Nini chanzo cha ugomvi wa January Makamba na Musukuma?

Nini chanzo cha ugomvi wa January Makamba na Musukuma?

Wewe unataka kumtetea Makamba inaonekana.

Ni nani anafurahia utendaji wa Makamba? Utendaji ni kukata umeme kwa visingizio lukuki? Walisema maji, Mungu si Athumani, akaleta mvua. Sasa ndio wakaja na visingizio vya maintanance.

Anataka apewe miaka 4 kama vile ndio tumepata uhuru? Kwanini anataka kukata connection ya regime hii na nyingine?
Serikali haikatiki.

Halafu anadhani kila mtu anapenda madaraka kama yeye. Akiulizwa wajibu wake, anakimbilia kwenye madaraka.
Awajibu. Hakuna wa kudumu kwenye siasa.

Hakuna mwenye hati miliki ya uongozi. Uongozi ni dhamana.
Safi kabisa
 
Kwa aliyefatilia kikao cha Jana cha Bunge atakuwa amepata picha kile ninachojaribu kuelezea hapa.

Musukuma anamtupitia mashambulizi makali Mh Makamba kwa kutoa ushahidi wa kile alichokuwa anakiona wakati akiwa mjumbe wa kamati ya nishati kwa miaka 6 sasa.

Na Makamba anajibu mashambulizii kisomi na kitaalamu zaidi lakini mwisho wa majibu yake anamwambia Musukuma

"Kama una shida na uwaziri, sema mengine ila kama shida ni ukatikaji wa umeme ilo sio tatizo langu."

Kwa kauli ya Makamba na Musukuma inaonesha hawa watu hawako kwenye good term Liko jambo linafukuta kati ya watu hawa wawili.

Ikumbukwe Makamba ni Waziri kwa miezi minne tu, ila Musukuma ni mjumbe wa kamati kwa miaka 6, kwanini anayoelezea Makamba kamati haiyajui? Au ni makusudi ya wasukuma kujiziba masikio?

Au ni chuki maana nasikia Makamba hatoi bahasha kwa wajumbe wa kamati wakija. Kumtembelea?

Musukuma anasema Makamba anapanda Elikopita kukagua mabwawa wakati yeye anaendaga na baiskeli.

Nini kinaendelea kati ya Musukuma na Makamba?
January hajawahi kuwa smart na kama kweli ameongea jambo hilo anaonesha jinsi ambavyo hana akili. mtu unaulizwa unasema issue ni uwaziri? hii ni kauli ya mtu ampuuzi asiyejiamini na asiyetaka kuhojiwa. so anatumia kama defense of mechanism
 
kwa hiyo makamba unaamini ni kwa sababu ya uganga ndi uliomfikisha hapo ndo maana ametoa majibu ya kipuuzi
Kuna watu huwa ni washamba na waganga waganga , sasa huwa wanajisahau kama wametumia uganga uganga kufika walipo..Ndumba, utapeli, unafiki, ushamba wa kijinga, wizi mitaani ndio maisha ya baadhi ya watu..

Kuna watu wametoka royal family, wamekuzwa vizuri na kulelewa kwenye mifumo, vichwa vyao vimetulia na hata malezi yanaonekana sio mabaya.. lakini pia watu wengi wa hivi hawana mihemuko zaidi ya utulivu na tafakari.m
o
 
Kwa kifupi kabisa huyu mtu anaitwa Musukuma ni mtu wa hovyo sana na mpenda fitina za kijinga. Ameumiza watu wengi kwa fitina zake za hovyo. Naamini watawala wameelewa uhuni wake. Niishie hapo, inatosha.
Hakuna cha uhuni wowote kwa msukuma. Kwa msiojua msukuma anawakilisha mawazo.ya wananchi. Nani anafurahia utendaji wa makatani?. Toka aingie madarakani,tumeshuhudia mambo ya ovyo hapo Taneco. Mambo mengi ni ya kuwaumiza wananchi. Halafu anataka apewe miaka minne. Stupid
 
January ni mtoto wa mjini ifike pahali Msukuma atulie kwanza,watoto wa mjini wapo kwenye system acha wafanye ya kwao.
mama Samia ndo kamteua Makamba na anajua kinachotakiwa kifanyike kwenye swala la umeme.
Usimtwishe Mama mzigo.
 
Hapo hakina ugomvi ni hoja lakini mwingine anaona kama musukuma hataki awe waziri. Kwani msukuma ndo anayeteua? January ajibu tu hoja kwa nini umeme unakatika katika aachane na musukuma.
 
Yaani Makamba anabishana na PhD holder.

Kweli nchi ina vijana wa hovyo
[emoji23][emoji23][emoji23] ni kama ile amsha amsha amsha ya Mayele baada ya kumtungua golikipa wa timu pinzani.
 
Midimay Umemchambua vyema Sana mkuu, yaani Kwa mtu was hovyo hawezi kuelewa,huyu Makamba hafai,fikiria alienda kukodi App nchini lndia ya billion 4,aise!! Alafu watu wakisema mtu anatokea kutetea ujinga,Jana alikuwa akijibu kihuni bungeni.
 
Wote tu wanataka sifa waonekane kwa mwenyekiti...

Nchi hii kila kitu ni agenda,,, Siku tukijua ya kuzingatia na kuachana na yasiyotuhusu, tutapiga hatua sana
 
Umemchambua vyema Sana mkuu, yaani Kwa mtu was hovyo hawezi kuelewa,huyu Makamba hafai,fikiria alienda kukodi App nchini lndia ya billion 4,aise!! Alafu watu wakisema mtu anatokea kutetea ujinga,Jana alikuwa akijibu kihuni bungeni.
Bilioni 4?? Ni Bilion 70
 
Kwa hiyo anamwakilisha Rais kutoisimamia vzr Tanesco?
mpaka sasa hakuna ushahidi wowote kwamba Waziri ameshindwa kuisimamia Wizara, kilichopo tunachokiona ni majungu na kinyongo baada ya Waziri aliyetangulia kupigwa chini.
 
Back
Top Bottom