Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Ninavyomfahamu Ludovick Joseph Rwezaura (kilio cha usaliti)

Chris Lukosi, kwa kuwa uko hapa kama verified user, naomba nikuulize a hypothetical question...unao uhuru wa kujibu ama kutojibu.
Hivi Chadema kusambaratika leo na kutoweka kabisa katika medani ya siasa Tanzania, je kutawezesha;

  • Maisha bora kwa Watanzania kupatikana?
  • Madawa kupatikana mahospitalini?
  • Waalimu na madawati kupatikana mashuleni?
  • Ufisadi na wizi kukomeshwa serikalini?
  • Utapanyaji wa mali za asili kumalizwa nchini?
  • Utiaji saini wa mikataba mibovu kusitishwa?
  • Utawala bora unaotoa haki kuimarika?
  • Viongozi waliotanguliza rushwa kutokomezwa?
  • Matatizo lukuki yanayowakabili Watanzania kutatuliwa?
Nimeyaita haya hypothetical questions kwa sababu moja tu, najua Chadema haifi, imevuka ile threshhold ya kusambaratika...lakini hata kama hilo lingewezekana, mwamko wa mwananchi hauwezi kuzimwa hata kwa kutumia mtutu wa bunduki. Hivi sasa naamini kwa dhati kuwa Chadema ni zaidi ya viongozi wake, Chadema ni zaidi ya wabunge wake na Chadema ni zaidi ya wanachama wake moja moja...Chadema is a movement and is much more than anything else in its physical form.
Mag3,
hakuna anayetaka chadema ife , tatizo ni viongozi wa chadema kuwapotosha wananchi kwa kuwalaghai kuwa wao wakichukua nchi mabomba yatatoa maziwa baridi.
 
Huaminiki hata na Katoto Kachanga,Huna tena nafasi kwa umma wa watu makini.....tunajua unafanya haya kwa kujipendekeza,pole!
 
Yani wewe mwampamba nawashauri hata marafiki zako wawe makini sana na mambo wanayokwambia.kuna siku utakuja kuwaanikia siri zako peupe!unabwatuka sana kijana..kunyalisya!
 
Mwambapa Ugonile malafyale!
Uliyoongea ni kweli kabisa. Kijana katumika kama vile mtu anavyokula muwa ukiisha utamu unatupwa na kusahau palepale.
Huyu kijana aliweza kudivert emails zangu na kuzipeleka kwa Slaa. kijana alikuwa mtiifu sana lakini wanaogopa wakimkubali tu watakuwa wamekwisha.
Kesho usishangae wakamkana Ben Saa nane kuwa hawamfahamu mara atakapoamua kuimba

Hee,Bee,Kamwene Kaka Chris..
Ali divert email zako na kuzipeleka kwa Slaa?...Ndauli ndauli hapa?yaani ki namna gani?
Hapa ni mahala ambapo kila kitu kinasemwa...umetwambia nusu Kaka."Funguka"
 
Mbowe, Slaa,kwa nini lakin?mna matatizo gani?chama kimewashinda,modulators tunapost,tunatoa maoni huru kama changamoto,matokeo post zinafutwa,ukweli Mbowe si kiongozi na Slaa si kiongozi,sababu ni nyingi,modulators wawe fair,hata kama wao ni chadema,wengine tunajenga hatuna chama,tuishi kwa uadilifu,hata uwe na lipi hakuna jipya hapa dunian,mbowe,slaa please,mnaivuruga chadema,modulators na nyie kuweni fair,post zangu zaid ya 3 nikieleza udhaifu wa mbowe na slaa mnazifuta,sio fair,cjatukana ni hoja,acheni ushabiki,tujenge nchi.

Pole kaka japo spellings zina kusumbua..najua ni kwa sababu ya hasira (ila mshkaji neno modulators umelirudia mara nyingi kwa kuchapia).

Ki ufupi Mods sijui wanafanya kazi kwa niaba ya nani. CDM imechafuka jama hata mfute maoni ya members haisaidii kitu. hata mkifuta threads za kupinga CDM haisaidii kitu. Ngoma ipigwavyo ndio ichezwavyo..najua hii thread haina zaidi ya masaa mawili. Mark my word!
 
Mag3,
hakuna anayetaka chadema ife , tatizo ni viongozi wa chadema kuwapotosha wananchi kwa kuwalaghai kuwa wao wakichukua nchi mabomba yatatoa maziwa baridi.

Mbona mtu mzima unadiriki kusema uongo? Kiongozi gani wa Chadema aliyasema haya. Unadhihirisha tu kuwa wewe ni mtu mzima hovyo kabisa
 
Mwampamba,wewe na baba yako endeleeni tu na kazi yenu ya kuipamba CCM.Na hii ndiyo njia yako mbadala ya maisha,keep going,itumikie CCM upate posho.Waache watz waendelee kusota.
Mwisho sikupendi sana na laiti ningekuwa mchawi ningekuroga.
 
Mtela Mwampamba huna tena cha kueleza maskin kijana wa watu uliyekuwa kamanda mpiganaji lakin ukakubali kurubuniwa kirahisi na huyo Zitto na leo umebaki tu kuwa mpika majungu wa mitandaoni mpaka nakuona huruma sio siri kamanda wangu, Real inaniuma sana.
 
Last edited by a moderator:
Mbowe, Slaa,kwa nini lakin?mna matatizo gani?chama kimewashinda,modulators tunapost,tunatoa maoni huru kama changamoto,matokeo post zinafutwa,ukweli Mbowe si kiongozi na Slaa si kiongozi,sababu ni nyingi,modulators wawe fair,hata kama wao ni chadema,wengine tunajenga hatuna chama,tuishi kwa uadilifu,hata uwe na lipi hakuna jipya hapa dunian,mbowe,slaa please,mnaivuruga chadema,modulators na nyie kuweni fair,post zangu zaid ya 3 nikieleza udhaifu wa mbowe na slaa mnazifuta,sio fair,cjatukana ni hoja,acheni ushabiki,tujenge nchi.

Povu la nini kama hazikidhi masharti ya JF (mojawapo la umbea hatulitaki) chapa lapa
 
Hata CCM wanatakiwa wawe makini naupayukaji wako..wewe hutakiwi ku-access classified information!
 
Ni kweli mkuu hafai kabisa huyu gamba, ni mnafki sana.
Wewe si mtu sahihi wa kuleta maelezo yanayohusiana na CHADEMA, DR. SLAA au viongozi wengine wa CHADEMA kwa sababu huaminiki na pia una chuki binafsi na CHADEMA na viongozi wake. Tunahitaji taarifa ya mtu mwingine kuweza kufikiria kama unachokisema ni kweli au la maana tayari kuna mengi, tangu utoke CHADEMA umeyasema kwa chuki kwa nia ya kujipendekeza CCM. Umekosa credibility!! Mtu kigeugeu, asiyeaminika, hata taarifa yake haiwezi kuaminika.
 
Hee,Bee,Kamwene Kaka Chris..
Ali divert email zako na kuzipeleka kwa Slaa?...Ndauli ndauli hapa?yaani ki namna gani?
Hapa ni mahala ambapo kila kitu kinasemwa...umetwambia nusu Kaka."Funguka"
Kamwene apolinary,
Nitamwaga mboga soon. Stay tuned.
Hiyo technology ya kurekodi kwa vikamera vidogo imetokea huku magharibi, which means kuna siku kombora litadondoka hapa na ndio utakuwa mwisho wa chadomo.
 
wewe ndiye uliyetunga maneno na kuyatengenezea sauti kama ya rwakatare hivyo huaminiki kamwe , nawe nilazima uunganishe kwani msaliti namba 2 baada ya mwigulu kuchukua na. 01
 
Kanuni zipi?
Kimeishanuka tayari hakuna siri tena

hebu waulize hao jamà zako wa zamani hiviîngekuwa ni Post ya MWIGULU au NAPE wangethubutu kusema ifungwe? toka Lwakatare akamatwe wote wanarukana wàmbie tiutasikia mengi kuanzia BAVICHA hadi tender za Magari
 
Mpaka jana Rwakatare alikuwa anaendelea na uhamasishaji wa chadema huko mahabusu na mda si mrefu wafungwa watapata nao ukombozi wao
Itapendeza sana pale atakapovaa jezi za orange na kuwa muwakilishi wa kudumu miaka 30 inatosha kueneza ukombozi jela.
 
Mag3,
hakuna anayetaka chadema ife , tatizo ni viongozi wa chadema kuwapotosha wananchi kwa kuwalaghai kuwa wao wakichukua nchi mabomba yatatoa maziwa baridi.
Najitahidi kukuheshimu na kukuelewa na JF inasomwa na wengi...je nichukulie kama hili ndilo jibu lako kama Chris Lukosi, verified user? Kwa kuwa uliwahi kujiunga na hiki chama wakati fulani je ndiyo hayo ulikuwa ukiwaeleza wananchi...kwamba Chadema wakichukua nchi, mabomba yatatoa maziwa baridi? Hilo moja, la pili nimekuuliza hivi, ikitokea Chadema ikafa, matatizo niliyoyaorodhesha yataisha? Narudia hilo kwa sababu naamini unao uelewa zaidi ya huo uliouonesha katika majibu yako, je ni wapi nakosea?
 
Last edited by a moderator:
Mwambapa Ugonile malafyale!
Uliyoongea ni kweli kabisa. Kijana katumika kama vile mtu anavyokula muwa ukiisha utamu unatupwa na kusahau palepale.
Huyu kijana aliweza kudivert emails zangu na kuzipeleka kwa Slaa. kijana alikuwa mtiifu sana lakini wanaogopa wakimkubali tu watakuwa wamekwisha.
Kesho usishangae wakamkana Ben Saa nane kuwa hawamfahamu mara atakapoamua kuimba
He! Kumbe ni kweli huwa mnatimuliwa kwa kuwa ni wasaliti? Uliandika nini? Hawa watu jamii imeingia hasara
 
Back
Top Bottom