Ninawashukuru watu hawa kabla mwaka huu kuisha.

Ameeeeen amen amen
 
Ninajua unamaswali..karibu ERon.[emoji2][emoji2]kama nitaweza kukujibu basi nitafanya hivyo
Sina maswali mkuu,
Niungane na wewe kuwashukuru watajwa hapo kwa mchango wao katika maisha yako. Wachache wanaweza ku-appreciate!
 
Ukweli mtupu BS.

Bado ndoto ya kusaidia watu ipo ndani yangu sijaisahau.
Ninajua thamani ya kutokuwa nacho na akajitokeza msamaria kutoa msaada.

Habari ya huko ulipo BS.
Nakumbuka sana ukarimu wako na Mungu atakupa na kukuongezea kila unachotoa
Mimi huku namshukuru Mungu
Naamini hata ukiweka Nia tu ni thawabu
Tuko pamoja sana
 
Ukiondoa ile uandishi wa kihuni ( kimjini mjini)...unaonekana una roho nzuri una 'appreciate'kwa kila lililo jema ulilotendewa, na unawapendea watu wapate yale yaliyo mema ...mpaka hapo tu utabarikiwa sana!

Kingine huna mambo ya kimama mama I wish uwe rafiki yangu

Cheers [emoji1635]
 
Wala usiwe na wasiwasi dada yangu, maisha yetu yapo nje ya uwezo wetu, kuna ambaye ndie alie juu ya wote, juu ya yote na juu ya vyote.
Anajua kesho yetu na kila kitu kutuhusu, usifikirie negative yoyote kutoka kwa mtu yoyote iwe kwa kusema au kuandika, neno huwa lina kata kwa makali kuliko chombo chochote chenye makali ndio maana tuna sawa sana kuwa wakimya, lakini kumbuka kwenye maandiko ya Mungu neno Usiogope limetajwa na kurudiwa mara nyingi sana, hivyo usiogope.
 
Mada yako Chakorii imenigusa sana kila kona, nimejisikia vibaya sana kwa sababu wakati inatoa shukurani kwa hao ndugu nikajifikiria kwenye mzunguko wa maisha yangu hakuna anae weza kunipa shukurani kwa sababu hakuna cha maana nilivhoweza kutoa kwa yoyote, hii ni kutokana na umaskini, maandiko yanasema atoaye ana heri kuliko apokeaye, kama huna cha kutoa ni dhahiri heri hautakua nayo.

Ingawa ingawa mimi binafsi ni mtu wa kujitoa sana , najitoa kwa hali na mali, lakini kile nikitoacho thamani yake ni ndogo so sio rahisi kumgusa mtu na kuniambia asante!

Kupitia mada hii nimejifunza mengi , kwanza kuzidi kujitoa kwa yoyote alie mbele yangu, pili kupambana sana kupunguza umaskini , tatu kushukuru kwa yoyote alie kugusa kwa namna moja ama nyingine.
 
Hakika Utauingia mwaka 2023 Ukiwa imara na mwenye nguvu kuliko huu 2022,hakuna baya litakugusa Wala kukupata.

Wewe Ni baraka sana.

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Ukiwa na uwezo wa kujicheka huwezi ishiwa vya kukuchekesha

Ni ngumu sana mtu kukaa na kuhesabu mema na wema waliomzunguka na kuwatakia Kila la kher

Watu waina yako mnakuwa na furaha muda mwingi

Hope everything is fine, all the best
 
[emoji2][emoji2]kichwa chako kibovu..

Ninapita sana tu…nitaangalia ratiba yangu itakaaje(nitasafiri siku za hivi karibuni)ili nishuke lamadi ninunue samaki.kuna samaki wengi sna pale.
Usisite kunambia ili ukute nimekuandalia samaki wengi na wa kutosha na usipete usumbufu wa kununua samaki kwenye madirisha ya gari/basi

Au utakuwa na ile gari yako pendwa?
 
Chakorii ni mtu bora Sana. Siku akiwa rafiki yako,nakuahidi utakuwa umepata rafiki bora maishani.

Unenifurahisha sana vile umesema ana uandishi wa kihuni!!

Sent from my CPH1923 using JamiiForums mobile app
 
Mungu ana mizungu mingi, hutenda kupitia watu anaowaleta yeye mwenyewe...
Hakika anko dereva.
Kuna video clip ya Ambwene mwasongwe ninatamani kuiweka hapa ukiitafakari Unaona kabisa Mungu aliwaepusha na ajali.
Nikiipata nitaiweka hapa
 
Ukiwa na uwezo wa kujicheka huwezi ishiwa vya kukuchekesha

Ni ngumu sana mtu kukaa na kuhesabu mema na wema waliomzunguka na kuwatakia Kila la kher

Watu waina yako mnakuwa na furaha muda mwingi

Hope everything is fine, all the best
Ni kweli mkuu..
Nashukuru sana mkuu.

Everything is fine mkuu ingawa watoto wananichapa maswali mnoπŸ˜€πŸ˜€
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…