Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Alipiga vinara wote wa Yale maandamano walitumika maaskari wadunguaji yaani snipers wa Taifa...na ule huwa ni uamuzi wa mwisho pale maandamano yanapokuwa ni ya kiuhalifu na hata kuleta mauaji.
sasa unaambiwa acha kuandamana unajifanya husikii na kujiona wewe ni imara zaidi.utapigwa tu maana hamna namna.
 
Chanzo kwanza mkutano ya hadhara ya nje ya nyumba za ibada ,kukashifiana
Pili mikutano/hutba ndani ya ibada kuhusu kukashifu dini za wengine
Tatu,kuishambulia serikali kuhusu Mambo ya kidini ndan ya ibada.mambo ya mabucha ya nguruwe nk

Chanzo walipoamuliwa kutii walikaidi nguvu ya kadri ilivyotumika wakaongeza nguvu wakishambulia na kurudi misikitini...kilichotokea Ni maamuzi magumu.
Walikamatwa wakristo na waislam kwa kuwa waliokamatwa walikua eneo la tukio hata mpita njia pia alikamatwa.
 
Sababu ilikua Waislamu walitaka kulazimisha watu wasile Kitioto. Pale kulikua na bucha la kitimoto likiitwa Mbokomu. Waislamu wenye msimamo mkali wakiongozwa na huyo mwanaharakati Ponda na kina Mwaipopo walivamia bucha. Ila wanabahati hawakwenda kigogo maana huko wachaga walijiandaa na bisibisi za milunda ya nondo kungetokea mauaji. Walidhani sababu rais ni muislamu angewapendelea kwa ujinga wao. walisahau tanzania ni ya dini nyingi
Nasikia Mwaipopo aliokoka
 
Mauaji ya mwembechai yalikuwa ni kilele cha kilio cha waislamu juu ya ubaguzi dhidi yao wa siri na dhahiri katika nyanja nyingi hususan elimu na ajira serikalini, Serikali ya Mwalimu haikufanya vya kutosha kubridge gap kati ya Wakiristo waliokuwa na advantage kielimu toka wakati wa mkoloni. Hata shule za Kanisa ambazo Nyerere alitaifisha kwa hoja kwamba Watanzania wote wasome haikusaidia kwa sababu gepu la kielimu liliendelea. Na badala ya Nyerere kujenga shule mpya nyingi yeye alitaifisha zilizokuwepo ambazo bado ziliendelea kuwa chache na ndiyo maana watoto walikuwa wakifaulu primary school hawachaguliwi kutokana na uhaba wa shule za Sekondari.

Viwango na idadi ya waislamu chuo kikuu ilikuwa ni ndogo sana na serikali ya Nyerere na ya Mwinyi ambayo iliendelea kuwa under watch kali ya Nyerere kama Mwenyekiti wa CCM hadi mwaka 1990 haikuweza kuaddress tatizo hili.

Mkapa alivyoingia madarakani alikuta tatizo hili limefikia peak, mihadhara ilikuwa ni sehemu mojawapo tu ya waislamu kufikisha grievences zao kwa serikali.
Mkapa akaona atoe kile chuo cga TANESCO morogoro kuwapa waislamu ili kupunguza gepu na kilio hiki cga waislamu kuwa marginalized kwenye elimu.

Alipoingia JK akafanya kazi nzuri sana ya kujenga shule za kata kila nchi, kwa hiyo waislamu wakaweza nao kuaoma kwa wingi na pia JK akapandisha hadhi vyuo vya advanced diploma na kuvifanya vitoe digrii kwa hiyo katika mazingira haya huwezi kuwabagua tena waislamu.
Katika ishu ya teuzi, Kikwete alijirahidi kuteua teua na waislamu kwa wingi kidogo ijapokuwa wakiristo overall waliendelea kuwa wengi.

Alipoingia Magufuli, amejaribu kurudisga nyuma mafanikio haya ya kubalance demography za taifa katika utumishi wa serikali.Teuzi za Magufuli zinanuka Udini.
Proportiaonally ukiangalia idadi ya ma RAS, MaDAS, Wakuu wa wilaya, Wakuu wa Mikoa, Wakurugenzi wa Mashirika ya Umma, Mawaziri, Manaibu Waziri, Wenyeviti wa Bodi Waislamu ni wachache mno kulinganisha na proprtion yao katika hii nchi.
Kitila mkumbo kabla hajaenda CCM aliandika makala juu ya hili akasema ni muhimu kwa kiongozi kubalance demography za kitaifa ktk utumishi wa serikali.
Magufuli aishukuru sana BAKWATA na Sheikh mkuu, hawa wamekuwa kama nguzo yake kuu katika kutuliza munkari wa waislamu, lakini kiukweli lazima ukweli usemwe Teuzi za serikali y awamu ya tano zinanuka udini.

Na kama akishinda uchaguzi ujao akaendeleza teuzi za hivi basi ajue matatizo mengi ya utawala wake kupigwa vita sababu mojawapo ni yeye kushindwa kubalance force za demography kwenye watu wa kumsaidia kazi. Akimarginalize watu ajue pindi anapohitaji force za kumuunga mkono anaweza asizipate na kibaya zaidi inajenga chuki kali kwa wananchi ambao wanahisi wanatengwa
Ila miaka ya nyuma waislamu walikuwa wanaweka msisitizo Sana kwa watoto wao kwenye elimu ya dini kuliko elimu dunia Kama wanavyoita na hii ilisababisha Hilo gap unalozungumzia namaanisha kwenye ajira na vyuoni hata katika shule za sekondari
 
Ila miaka ya nyuma waislamu walikuwa wanaweka msisitizo Sana kwa watoto wao kwenye elimu ya dini kuliko elimu dunia Kama wanavyoita na hii ilisababisha Hilo gap unalozungumzia namaanisha kwenye ajira na vyuoni hata katika shule za sekondari
Jhounne,

Haiwezekani kuielewa ahadi ya Nyerere katika haki na usawa kwa raia wote kama alivyoahidi wakati wa kudai uhuru, hadi usome hotuba yake aliyoitoa tarehe 10 Desemba, 1962 katika Bunge wakati Tanganyika inakua jamuhuri.

Hotuba ya Nyerere ilijikita kwenye matatizo ya upogo kati ya Waislam na Wakristo.

Nyerere alifanya hivi labda akijua kuwa ingawa yeye alikuwa Rais Mkatoliki lakini alipata uongozi wa Tanganyika kwa msaada mkubwa wa Waislam wakati wa kupigania uhuru wa Tanganyika.

Nyerere alikuwa na haya ya kusema:

''Hakuna njia nyepesi ya kuondoa tafauti baina ya raia wetu Waafrika na wasio Waafrika; hakuna njia nyepesi ya kuondoa tofauti za elimu kati ya Wakristo na Waislam, au baina ya wachache wenye elimu na wengi wa watu wetu wasio kuwa na elimu; hakuna njia nyepesi ambayo Wamasai na Wagogo wanaweza wakalingana na Wahaya na Wachagga na Wanyakyusa.''

Hii ilikuwa kauli ya serikali ya kudhihirisha nia yake njema.

Kauli hii ilikuwa ya kuwapa matumaini na kuwahakikishia Waislam na wale wote walioathirika na dhulma ya wakoloni, kuwa serikali ilikuwa inatambua shida zao na itachukua hatua zifaazo kurekebisha hali hiyo.
 
Kwenye amani ya nchi hatutaki watu waichezeee,,narudia tena iwe kwa gharama yeyote ilindwe,watu tuendelee kuvuta hewa ya mungu kwa amani,tuchati kwa amani,.n.k

Ukiyaangalia maelezo ya watoa comment hapo juu unabainisha pande kuu mbili,upande wa serikali na upande mwingine,upande mwingine bado unayale mafunzo ya dini kwa hiyi ni ngumu kuelewana,lakini ukiunganisha vidot unaona kuna viji boko haram,alpaeda IS,alshabab vilikuwa vinataka kupandikizwa kwenye jamii fulani kwa matakwa yao.sasa nchi yetu haina itikadi ya imani fulani ....
 
Ndio nilikua karume primary school miaka ile,hlf nyumba ya babu ndio imepakana na mlango wa kuingilia msikitini upande wa akinamama,so nyumba yetu ilikua iko ndani ya tando la wale jamaa wa gomez!nikikumbuka maisha tuliyokua tunaishi kwa wakati ule mchache!
 
Kwenye amani ya nchi hatutaki watu waichezeee,,narudia tena iwe kwa gharama yeyote ilindwe,watu tuendelee kuvuta hewa ya mungu kwa amani,tuchati kwa amani,.n.k,
Ukiyaangalia maelezo ya watoa comment hapo juu unabainisha pande kuu mbili,upande wa serikali na upande mwingine,upande mwingine bado unayale mafunzo ya dini kwa hiyi ni ngumu kuelewana,lakini ukiunganisha vidot unaona kuna viji boko haram,alpaeda IS,alshabab vilikuwa vinataka kupandikizwa kwenye jamii fulani kwa matakwa yao.sasa nchi yetu haina itikadi ya imani fulani ....
Humu hakuna jibu la sababu za yale mauwaji,tunachotaka kujua wengine huku ni uhalali wa yale mauaji ni nini hasa kilichopelekea hadi ikatumika nguvu ya kiasi kile ni kwamba ni hizo karate tu tunazoambiwa au kulikuwa na nini hasa? Sasa badala ya watu kuelezea uhalisia wa tukio naona wanazunguka tu zunguka tu.
 
S

Sio unyama tatizo wananchi wa tz mnavoishi kwa amani hivi na uhuru wote mlionao wa kutukana, kudharau mamlaka na mengine meengi hadi mnajipa kiburi dawa yenu ilikua ni kukumbushwa kwa stahili ile ya mwembe chai kuwa amani ya nchi huwa haichezewi! Kwani baada ya pale somo si lilieleweka vizuri sana hadi leo na ndio maana bado tunakumbushana kwa mada kama hizi kuwa serikali ipo. Ungekuwa unaishi zenye vurugu huko waliozoea vichapo leo usingehoji elimu ile mubashara ya mwembe yanga.
Reasoning ya watanzania bwana kwahiyo kuua watu ndio kutoa somo??vipi Kenya na kuua masheikh ndio ugaidi umeisha?? Vipi somalia na Iraq violence imemaliza mgawanyiko wa watu na usalama kudorora??

Hivi mpaka marekani iliamua kuingia kwenye mazungumzo na Taliban unadhani ni wajinga? Wamegundua violence na mabavu sio njia pekee ya kuleta amani au usalama.

Msijitie kiburi sababu mnapambana na raia wasio na silaha...... Mkipambana na vikundi kma Al Shabaab au Boko Haram ndio mje kujisifu hapa sio dharau na kejeli kuua raia wasio na silaha.

Shame on you
 
Muislam safi unashindwa hata kuandika Assalaam alaykum+Taqbir,

Hahahaha.
Aslamwalekhum
Serikali ni kichwa dini ni masikio na sio kinyume chake. Masikio yanapotaka kuzidi kichwa haitaleta picha nzuri,
Dini ibaki kuwa dini, na hakuna sababu ya kuleta uwiano sawa wa serikali katika watu wa dini.

Yaliotokea yameyokea lakini tujifunze mipaka yetu mashekh wenzangu, ya kaisari yabaki kwa kaisari na ya mungu tumuachie mungu

Mimi kama muislam swafi hadhia ya mwembe chai chanzo kilikua sis wenyewe waislam ukweli ambao hatuutaki kuusikia (mtanisamehe kwa hili)
Tunatumia nguvu katika kuaminisha uislam ni dini ya kweli na haki, mihadhara isiyo na tija na tunajisahau kwa maneno ya kashfa katika dini za wenzetu tunafika mbali hadi kuingiza itikadi zetu kitaifa (hili taifa haliamini katika dini )

Mafunzo ya karate na Kong fu tunajilinda na nani??? Kwani jeshi la kulinda nchi halipo??? Hayo mafunzo yapo katika misingi gani??? Mafunzo ya karate katika nyumba za ibada tunaabudu mungu au tunaandaa jeshi??? Kwanini mafunzo ya karate yanakua kama ya lazima kuna ajenda gani??? (Hapa kuna maswali mengi yasiokua na majibu)

Takbil.....
 
Nanachojua ni umavimavi wa sheikh Ponda kujifanya wafuasi wake wanaweza kutumia upanga dhidi ya bunduki.
Hapa Ponda kasingiziwa. Shida ilianzia pale kwenye kile kikundi cha "Yesu sio mwana wa Mungu" mahubiri/mihadhara yao ilichukua muda mrefu sana bila reaction yoyote kutoka kwa Wakristo, kilipokuja kile kikundi cha bwana Simbaulanga cha "Biblia ni JIBU" ndipo sasa ikaanza kuonekana eti serikali ina mfumo "Kristo" Kina "askofu" Mwaipopo walitukana Ukristo weee na Wakristo wakawa kimya tu miaka yote, Kina Simbuulanga wakaaanza kuonesha jinsi mtume Mohamadi alivyo pewa utume na kuonesha idadi ya kina mama aliokula nao URODA, weee, watu wakakosa uvumilivu, yaliotokea ni historia tu. Nilikuwepo Dar mwaka huo, nakumbuka vizuri sana
 
Humu hakuna jibu la sababu za yale mauwaji,tunachotaka kujua wengine huku ni uhalali wa yale mauaji ni nini hasa kilichopelekea hadi ikatumika nguvu ya kiasi kile ni kwamba ni hizo karate tu tunazoambiwa au kulikuwa na nini hasa? Sasa badala ya watu kuelezea uhalisia wa tukio naona wanazunguka tu zunguka tu.
Mauwaji ni baada ya kuamuliwa kutii Bila shuruti hawakutii
Mabomu ya machozi yalipotumika waliojibu mapigo.
Hapo ndipo risasi za moto zikatumika.
Hoja je yalikua halali?vifo ni matokeo ya mvutano umkumbuke nguvu inaongezwa kadri majibizano yanavyo ongezeka.
Baada ya Askari kuanzia kuzidiwa nguvu na kupigwa kwa wakati huo ilikua ni namna gani wataweza kudhibi.jibu ikawa risasi.kwa kusema je uhalali upo au haupo lazima
Humu hakuna jibu la sababu za yale mauwaji,tunachotaka kujua wengine huku ni uhalali wa yale mauaji ni nini hasa kilichopelekea hadi ikatumika nguvu ya kiasi kile ni kwamba ni hizo karate tu tunazoambiwa au kulikuwa na nini hasa? Sasa badala ya watu kuelezea uhalisia wa tukio naona wanazunguka tu zunguka tu.
Chanzo Cha mauaji ni wahusika
Mosi,kukaidi amri halali ya jamhuri
Pili,kuanzia kujibizana na jamhuri
Tatu,kuwajeruhi Askari na wapita njia.
Hapo jamhuri ikatumia nguvu kurudisha Hali km ulivyo nje ya hapo Askari wangekwisha
 
Back
Top Bottom