Ninaposema Mwafrika kapunjwa akili na Mungu kwa makusudi kabisa muwe mnaelewa. Rejea ajali ya ndege Bukoba 06/11/2022

Hiyo haiwezi nyenyua ile ndege hata ikiwa tupu.

Ile ATR 42 ikiwa tupu ni 11.7T
Helicopter hiyo ya Airbus ni 5.T lift capacity
Sawa mtaalam.
Basi ingekuwepo around pamoja na divers waokoe watu.
 
Tena muda mwingine hicho kiboti kidogo cha uokoaji kilichopaki pembeni hata mafuta hakina yaani ikitokea ajali hakiwaki...... Sisi ni bado saana mkubwa.!
 
Hii ajali ukiangalia kwa upana na marefu yake. Ni ajali ya kukosa uwajibikaji. Yani tumerudi kule tumetoka. Jiulize angekuwa hai Mzee Magu.... End
Mama anayesufiwa anatoa tamko la kijana mwokoaji aajiriwe Jeshi la maji, badala ya kutafakari wapi palikuwa na tatizo kwenye uokoaji na bila kuwa na vifaa !! Angetoa tamko la kununua boti ya mwendo Kasi ya uokoaji tungemwelewa.
Kwa hiyo kijana akiajiriwa ndio kifaa cha uokoaji ikitokea tatizo lingine si ndio!! Ama kweli Kuna aliyeturoga na alishaondoka zake!!
 
...Na Ajali Ile ya Meli pale Mwanza Miaka Michache nyuma inaelekea haikufundisha lolote licha ya Matamshi Kadhaa ya Kisiasa yalitolewa wakati ule!!
Mkuu, hilo ndilo kinaloumiza, ungetembea baada ya ajali ya Mv Bukoba, vitengo vya ukoaji na boti maalumu kwa ajili ya kazi hiyo ningeanzishwa Mwanza, Bukoba na Kigoma, ili kukabiliana na ajali zinatokea katika ziwa Victoria na Tanganyika.
Ni kweli ajali haina kinga, lakini ikitokea inabidi itupe somo.
Kwangu mimi ndio hapo naona uzembe wa serikali, sio hii ya Mama Samia tu, bali tokea nyuma.Mungu libariki taifa letu.
 
Naomba kufahamishwa kazi ya wanajeshi wetu wa Navy tafadhali.
Wanajeshi wanahusikaje hapo??? Uliza kazi ya jeshi la zima moto na uokozi linakazi gani? Kusubiri moto?? Uliza tena vituo vyao kwa nini vipo mjini peke yake? Ziwani na vijijini hakuna majanga??? Ziara ikatizwe.
 
Wanajeshi wanahusikaje hapo??? Uliza kazi ya jeshi la zima moto na uokozi linakazi gani? Kusubiri moto?? Uliza tena vituo vyao kwa nini vipo mjini peke yake? Ziwani na vijijini hakuna majanga??? Ziara ikatizwe.
Mimi nimeuliza swali maana yake sikuwa nafahamu. Ila tayari nimeshaelimishwa. Asante
 
Tuendelee tu kuwa waoga kwa kisingizio cha amani lakini ukweli ni kwamba siku tunavamiwa na jeshi la nchi nyingine tunaweza tukateketea kama kuku.
Yaan mnamaanisha siku tunavamiwa tunakufa km Kuku huku wao wakiwa wamekaa tu pembeni wanatuangalia tu tunavyokufa wakiwa wanasubiria amri kutoka juu au sijaelewa mkuu?
 
Yaan mnamaanisha siku tunavamiwa tunakufa km Kuku huku wao wakiwa wamekaa tu pembeni wanatuangalia tu tunavyokufa wakiwa wanasubiria amri kutoka juu au sijaelewa mkuu?
πŸ˜€πŸ˜€ hilo nalo linawezekana.
Au wanaweza wakaja vitani bila silaha
 
πŸ˜€πŸ˜€ hilo nalo linawezekana.
Au wanaweza wakaja vitani bila silaha
Duuuh alafu wananchi wakaanza kujipambania na silaha za kijadi, itakua kubwa kuliko hio itavunja rekodi dunia nzima
 
Rescue facilities siyo boti tu...na ukitaka kuweka kila sehemu ni ghali kwetu sisi,siami kwamba hakuna patrol boats Viktoria..lakini moja itasaidia nini!?
Unaambiwa kila Halmashauri ina Kamati ya Maafa

Serikali inatenga Fungu kwa ajili ya Maafa na kila Halmashauri inapewa Fungu lake

Nini kazi ya hili Fungu?

Na kusipotokea Maafa hilo Fungu linakwenda wapi?

Hili swali kuna mdau aliwahi kuhoji

Sasa hili Fungu sijaelewa linatengwa kwa ajili ya kuokoa watu wanapopatwa na Maafa na kabla ya watu kupatwana Maafa au linatengwa kwa ajili ya kuzikia marehemu baada ya Maafa?

Yaan utaambiwa, 'Serikali itagharamia Mazishi', Pesa ya kugharamia Mazishi inatoka kwenye lile Fungu la Kamati ya Maafa kutoka Halmashauri lililotengwa na Serikali
 
Kwani PM alisemaje mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…