Mkuu, unachanganya sana madesa, yule aliyemsifia Magufuli ni mkurugenzi wa Kahama, wa Geita hadi leo hajarudishwa kazini mkuu; usichanganye mafaili! Bado nauliza, ni lini Msukuma aliwahi kumuongopea mtu kwa kumuonea? Kwenye issue ya umeme, January kachemka, hata kama tunampenda but pale kaingia mkenge. Ningekua karibu nae ningemshauri ile wizara asingeikubali, wizara ile haiwafai watoto wa mjini, watoto wa mjini wanapenda sana pesa, pale panaua ndoto zake za urais kabisa. Kibaya zaidi majibu alioyatoa ni mepesi mno kulinganisha na issues alizo raise bwana Kasheku Msukuma, Msukuma alijikita kwenye issue ya umeme na bwawa la mwalimu Nyerere, January aka personalize jambo!
Msukuma ni mtu wa kila siku kufanya madili na ndio maana ana kesi chungu nzima za kukopa benki kwa ujanja ujanja hataki kulipa huku akijifanya mfanyabiashara maarufu!! Musukuma ndio aliyemsagia kunguni yule mkurugenzi kwa Jiwe kuwa alikuwa amenunua gari bila kufuata utaratibu kumbe ni uongo!!
Kama ni suala la kupenda pesa hakuna tofauti kati yao; wawe wa mjini au wa shamba wote ni sawa; kitu kinachowaunganisha ni chama chao kinachowafuga hao chawa!!