Nini chanzo cha ugomvi wa January Makamba na Musukuma?

Mkubwa, Kazi ya mbunge ni kuisimamia serikali. Serikali inaundwa na Rais na Mawaziri. Kwa taarifa yako, Bunge lilimvua madaraka waziri Mkuu Lowasa . Bunge likiomba iundwe kamati my friend waziri anaondoka (kama kuna makandokando)
Tayari Mbunge Mpina ameingia kuomba Kamati iundwe. Subiri moto.
Wabu ge wanawakilisha wananchi ,wananchi wanataka umeme.
 
Kwa kifupi sana, Msukuma yuko nyuma kumtetea Kalemani msukuma mwenzie na Marehemu wao katika jaribio la kuonyesha kwamba Waziri Makamba si lolote wala si chochote ndio maana Magufuli alimwachisha uwaziri na kwamba Kalemani ndio alikuwa Waziri bora kwenye hiyo wizara. Waziri Makamba nae amekuja na facts na figures muhimu kwetu sote na pia kumjuza Msukuma & company kwamba huko nyuma propaganda za uongo zilikuwa nyingi - sasa basi na kwamba Makamba yuko nyuma ya Rais wa sasa na ndio relevant. Kwa kuhitimisha, Makamba yuko sana tu na atakuwepo. Msukuma yuko vilioni bado, mithili ya Ndugu yetu Polepole.
 
Msituletee hisia za ukabila hapa. Umeme sio wa Wasukuma .Umeme ni faida kwa wote. Kwa hiyo unamtetea Mtanga mwenzio?
 
Hili suala la umeme ni sensitive issue kwa uchumi wa nchi, ila naona wadanganyika mnalijadili kisiasa zaidi. Hivi karne hii ya 21 ni nani atataka kuja kuwekeza kwenye li nchi lenye umeme wa kuunga unga?? Chief Hangaya juzi huko Ufaransa eti kaomba kiwanda cha chanjo ya Corona kijengwe : hivi wazungu gani wapuuzi watajenga kiwanda kwa umeme wa mgawo??? Kiuchumi madhara yake ni makubwa sana, ila kwa vile mmeamua sijui kuleta Usukuma gang na msoga gang basi subirini 2025 ifike tuone uchumi wa nchi ulipanda au uliteremka.

Ila ukweli utabaki mbunge Musukuma ana hoja ya msingi na huyo poyoyo Makamba hajui anachofanya kwa sasa. Kusema eti waya ziko uchi na nini sijui hizo ni mbinu tu za kutaka ulaji na kupiga pesa, angetatua kwanza suala la mgawo wa umeme kukiwa hivyo hivyo kulivyo, then hayo mengine yafuate tuone kama watu wangepiga kelele tena. Kumbukeni mara ya kwanza walisema uhaba wa mvua ... To be honest hio wizara ni kubwa sana kwa huyo seti tupu Makamba, wizara zinazomfaa ni kama ya yule seti tupu mwingine kule Habari. Kwa kumteua Nishati naona Chief Hangaya amechemsha labda awe alifanya hivyo kwa nia safi ya upigaji. 2025 sio mbali sana, ngoja tusubiri tuone jeuri ya huyu zero.
Tuzidi kula mtori nyama tutazikuta chini!!!
 
Sawa, na sisi ambao sio wasukuma na tunataka umeme ili kazi ziende mnatusaidiaje?
 
Mkuu, unachanganya sana madesa, yule aliyemsifia Magufuli ni mkurugenzi wa Kahama, wa Geita hadi leo hajarudishwa kazini mkuu; usichanganye mafaili! Bado nauliza, ni lini Msukuma aliwahi kumuongopea mtu kwa kumuonea? Kwenye issue ya umeme, January kachemka, hata kama tunampenda but pale kaingia mkenge. Ningekua karibu nae ningemshauri ile wizara asingeikubali, wizara ile haiwafai watoto wa mjini, watoto wa mjini wanapenda sana pesa, pale panaua ndoto zake za urais kabisa. Kibaya zaidi majibu alioyatoa ni mepesi mno kulinganisha na issues alizo raise bwana Kasheku Msukuma, Msukuma alijikita kwenye issue ya umeme na bwawa la mwalimu Nyerere, January aka personalize jambo!
 
😆😆
 
Sio kweli ni DED wa Geita ktk jimbo la Msukum
 
Makamba ana mizizi ndani ya CCM na inakuwa rahisi kupelekeshana na Msukuma wakiwa wabunge wa chama kimoja.

SSH anamuweka ndani ya baraza lake kwa mikakati maalum ya huko ndani ya CCM, kama akimuondoa basi Makamba atakuwa ameharibu mazima ile wazungu wanaita 'irreparable damages', kwamba ushahidi usiotiliwa shaka ndio utamuondoa pale hizi tetesi ni ngumu kuzitumia kumuondoa ukizingatia mizizi aliyonayo.
 
January ni mtoto wa mjini ifike pahali Msukuma atulie kwanza,watoto wa mjini wapo kwenye system acha wafanye ya kwao.
mama Samia ndo kamteua Makamba na anajua kinachotakiwa kifanyike kwenye swala la umeme.
nchi ndio maana haendelei kwa fikra kama hizi zako, so tuendelee kukaa giza huku tukiamini watoto wa mjini ndio waelewa kutuzidi sisi tuliokulia vijijini ?
kuna member fulani humu ndio maana juzi alisema bora mkaburu angebaki south maana weusi hatupendani
 
ninachoipendea CCM ni chama kinachowajua watanzania wengi mfano wewe hapo ndio maana wanapeana vyeo kwa kupendelea
For the record Tanzania hakuna Royal family wacha porojo zako mkuu
 
Mkuu punguza CHUKI hazita kusaidia katu abadani

Naheshiu sana maoni ya kila mmoja lakini haya yako sio maoni ni chuki binafsi
 
Mkuu punguza CHUKI hazita kusaidia katu abadani

Naheshiu sana maoni ya kila mmoja lakini haya yako sio maoni ni chuki binafsi

hili suala la umeme, wengi wameelekeza chuki binafsi zaidi kuliko hata suala lenyewe..
 
Mkuu punguza CHUKI hazita kusaidia katu abadani

Naheshiu sana maoni ya kila mmoja lakini haya yako sio maoni ni chuki binafsi
Kama tu kuulizwa maswali ya sekta iliyoko chini ya wizara yake anaona ni chuki au watu hamtakii uwaziri au watu wanamchukia Rais, sishangai mashabiki wake mkiona haya maneno ni chuki.
 
Makamba ni mhuni na tapeli kama walivyo matapeli wengine. Amekuta hatuna matatizo ya umeme keshayaanzisha tena. Sasa anajitetea kwa kumuweka Rais kwenye upumbafu wake. Ngoja tume iundwe abaki uchi.
 
Kama tu kuulizwa maswali ya sekta iliyoko chini ya wizara yake anaona ni chuki au watu hamtakii uwaziri au watu wanamchukia Rais, sishangai mashabiki wake mkiona haya maneno ni chuki.
Wanachofanya Makamba na Msukuma ni siasa
Wewe badala ya kujadili mada umeanza personal attack
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…