Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Ningekutana na Rais leo, Nimgemwuliza kwanini amemtoa Mchengerwa Utawala Bora

Mr Q

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2012
Posts
18,046
Reaction score
38,598
Wizara ambayo ukiiangalia chini ya utendaji madhubuti wa mchengerwa , kero mbalimbali zilikuwa zinapatiwa ufumbuzi bila kuonea wala kukandamiza upande mmoja.

Alishaanza kutengeneza mifumo ambayo kwa vizazi vingi mbele vingenyoosha utendaji kazi wa watumishi na maafisa utumishi na mabosi wa maafisa utumishi.

Kifupi kila mtu angefanya kazi kama taratibu za kazi zinavyo taka.

Sio unaamka tu kwakuwa unamamlaka unasitisha likizo, unalimbikiza stahiki za mtumishi, unamcheleweshea haki zake n.k

Hayo yote Mchengerwa naona alikuwa anayanyoosha ipaswavyo.

Pengine siku moja atarejeshwa wizarani kama ilivyotokea kwa waziri wa afya Mwalimu.
kila la kheri
 
Mama chonde chonde, nakuomba tena kwa kusisitiza sana, mrejeshe Mohammed Mchengerwa Wizara ya Utumishi. Huyo bwana hapo alikuwa smart sana na alijitahidi sana kushughulikia na kutolea ufafanuzi kwa ufasaha kabisa masuala ya kiutumishi.

Huyu kipaza sauti uliyemleta utumishi naomba arudi huko kwenye sera na siasa nyingine. Mhagama ni mpiga mayowe tu na hawezi kujenga hoja, atasababisha uchukiwe bure na watumishi.

Mchengerwa ni smart sana ambaye ameanza vizuri, hupaswi kumkatisha tamaa kwa kupeleka huko.

Yule anatakiwa Utumishi au TAMISEMI. Very smart

Mwisho rekebisha jina la Wizara ya Gwajima hasa pale kwenye Wanawake na Jinsia hapajakaa vizuri maana neno jinsia linatisha sana

Kazi iendelee!!
 
Mchengerwa alikuwa very smart na alishaanza kuwafanya Watumishi waipende Serikali yao na waone inawajali of which ndiyo kazi ya kwanza ya Mwanasiasa,kupigiwa kura kunafuata.Alifanya vyema sana sijui nini kimetokea.
Inashangaza sana au kapigwa figisu kimyakimya bila mama kujiridhisha akapitisha maamuzi?
 
Laana inawatafuna na bado lichama lenu limesha kufa...
Hapa hatuamgalii lichama tunaangalia mtu ambaye kwa hakika alishaanza kunyoosha mapito ya watumishi.

Alitaka kuanzisha E-malalamiko yani ukiona haki zako kama mtumishi zinapokwa na waliovimbiwa madaraka unaclick tu moja kwa moja yanafika kwenye kitengo wizarani halafu unasubiri mrejesho. Ni moja ya mawaziri walio sisitiza sana watumishi wapandishwe madaraja na sibakizwe mtu ntuma mwenye vigezo vyote
 
Hujaona alichofanya Bungeni kusambaratisha Kambi jeuri kwa weledi na ustadi hadi wenyewe wanarukana

Sasa hivi anaenda kusambaratisha makatili waliowekwa kwny Utumishi
Hebu funguka zaidi
 
Back
Top Bottom