Asante kwakuliona hile. Nimesoma hii post nikaanza kuipa credit kwa kiasi fulani, nilipoangalia imeandikwa na nani nikapata kichefuchefu. Kama anayosema Mtela ni kweli; utamuamini vipi wakati na yeye ni msaliti? Niseme wazi nawachukia sana watu wa aina hii ya Mtela. Sipendi kabisa watu wanaotoka ndani ya chama nakuanza kulialia; inaonyesha wazi sio watu imara wakuweza ku-stand the heat inside the kitchen. Nawaheshimu sana Lowassa, Sita na wengine wote ndani ya CCM kwani wao ndio wanasiasa kamili. Sizungumziii ufisadi; ni kutokana na kwamba pamoja na kuwashiwa moto ndani ya chama, wameamua kusimama huko huko na kupigana huko huko. Mtatiro pamoja na kuwa na tofauti na viongozi wake kipindi fulani, alisimama imara na kutetea anachokiamini. Hawa wote pamoja nakwamba wanaweza kuwa wanatofautiana kimawazo na wewe na mimi; lakini wanaonyesha ni jinsi gani wanaamini wanachokitetea. Hii inaonyesha pamoja na kwamba hawakubaliani na mambo ndani ya chama; lakini wanaamini hasa kwenye itikadi ya chama chao. Same as those people ambao wameamua kubaki CDM,NCCR, CUF etc pamoja na mapungufu yaliyopo, wameamua kupigana huko huko kwani wanaamini kwenye itikadi yao. Sasa hawa watu wa aina ya Mtela, Shibuda and the like, huwa nawaogopa sana maana huwaelewi wanasimamia nini. Wao wanaangalia upepo unakoelekea ndio wanakoenda. I hate this type of people regardless ya chama alichotoka. Hata sikumoja hawawezi kukueleza tofauti za kiitikadi wanazoona kwenye chama au policies, wao ni umbea mwanzo mwisho. Unless useme wazi hukubaliani na itikadi ya chama ulichohama, hayo mengine ni kuwapumbaza watanzania kwani hata wewe Mtela credibility yako ni questionable. Hivi mbona sijawahi kumsikia Prof Safari akielekeza personal attack kwa watu ndani ya CUF? Sijawahi kumsikia yule aliyehama CUF (nimesahau jina) akahamia CCM kipindi kile cha uongozi wa Makamba akitumika insanely kama ninyi vijana? Vijana wa Kitanzania hasa walioko kwenye medani ya siasa, kama vile hawajielewi elewi hivi. Aaargh! Halafu eti vijana ndio wapewe uongozi wa nchi, ili iweje? Kama ni rahisi kuuza utu kiasi hiki utashindwa kuuza nchi au hata kama ni jimbo utakalokuwa ukilisimamia?
Yule aliyehama kutoka CUF na kuhamia CCM kipindi cha MAKAMBA anaitwa TWAMBWE HIZA.Hapo kiongozi nimekubaliana na wewe kabisa katika uchambuzi wako kwa sababu vijana wengi wamaekua kama mashua bila upepo kuvuma upande wanakotaka hawaendi. Ukizingatia kipindi hiki ni cha mageuzi makali vijana ndio tungekuwa chachu lakini tumekua wasaliti utafikiri hatujui wala hatuoni kinachotokea katika Taifa hili. Ushabiki umekidhiri kuliko hata uzalendo. Sasa hivi CCM wanajipanga kwa gharama yoyote ili tu ifikapo 2015 wapate pa kutokea na nini cha kusema. Ni wajobu wetu vijana nasi kupambana kwa gharama yeyote tusighafiliwe na mtu yeyote au kundi la watu kisa tamaa za hela. Wakatia wengine wanapambana mahakamani wengine wanapambana na vijana wa BODABODA kwa kuwadanganya wanawafungulia SACCOS na kuwafanyia michango ya mamilioni ya hele. Hii yote ni kucheza karata na vijana ambao ni wengi. Kama kweli wanataka kuwasaidia watanzania wawakusanye watoto yatima ambao wazazi wao wamefariki kwa ugonjwa wa ukimwi au hata ajali wawasaidie waweze kupata Elimu kama watoto wengine ambapo ni haki yao kikatiba. Wamecheza karata kwenye makinisa na misikiti wakaona wamegundulika sasa wameamua kuhamia kwa vijana. Yako mambo mengi yakufikiri na kujipanga kama vijana wapambanaji na wanamapinduzi wa kweli. Iko kazi ya kuhamasisha vijana kujiandikisha ktk daftari la kudumu la wapiga kura kisha wapate elimu ni jinsi gani ya kupiga kura ili wajikomboe kutoka hapo walipo. Kijana yeyote yule anatakiwa atambue kwamba CCM ndie adui yake namba moja na sio kushabikia kesi zilizoko mahakamani au kutoa siri au mambo yaliyojiri baada ya mambo kufika mahakamani. Alikuwa wapi siku zote asiyaseme haya, hawa ndio wale wanasubiri ajali zitokee ndio waweke matuta barabarani. VIVA CHADEMA VIVA SLAA ALUTA CONTINUE! Mapamabano yanaendelea until last drop!!!!!!!!!!!!