Ndo utuambie walipo ,nimesoma kayumba ila karibu 75% tulifanikiwa kufaulu kwenda high schools to universities+colleges na sasa tumesambaa nchi nzima wengine ni mainjinia ,madaktari ,MACO,Walimu na wahadhiri one of them UDSM but kati yetu wote kuna njemba inatuburuza kwa utajiri na ilipata div 4 point 26.Ana utajiri unaokadiriwa kufikia 2 bilions na bado hapoi hope by 45 atakuwa ana atleast 40+ bilions kwa mwendo anaokwenda nao , huyu naye ana exposure ipi? Je,wanae watalingana kimaisha na mfanyakazi wa UN ambaye analipwa 4millions per month ambaye akiondoka tu duniani UN wanaajiri mtu mwingine wanamsahau ghafla tu na familia yake inarudi kwenye msoto maana waliishi kwa kutegemea mshahara huo tu wakasoma hizo Feza Schools then wanabeba vyeti kusaka kazi mguu kwa mguu!? Mimi naamini ishu ya mafanikio ya mtu haijalishi kasoma Kayumba au wapi huko International schools sana watoto wanatengenezewa connections tu kutokana na kipato cha wazazi wao sio kwa kuwa they are better than Kayumba students kuihudumia jamii ndiyo maana hata hao wa shule hizo wengi wao hatuwaoni wakiwa tofauti na hawa waliosoma kayumba ukiwatenganisha wao na mitaji ya wazazi wao.
Mfano ishu ya Fernandez hiyo ni akili ya kibiashara tu alipokuja na ishu ya NALA fedha ya home ilimpush kutoka kufeli kidato cha nne hadi kufika Havard na kuwa successfull huko kuendelea lakini ikumbukwe business huenda ndicho kilikuwa kipaji chake tangu awali kwingine alikuwa anazunguka tu.Ndicho mtoa post anazungumzia kwamba besides kusoma huku au kule reflection ya elimu ya gharama inayolipiwa katika shule hizo haionekani katika maisha yetu kama taifa kwa namna tarajiwa.Mfano yupi ni mwl bora kati ya graduate wa kayumba na huyu wa hizo shule za multi millions ? Wapime kisha leta mrejesho.
Kuhusu huyo Adams ninawaza tofauti kidogo kwa mfano hai tu Diamond kasoma kayumba tu ila mafanikio yake tu kimziki anawazidi waliosoma kokote hata waliosomea muziki wenyewe iwe Harvad au kwingine (wa hapa kwetu).Diamond ana exposure kubwa kwa sababu ya talent yake tu not shule aliyosoma na ndiyo hapo tunaposema unapaswa kutazama vema elimu ya wanao inalenga nini zaidi maana maisha halisi yana mitaala kibao ambayo ukiizingatia tu utaisaidia jamii na kufanikiwa pakubwa wewe binafsi.
Simu yako ikifa hapa unamkimbilia std 7-Form 4 ndo akutengezee maana wengi wao wapo hapo kielimu na watakupiga bei wanayotaka na utakubali kisa shida yako maana huna elimu ya wanachofanya kuiponya simu yako japo una degrees za hizo international schools maana wao wana degrees kwenye angle nyingine ya maisha ambayo mtaala hauitambui rasmi.
Unafahamu kwamba screen ya simu yako ya Tsh milion 1 inauzwa Tsh 50000 tu ila fundi anakuhenyesha anakwambia kuiweka mpya na ufundi ni tsh 300000 na unatoa unampa kwa pongez kibao wakati ni kazi rahis tu!? Yaani yeye kutengeneza 1mil anaweza kuhitaji wateja watano tu kwa siku moja sema tu kutunza pesa ndo hawajui ila hawa wanathibitisha kuamini sana elimu ya kukariri darasani ni ujinga kimtindo na tuwaepushe watoto na elimu hii inapobidi tudeal na vitu vinavyoigusa jamii moja kwa moja.