Rev. Kishoka
JF-Expert Member
- Mar 7, 2006
- 4,526
- 1,540
- Thread starter
-
- #181
kuna hiyo document hapo nyuma ya kina Wangwe, tetesi ni kuwa ukisoma sana utagundua kiasi kilichokuwepo... i.e tupu!
Zakumi,
Hakuna sababu kubwa kama Mapaka shume..!..Utawala wa Ethipian Airways hawana Mapaka shume (Mafisadi wa ndani) kama sisi, yawezekan wakawa na Nguchilos (mafisadi wa nje)..Kisha Kumbuka mkuu wangu Ethipian Airways ilianza toka mwaka 1948 na Wamarekani nafikiri ilikuwa TWA kama sikosei kufungua tawi lao Afrika...
Na ktk miaka ya 80 wamechukua tuzo za DUNIA kama Airline bora mara tatu, Marubani bora mara mbili kwa hiyo huwezi kabisa kupima vitu hivi viwili...
Ktk swlaa la Kubinafsisha ATC hatukulazimishwa isipokuwa ktk kuchukua mikopo mkuu wangu ni lazima uweke rehani..Kama huna cha kuweka rehani mwenye kutoa mkopo anakuwa na masharti yake. Acha hizo benki za Dunia hata wewe ukitaka kunipa Mkopo mimi hapa Mkandara utataka kupata uhakika wa mkopo wako kurudi aidha niweke rehani shamba langu, gariu langu au hata mke wangu.. kama siwezi basi utaniwekea masharti ya fedha hizo kutoka...inawezekana ukasema ni lazima nishirikiane na mdogo wako ktk shughuli hiyo..
Hiki ndicho kinachoendelea siku zote ktk mikopo yetu, tunalia masharti magumu ni kwa sababu hatuna kitu benki.... hatuna kitu.. mwalimu alivuta ndege mbili mpya toka Boieng, leo ati tunadai tuna akiba tunaenda nunua ndege zilizokwisha simama zimewekwa uwanja wa kuuza parts!..Kama sio mapaka shume kitu gani mkuu nambie wewe..
Damn ni aibu mkuu wangu ni aibu kubwa kujaribu kufikiria unaweza kubadilisha maisha ya wakazi wa uwanja wa fisi kwa kutumia vitabu.. Hapana ni lazima uishi uwanja wa fisi (nchi maskini) upate kuelewa maisha yao, mazingira yao, tabia zao na taabu wanazopitia kisha ndo unapanga strategy na vipaumbele..Unaposema swala hili ni complex ni muhimu ujue kwamba hakuwezi kutegemea kitabu lingekuwa sio complex nakubali vitabu vinaweza kabisa kujibu..
Is there possibility kuwa Tanzania mpaka sasa haijajiandaa kujijenga kiuchumi na miundo mbinu kulingana na ongezeko la raia na kusambaa kwa watu kutanda nchi nzima?
Ikiwa motisha wa uhujumu ulikuwa ni kujipatia cha ziada, tukirudi kwenye theory zetu za supply na demand, na hata hoja ya kuwa viwanda viliishia au mwanzo wa mapungufu ya bidhaa na huduma, je zilikuwa ni sababu ya 1. Uhujumu, 2. uongozi mbaya, 3. kukosekana utaalamu na ufanisi, 4. ongezeko la watu, 5. ushindani wa kibiashara na bidhaa kutoka nje, 6. kushuka kwa thamani ya shilingi, 7. njaa na ukame uliotawala kanda ya Afrika mashariki, 8. vita vya kagera, 9. ubeberu wa IMF na nduguze?
Huh!?!? Kama kulikuwa hakuna hela (i.e. tupu, zero) kwa nini inabidi mtu uisome "sana" hiyo ripoti ili kugundua kiasi kilichokuwepo? Si namba hazidanganyi, au?
Hile paper haikupi namba moja kwa moja. Inabidi ufanye deduction. Ninaweza kutoa hints tu, jinsi ya kuitumia hiyo paper kupata number.
hizi ni hints:
-Mwaka 1984 sehemu kubwa la pato la taifa lilitegemea uuzaji wa mazao ya kilimo.
-Mwaka 1984 kilikuwa ni kipindi cha ukama. Hivyo mapato yalipungua kutokana na ukame.
-Mwaka 1984 (mpaka sasa) zaidi ya 50% ya bajeti ilitegemea wahisani. Wahisani wengi walijitoa kushinikiza mabadiliko.
-Mwaka 1984 bei ya mafuta ilikuwa sio nzuri kwa mtumiaji
-Mwaka 1984 Tanzania ilikuwa na uhusiano mbaya na vyombo vya fedha kama IMF.
Summary ya hizo hints ni kuwa hazina ilikuwa tupu.
Dogo watu wengi hawakwambii kuwa wapo broke, atakachosema ni kuwa hajapata paycheck yake au paycheck ya sasa anaitumia kulipa pango.
Hile paper haikupi namba moja kwa moja. Inabidi ufanye deduction. Ninaweza kutoa hints tu, jinsi ya kuitumia hiyo paper kupata number.
hizi ni hints:
-Mwaka 1984 sehemu kubwa la pato la taifa lilitegemea uuzaji wa mazao ya kilimo.
-Mwaka 1984 kilikuwa ni kipindi cha ukame. Hivyo mapato yalipungua kutokana na ukame.
-Mwaka 1984 (mpaka sasa) zaidi ya 50% ya bajeti ilitegemea wahisani. Wahisani wengi walijitoa kushinikiza mabadiliko.
-Mwaka 1984 bei ya mafuta ilikuwa sio nzuri kwa mtumiaji
-Mwaka 1984 Tanzania ilikuwa na uhusiano mbaya na vyombo vya fedha kama IMF.
Summary ya hizo hints ni kuwa hazina ilikuwa tupu.
Dogo watu wengi hawakwambii kuwa wapo broke, atakachosema ni kuwa hajapata paycheck yake au paycheck ya sasa anaitumia kulipa pango.
Matumizi yako ya maneno "hazina ilikuwa tupu" sio sahihi. Kuwa na bajeti tegemezi zaidi ya asilimia 50 haimaanishi utupu! Ungesema asilimia 100 ya bajeti yetu ni kutoka kwa wahisani ungeweza kuwa sahihi kwa kiasi fulani.
Sehemu kubwa ya pato la taifa mwaka 1984 kutegemea mazao ya kilimo haimaanishi utupu. Kama sehemu kubwa ilitegemea mazao ya kilimo, sehemu ndogo ilitegemea nini?
Kupungua kwa pato kwa sababu ya ukame haina maana tulikuwa tupu. Kupungua sio kuisha. Kama hujui maana ya maneno hayo tafuta kamusi.
Kupanda ama kushuka kwa bei ya mafuta sijui kuna husiana vipi na hazina yetu, hata hivyo, haimaanishi tuliishiwa kabisa. Labnda unambie tulipata msukosuko na ikabidi tujifunge mikanda.
Uhusiano mbaya na mashirika ya fedha haimaanishi tuliishiwa tukabaki hatuna hata shilingi moja.
Sasa nikuulize wewe, maana ya kuwa tupu ni nini? Ni kuishiwa kabisa na kuwa huna hata senti moja au ni kupungukiwa, let's say, kutoka shilingi mia moja hadi shilingi arobaini na tano?
Na mtu akikwambia kuwa yuko broke, wewe unaelewa anamaanisha nini? Kuwa hana kitu kabisa au?
Ni viongozi wa juu kabisa waliotumia msamiati huo. Na ndugu Warioba na Mwinyi.
Lakini kwa sababu inaonyesha kuwa utupu ni msamiati mwenye utata. Basi naomba msamaha wajemeni.
Katika sehemu zote nilizosema kuwa Hazina ilikuwa tupu naomba ieleweke kuwa kulikuwa na ukame Hazina.
Zakumi.. you I really like your style. Katika maandishi yako hapa chini umefanya vitu viwili (ambavyo sikutegemea kama ungevifanya)
a. Umefuta matumizi ya maneno "hazina ilikuwa tupu" kwa kuonesha kuwa tulikuwa na vitu vyetu sisi wenyewe, na ya kuwa upungufu wa fedha za kigeni haina maana kuwa hazina ilikuwa tupu. Kwa maneno mengine, kwamba kiongozi kuchagua kati ya "kugomboa meli moja" na kuhakikisha wananchi wake wana chakula kiongozi mzuri haendi kugomboa meli!
b. Pili umefanya jambo nililolisema tangu mwanzo kuwa matatizo ya 1984 kuyaweka juu ya mtu mmoja siyo ukweli wa historia na ya kuwa matatizo ya kiuchumi ya wakati ule yalikuwa complex. Wewe mwenyewe umesema yafuatayo ambayo nakubaliana nawe 100%
Hapa unaelezea the complexity of our economic situations at the time. (yaani siyo suala la uzalishaji tu na uongozi au sera mbaya)
check!
Check! Nyerere hakuwa na uwezo wa kuzuia ukame; ukikumbuka vizuri ukame huo haukuwa exclusive to Tanzania. Ni wakati huo huo njaa kubwa kabisa ya Ethiopia ilitokea! Lakini kwanini Tanzania maelfu ya watu hawakufa kwa njaa? (wakongwe tunakumbuka "Unga wa Yanga na mafuta "From USA".
check!
check!
check! neno "mbaya" halitafsiri hasa kilichotokea; tulikuwa na uhusiano wenye mashaka na miaka michache baadaye tunajua ni kweli tulikuwa sahihi!
Sijui kama una mwalimu wa Logic kwa sababu the conclusion doesn't follow the premises! not in a long shot! Nice try though.
Mtu akisema yuko "broke" ana mana hana fedha taslimu' lakini haina maana hana kitu kingine. Na mtu anaweza kuwa broke kwa sababu ya a. kutokuwa na fedha inayoingia au b. fedha inayoingia kwenda moja kwa moja kwenye matumizi c. yuko katika subira ya kupata fedha.
Hata hivyo matumizi yenu (wewe na JokaKuu) kuwa hazina ilikuwa tupu, still yanabakia kuwa was purposeful misleading kwa watu ambao hawajui historia ya nchi yao. Kwa vile umeifuta hiyo, tusonge mbele.
BTW: Nyani, majibu yako yamenifanya niteremshie na mirinda!
Joseph Warioba said:Mwaka 1985 hatukuwa na akiba ya fedha za kigeni. Tulikuwa tunashindwa hata kulipia meli moja ya mafuta.....
Zakumi,MKJJ,Nyani-Ngabu,Mkandara,
..naona ktk kuielezea hali ya kifedha ilivyokuwa hazina 85 turejee kauli ya Joseph Sinde Warioba, ambaye wakati huo alikuwa Waziri Mkuu.
..Zakumi ametoa listi ya economic challenges za wakati ule. lakini kila uongozi hukutana na challenges za aina moja au nyingine.
..umahiri wa uongozi wowote ule hupimwa kutokana na challenges ilizokutana nazo, hatua zilizochukuliwa, na matokeo ya hatua hizo.
..hakuna ubishi kwamba matokeo ya hatua za kupambana na uchumi miaka ile yalikuwa mabaya. uchumi uliendelea kutitia, na ilipofika 85 ndipo yakatokea hayo ya "Hazina na meli ya mafuta." kwa msingi huo hatua zilizokuwa zinachukuliwa hazikuwa nzuri.
..ndugu zangu, ikifika mahali kwamba kama taifa tunakuwa na option ya aidha kukomboa meli moja ya mafuta, au kushughulika na mambo mengine, ujue uongozi umelikoroga kweli kweli.
..naomba tuzingatie kwamba wakati huo serikali ndiyo walikuwa waagizaji wakuu wa mafuta. je, hali hiyo ingeendelea mwezi mmoja, miezi sita, au mwaka mmoja, hali ingekuwaje ndani ya nchi?
..HALI YETU KIUCHUMI ILIKUWA MBAYA SANA. NI VIZURI TUKAJIFUNZA WAPI TULIKOSEA ILI TUSIJE KURUDIA MAKOSA YALE.
NB:
..Zakumi umetoa hoja kwamba bei ya mafuta ilipanda miaka ya 80. naomba kukumbusha kwamba hali hiyo ilitokea miaka ya 70 na uchumi wetu haukuyumba sana. kwa msingi huo miaka ya 80 tulitakiwa tuwe na uwezo na maandalizi ya kupambana na hali hiyo.
..pia kwa nchi inayotegemea misaada kwa zaidi ya 50% ya budget, siyo busara kuwa na mahusiano mabaya na wafadhili wetu na vyombo vya fedha vya kimataifa.
Zakumi.. you I really like your style. Katika maandishi yako hapa chini umefanya vitu viwili (ambavyo sikutegemea kama ungevifanya)
a. Umefuta matumizi ya maneno "hazina ilikuwa tupu" kwa kuonesha kuwa tulikuwa na vitu vyetu sisi wenyewe, na ya kuwa upungufu wa fedha za kigeni haina maana kuwa hazina ilikuwa tupu. Kwa maneno mengine, kwamba kiongozi kuchagua kati ya "kugomboa meli moja" na kuhakikisha wananchi wake wana chakula kiongozi mzuri haendi kugomboa meli!
b. Pili umefanya jambo nililolisema tangu mwanzo kuwa matatizo ya 1984 kuyaweka juu ya mtu mmoja siyo ukweli wa historia na ya kuwa matatizo ya kiuchumi ya wakati ule yalikuwa complex. Wewe mwenyewe umesema yafuatayo ambayo nakubaliana nawe 100%
Hapa unaelezea the complexity of our economic situations at the time. (yaani siyo suala la uzalishaji tu na uongozi au sera mbaya)
check!
Check! Nyerere hakuwa na uwezo wa kuzuia ukame; ukikumbuka vizuri ukame huo haukuwa exclusive to Tanzania. Ni wakati huo huo njaa kubwa kabisa ya Ethiopia ilitokea! Lakini kwanini Tanzania maelfu ya watu hawakufa kwa njaa? (wakongwe tunakumbuka "Unga wa Yanga na mafuta "From USA".
check!
check!
check! neno "mbaya" halitafsiri hasa kilichotokea; tulikuwa na uhusiano wenye mashaka na miaka michache baadaye tunajua ni kweli tulikuwa sahihi!
Sijui kama una mwalimu wa Logic kwa sababu the conclusion doesn't follow the premises! not in a long shot! Nice try though.
Mtu akisema yuko "broke" ana mana hana fedha taslimu' lakini haina maana hana kitu kingine. Na mtu anaweza kuwa broke kwa sababu ya a. kutokuwa na fedha inayoingia au b. fedha inayoingia kwenda moja kwa moja kwenye matumizi c. yuko katika subira ya kupata fedha.
Hata hivyo matumizi yenu (wewe na JokaKuu) kuwa hazina ilikuwa tupu, still yanabakia kuwa was purposeful misleading kwa watu ambao hawajui historia ya nchi yao. Kwa vile umeifuta hiyo, tusonge mbele.
BTW: Nyani, majibu yako yamenifanya niteremshie na mirinda!
Nyani Ngabu said:Hakuna mtu aliyebisha kuwa hali ya mwaka 85 ilikuwa mbaya. Kama kuna mtu anadhani sisi hali yetu ilikuwa mbaya kihivyo, basi aangalie picha na asome habari za nchi kama Ethiopia wakati huo....
Nyani Ngabu said:Na when push comes to shove, mimi nitamchagua kiongozi atakayehakikisha watu wake hawafi njaa kuliko yule atakayeweka kipaumbele kugomboa meli.....
Nyani Ngabu,
..labda sijawaelewa vizuri MKJJ na Mkandara. lakini kila tukisema tulikuwa na hali mbaya in the 80s basi hawa wawili wanapandwa na hasira.
..off course, Ethiopia walikuwa na hali mbaya kuliko sisi. lakini pia zipo nchi kadhaa za kiafrika zilikuwa na hali nzuri kuliko yetu.
..ninachojaribu kusisitiza siku zote ni wa-Tanzania kujaribu kujifunza toka kwa wale waliofanikiwa zaidi yetu. pia tujifunze kuepuka makosa ya wale wanaofanya vibaya, kama Ethiopia etc etc.
..as long as kuna ya Kiafrika inayofanya vizuri, hata iwe ni moja, basi kuna kila sababu ya sisi pia kujitahidi kufanya vizuri.
Nyani Ngabu,
..uchumi wetu ulikuwa unadhoofika mpaka 85 wakati Mwinyi na Warioba wanaingia ofisini ndiyo wanakuta hali kama hiyo. kwamba, hazina ina hali mbaya sana kiasi kwamba hawana hata uwezo wa kukomboa meli moja ya mafuta. hili halikuwa tukio la kushtukiza.
..ni hali ya hatari sana kwa nchi kama Tanzania kukosa mafuta. kuna shughuli nyingi sana za kiuchumi zingeweza kusimama.
..serikali inaweza kushindwa kutekeleza majukumu muhimu kama kuhakikisha wananchi hawafi njaa ikiwa kutakuwa hakuna mafuta. kwa mfano chakula kitasafirishwa vipi toka maeneo yenye surplus kupeleka kwenye maeneo yenye upungufu?
..ni kwasababu hizo hapo juu ndiyo maana wengine tunasema it was a critical moment, and we are thankful to the countries that came to our rescue.
Zakumi,
..nakubaliana na mwelekeo wa hoja zako. kama nilivyoeleza kila uongozi utakutana na challenges za aina fulani.
..suala hapa ni kuangalia njia ambazo tungetumia kukabiliana na challenges za miaka ile. vilevile tujiandae ili kuepukana na matatizo yaliyotokea in the 80s.
..umesema kweli kwamba hatuna tunachojifunza kama taifa. kwa mfano tunaelekea kurudia makosa ya mpango wa UPE ktk huu mpango mpya wa elimu.
..
Hakuna mtu aliyebisha kuwa hali ya mwaka 85 ilikuwa mbaya. Kama kuna mtu anadhani sisi hali yetu ilikuwa mbaya kihivyo, basi aangalie picha na asome habari za nchi kama Ethiopia wakati huo....
Na when push comes to shove, mimi nitamchagua kiongozi atakayehakikisha watu wake hawafi njaa kuliko yule atakayeweka kipaumbele kugomboa meli.....
Kweli, hali yetu kiuchumi haikuwa nzuri na mpaka sasa sijaona mtu yeyote hapa anayedai mambo yalikuwa hunky dory! Lakini pia si sahihi kusema kwamba hazina yetu ilikuwa tupu, hakiuwa hata na senti moja! Kwani kodi walizokuwa wanalipa watu zilikuwa zinaenda wapi? Sasa Jokakuu wewe huoni kusema kwamba hazina ilikuwa tupu kabisa ni upotoshaji?
...acha kujifananisha na Ethiopia ya wakati ule,walikuwa vitani kwa miaka mingi na Eritrea chini ya Dikteta Mengistu ambaye alikuwa haruhusu chochote kutoka nje na pesa,misaada na akiba yote ya chakula ilikuwa inaenda kwa wanajeshi,Ethiopia walikuwa na jeshi kubwa kuliko yote Africa wakati huo na budget yote ilikuwa inaenda jeshini,sasa TZ kulikuwa na nini zaidi ya uongozi mbovu tuu na siasa mbovu?