Wewe umepatia, haikuwa Sheikh Issa Ponda, kulikuwa na Sheikh Shabani MAGEZI na Mwenzie nimemsahau jina,ila nakumbuka kitu kama (MAZINGE), mmoja kati yao alikatwa mguu akaachana na mihadhara kabisa. Msikiti wa mwembe chai ndio ulikuwa base yao.Hapa Ponda kasingiziwa. Shida ilianzia pale kwenye kile kikundi cha "Yesu sio mwana wa Mungu" mahubiri/mihadhara yao ilichukua muda mrefu sana bila reaction yoyote kutoka kwa Wakristo, kilipokuja kile kikundi cha bwana Simbaulanga cha "Biblia ni JIBU" ndipo sasa ikaanza kuonekana eti serikali ina mfumo "Kristo" Kina "askofu" Mwaipopo walitukana Ukristo weee na Wakristo wakawa kimya tu, Kina Simbuulanga wakaaanza kuonesha jinsi mtume Mohamadi alivyo pewa utume na kuonesha idadi ya kina mama aliokula nao URODA, weee, watu wakakosa uvumilivu, yaliotokea ni historia tu. Nilikuwepo Dar mwaka huo, nakumbuka vizuri sana
Walikuwa wanashindana na kikundi cha BIBLIA NI JIBU kiliongozwa na Simbaulanga na Ndimbo.
Huyu ponda alikuwa na kitu walikiita BALKUTA lilikuwa linafadhiliwa na waturuki fulani kama sikosei. Hawa walikuwa na ugomvi wao na Bakwata na Serikali.
Miaka hiyo nilikuwa naishi Mtaa wa Matombo jirani na msikiti wa sheikh Yahaya, bondeni kuelekea Mburahati.
Mwembe chai ilikuwa mwembe chai kweli, migahawa ya chai mingi na mama ntilie wa kumwaga, Gereji za kumwaga na zile deal za Magomeni zilifanyikia hapo mwembe chai hiyo.