kufungua biashara ya Kuchoma MAHINDI ukaweka KIJANA....Usione aibu kisa Una uza BATIKI na VITENGE na mtaji ushafika hata 10Mil eti ukaacha kufungua kijiwe ukaweka kijana akauza Kahawa.

Biashara yoyote hata kama inalipa inakupa LAKI per day TRUSTME kuna siku utapata LAKI halafu ITAPOTEA YOTE (maisha ni changamoto) lakini kama ukiwa na vibiashara vidogo vidogo vingi hata ikipotea ile LAKI ila bado uutapata vi 20,000 au 10,000 kutoka kwenye vile vibiashara vyako vingine ila kama ukijifanya Kukaza shingo na kusema mimi dada duu/kaka duu siwezi uza mahindi wakati nina DUKA LA COMPUTER my Brother TRUST me IPO SIKU moja UTAFUNGA HILO duka.

Kwa kua una hela unajiona haziishi leo wala kesho Ukifunga utafungua biashara nyingine utaenda nayo utafunga tena Mwendo wako ndio huo huo.

TUJIFUNZE KWA WALIOTUTANGULIA kama kina Bakhresa na MO DEWJ hawa watu jmn wanauza hadi PIPI sio wajinga eti? na sio PIPI TU wana maduka na ma Show room ya magari sasa we baki KUDHARAU KAZI endelea na hiyo hiyo unayoifanya leo hapo dukani kwako,ukipita huko njiani wacheke wauza karanga,kahawa,mahindi Wacheke sana.

NOTE: haya maushauri ni kwa wale wenzangu na mimi tusio na ndugu wenye hela wa kutupa mitaji, wazazi wakutusaidia hata 100 YANI tupo sisi kama sisi Hata tukidondoka hamna mtu wakutupa pole na hata 500.. ILA kwa wale watoto wakina bakhresa kina MOO kina MENGI nk nk najua MA DON wako wengi na mpo mnasoma Huu ushauri sio wenu...SISI HATUSHINDANI NA NYIE MANA UKWELI UTABAKI PALE PALE nyie wazazi wenu waliweza kujiwekeza so mmetupiga GEPU hata mpoteze mamilioni mkirudi nyumbani mtapewa MITAJI TENA.

so

Makabwela wenzangu TANGO PORI HILO HAPO JUU.
 
Mtaji wa Tsh 500,000/= kama hautegemei na kula hapo hapo na unaweza kuvumilia angalau mwezi mmoja bila kudokoa faida hata Tsh 100/= unatosha sana. Cha msingi ni kujiandaa kwa lolote - kubadilisha maisha yako na kuwa na furaha au kupoteza hata hicho kidogo ulichobakiwa nacho.
Kama ukiweza kufanya biashara kwa mtindo wa Pre-Selling unaweza kufanikiwa pia. Unachotakiwa kufanya ni kufikiria kitu gani unaweza kuwauzia kwa Cash watu ambao unaweza kuwafikia na kisha nunua sample chache sana kwa ajili ya kutangazia na kuonesha. Baada ya hapo watembelee na uwatangazie kwa ajili ya kukusanya orders na kupata uhakika wa soko. Ukipata order sasa ndo unaenda kununua bidhaa husika kwa bei ya jumla na kisha kufanya delivery na kuwauzia wateja wako kwa bei ya rejareja. Kwa kuanzia anza na bidhaa za watoto na wanawake.
Bidhaa angalia zinazoendana na mahitaji ya eneo lako na mtaji wako. Mengine muombe zaidi Mungu atakusaidia.
 
Viti
Kama wewe ni mfanyabiashara naomba unitajie vitu vinavyohitajika ili kufungua baar au grocery

Utani kwenye mambo ya msingi hautakiwi
Friza ya wastani,Viti, frame, creti za soda ,maji kubwa na ndogo, unaeza anza na mbili la Pepsi na coca, creti za bia hta kiasi tu za kuanzia juice carton kadhaa kwa kuanzia c mbaya...... Na mziki mzuriii /TV
NB:ndobiashara yngu kimaskin lkn inanitoa sikosi 30000-50000 per day

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viti Friza ya wastani,Viti, frame, creti za soda ,maji kubwa na ndogo, unaeza anza na mbili la Pepsi na coca, creti za bia hta kiasi tu za kuanzia juice carton kadhaa kwa kuanzia c mbaya...... Na mziki mzuriii /TV
NB:ndobiashara yngu kimaskin lkn inanitoa sikosi 30000-50000 per day

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa Tsh laki tano 500,000 mwanaume anaweza kufanya hii kazi? Vipi kodi ya nyumba
 
kreti 9 za bia, viti 3, stuli 4 na opena
Kuna kodi ya pango, kuandaa eneo mfano kutengeneza kaunta, glass za kunywea vinywaji, friji, kuna baadhi ya vinywaji vikali vya muhimu na vikorokoro vingine vidogo vidogo.

Kuna leseni ya biashara ili kazi yako itambulike na serikali japo wengi wanafanya biashara bila kuzingatia hili!
 
baby nillaah upo maeneo gani nije kunywa na kujifunza hii biashara natamani kuifungua hapa dodoma
Viti Friza ya wastani,Viti, frame, creti za soda ,maji kubwa na ndogo, unaeza anza na mbili la Pepsi na coca, creti za bia hta kiasi tu za kuanzia juice carton kadhaa kwa kuanzia c mbaya...... Na mziki mzuriii /TV
NB:ndobiashara yngu kimaskin lkn inanitoa sikosi 30000-50000 per day

Sent using Jamii Forums mobile app

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimekuwa na biashara ya kufuga kuku wa mayai bahati mbaya nikauguliwa na mzazi nikauza kila kitu kilicho kuwa kinaweza kuuzika nikamuhudumia, hichi kimenifanya nirudi 0 ila namshukuru mungu mzazi alipona. Nisaidieni nianze vipi maana kuku wanahitaji mtaji mkubwa , naomba msaada wenu wa mawazo . Naishi Arusha

Tafuta jiko la mkaa ukubwa wa wastani kisha tafuta meza ndogo na ukiweza tafuta eneo uanze kukaanga samaki aina ya sato na sangara katika vipande kidogovidogo.
Jitahidi uwe msafi na uamke mapema kila siku ili ufanye maandalizi kwa wakati. Weka bei nzuri yenye faida pia.Nakuhakika shia utatusua hivi karibunia huo mtaji wako ni mkubwa sana.
 
Back
Top Bottom