Ninavyowafahamu wateule wapya wa Rais Samia kwa historia yao ya nyuma na uhusiano wao na viongozi wa leo

Kwa January umenena kweli IQ ndogo,pozi lake la kierevu🤣🤣🤣.

Huyu Hana tofauti na Kikwete yeye hujiona ni rais bora zaidi kuwahi kutokea ktk nchi hii kisa wazungu wanaikubali mpaka leo😂😂😂.
 
JPM alijaribu kuharibu hizi circle za madaraka kwa kuleta walau akili mpya lakini sasa tunarudishwa mule mule tena kwa lazima.

Ina maana hii nchi hakuna brain nyingine za kuongoza hadi turudie makosa haya haya kila mwaka?
Naamini mama anaambiwa amchague nani na amtumbue yupi. Kwa ufupi kuna nguvu kubwa inayohakikisha mama anatimiza matakwa ya hiyo nguvu. Kumrudisha fisadi na msanii Makamba? Angalia mkuu wa mkoa Dar? Nani asiyejua ngivu hiyo? Tunasubiri naye Membe aletwe kundini
 
Dai katiba acha majungu, na mpgiwe mchakae tu . Tukiwamahasisha kudai katiba mnatuita magaidi
 
Japokuwa Rais hapangiwi nani wa kuwateua katika nafasi mbalimbali, lakini ni sahihi wizara isiyo ya Muungano kupangiwa watu kutoka upande wa pili wa Muungano.Pili ni sahihi mkoa mmoja kuwa na mawaziri watatu, kutoka kwenye majimbo, wakati mikoa mingine haijatoa mawaziri kabisa.
 
Hiyo inaonakana ndo kawaida ya viongozi wetu. Maana hata JPM alikuwa anaweza mtumbua mtu na baadae akamrudisha tena. Ona kwa Simbachawene, Nchemba n.k.
 
System imeshakufa mtu anampangia njama Rais kipindi u makamu leo unamrudisha unataka tuseme ulikua kwenye NJAMA ... vetting gani mtu kama MAKAMBA ANAWEZA PITA KAMA sio Tz na UGANDA tu dunia nzima.
Mkuu ni lipi baya la Makamba linalomfanya awe hafai kurudi katika nafasi ya uwaziri ?

Maana kama kuondoka na kurudi barazani, watu wengi tu huwa wanafanya hivyo na mifano ipo.
1. Mwigulu Nchemba
2. George Simbachawene
3. Faustine Ndugulie n.k n.k

Kipi haswa mnakiona kwa January ?
 
JANUARY MAKAMBA alishaingizwa kwenye system na kuonekana ni Mpiga dili, bado anarudishwa tena.

Ataenda kuiba pesa nyingi ili aje kugombea Urais kama ilivyo ndoto yake
Kutaka kugombea urais hapo baadae (kwa mwanasiasa) haliwezi kuwa ni kosa.

Kuiba fedha za umma ni kosa kubwa sana (kwa mtu yeyote yule, sio lazima awe kiongozi au awe mwanasiasa). Sasa swali ni je, January aliiba nini, wapi na lini ?

Isaidie nchi uipendayo kwa kufichua wizi (sio sawa kutoa tuhuma za jumla jumla zisizokua na uthibitisho).
 
Kukopa 1b ktk mifuko ya jamii
Kuna mambo mawili,
1. Ni lazima iwe ni kosa kukopa kwenye mifuko ya jamii.
2. Ni lazima iwe ni kweli unayemtaja alifanya hicho ulichokisema kafanya.

Je, una hakika hayo mawili hapo juu ni kweli kwa Mh. Makamba au ni tuhuma za jumla zisizo na uthibitisho ?
 
Kuhusu January umesema kweli kweliiii kweliiiii 1000%.

Uwezo wa January ni mdogo mdogo sanaaa, he has no potential kabisa, as you said, nguvu kubwa imetumika kumweka January katika baraza la Mawaziri, ili alinde maslahi ya akina JK ya mafuta, Lake Oil and Lake Gas, pia Maslahi ya Rostam katika Gas, Taifa Gas and Mihan.

Sitegemei kama atadumu muda mrefu katika hii wizara ya Nishati, sbb kashfa ya rushwa au mikataba mibovu atakayoingia baadae au sera mbovu atakazopendekeza baadae kwa kulazimisha au upendeleo wa walimweka utadhihirika mapema na itamuondoa haraka, huwa sikoseagi kubashiri, hasa pia kikubwa kitakacho muondoa ni kutaka kugombea nafasi ya Urais hapo mbeleni, sbb ataanza makundi na mikakati mapema ili agombee, hapo CCM itamkata haraka.
 
Kwani wewe unaweza kukopeshwa na mifuko ya jamii pamoja na kuwa unaweza kuwa mwanachama
 
Unaposema WIZARA ISIYO YA MUUNGANO unamaanisha nini ?

Unamaanisha wizara yoyote ile nje na wizara ya muungano na mazingira ?

Ninachofahamu mimi kuna mambo ya muungano na mambo yasiyokua ya muungano, hakuna kitu inaitwa ''wizara za muungano" na "wizara zisizokua za muungano" hivyo tugawane uongozi wa wizara kutokana na nani anatoka upande upi wa JMT.

Labda unielimishe tena kwa mifano kwamba mtu kutoka Unguja au Pemba ni marufuku kuongoza wizara ABC....

Mtu anayetokea Pangani, Tarime au Mafinga ni marufuku kuongoza wizara XYZ....
 
Kwani wewe unaweza kukopeshwa na mifuko ya jamii pamoja na kuwa unaweza kuwa mwanachama
Ningependa sana unijibu mkuu. Ila kama umeamua mjadala uwe ni "swali kwa swali" basi sawa. Naishia hapo.
 

January amewekwa ili alinde maslahi ya akina JK na Rostam dhidi ya nani ?

Hayo maslahi yalikua yanalindwa na nani kabla January hajawa waziri wa nishati ?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…