Chinchilla, nadhani huwa humwelewi huyo unayemjibu na wengine wa aina yake, kila wanaposema "waislam".
Maana yao ya 'waislam' ni wale ambao hawapo kwenye mlengo wa BAKWATA. Wengi, kama sio waislam waliowahi kuwa viongozi serikalini, hawa watu hawawatambui kuwa ni 'waislam.' kwa vile wameegemea ndani ya BAKWATA au hawatambui kundi la waislam wanalolikubali wao.
Tatizo lipo hapo na litaendelea kuwepo hapa nchini kwa sababu sioni njia ambayo serikali ya aina yoyote hapa Tanzania itakubali wanayoyasimamia wao.
Lile kundi la wazee wa Dar es Salaam, analolipa sifa ya "mchango wa waislam ulikuwa hauna mfano...); tatizo lilianzia hapo ilipogundulika kuhusisha dini ndio iwe inaongoza siasa. Na hili ndilo linalohitaji kuelezwa watu wajue.
Kalamu1,
Nakushukuru sana kwa kuwaleta BAKWATA katika mjadala huu kwani umenipa mimi fursa ya kukueleza ilikuwaje hadi BAKWATA ikaundwa.
Nitajaribu kueleza kwa ufupi kwa kuwa kisa chake ni kirefu mno na ikiwa unakitaka kukisoma chote unaweza kukipata hapo chini na ni ''research paper'' (1989):
Naomba nikutahadharishe.
Hili si suala la kutaka kulifanyia haraka ni tatizo linalotaka mtu kujituliza ukasoma historia kwanza ya uhuru wa Tanganyika na si usome historia rasmi kwani hiyo ni katika moja ya matatizo ya wengi wanaojaribu kuwajadili Waislam wakija na historia rasmi ndani ya vichwa vyao.
Uniwie radhi kwa kujifanyia mimi mwenyewe rejea.
Historia ya uhuru wa Tanganyika ambayo inaweza kukuweka katika hali ya kulielewa zaidi hili tatizo ipo imeandikwa na inasomwa sasa huu mwaka wa 20 (Said 1998).
Sasa tuendelee.
Unapozungumza BAKWATA si watu bali taasisi na viongozi wake na wala hakuna asemae kuwa BAKWATA si Waislam.
Muhimu sana ufahamu kuwa BAKWATA haikuundwa na Waislam kwa maana ya kuwa Waislam wenyewe waliitaka iwepo.
BAKWATA imeundwa na kikundi cha masheikh na wanasiasa waliokuwa ndani ya TANU wakipewa msaada na serikali na vyombo vyake vyote.
Historia ya BAKWATA imeandikwa na watafiti wawili tu hadi sasa miaka 50 baada ya kuundwa kwake Kiwanuka (1973) na Said (1989).
Kiwanuka kaandika akieleza kwa nini serikali iliamua kuuunda BAKWATA na Said akaja kujibu (rejoinder).
Sasa ikiwa utawasoma hawa wote utakuwa umejiongezea elimu ya kutosha kuelewa tatizo la BAKWATA na Waislam.
Kwa nini serikali iliamua kuivunja EAMWS na kuunda BAKWATA?
Baada ya uhuru mwaka wa 1961 EAMWS illikuwa imeanza mipango ya kujenga Chuo Kikuu Cha Waislam kutokana na maazimio ya Muslim Congress ya mwaka wa 1962 iliyoweka mikakati ya kuwainua Waislam katika elimu kwa kujenga shule kila jimbo Tanganyika na kumalizia na kuwa na Chuo Kikuu.
Kuna watu walitishika na juhudi hizi za Waislam na njia pekee ya kuvuruga mipango hii ya elimu ilikuwa ni kuivunja EAMWS.
Hawakutaka Waislam waelimike kwani wakielimika watashiriki katika kuongoza nchi hapa kilichokuwa kinatafutwa ni ''maintenance of status quo.'' hali ile ile ya ukoloni iendelee kwa Waislam kuwa daraja la chini wasio na elimu.
Haingii akilini kuwa Waislam waliotoka katika dhulma za ukoloni uliowanyima elimu wataamua kuivunja EAMWS wakati inajenga Chuo Kikuu.
Baraza la Wazee wa TANU hata siku moja haijataka kuona kuwa Uislam ndiyo unaoongoza serikali.
Unasema jambo ambalo wewe huna ithibatinalo na ingeikuwa ni hivyo Nyerere asingeungwa mkono na Mufti Sheikh Hassan bin Ameir na Waislam wale wa 1950s.
Sikulaumu unasema hayo kwa kuwa huijui historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika.
Waislam hawajasimamia lolote ila kutaka haki na usawa.
Naomba nisimame hapa.
Nakusihi soma kwanza historia ya uhuru wa Tanganyika ndipo utakuwa katika hali ya kujadili ukiwa na elimu ya kutosha vinginevyo itakuwa ni mimi kurejea hapa tena na tena kukusahihisha na kukueleza ukweli kama nifanyavyo hivi sasa.