Nini hasa kilisababisha vurugu za Mwembechai mwaka 1998?

Ngoja nitembee na huu uzi na mimi nipate elimu kidogo.
 
View attachment 1207828
Zahaki Rashidi
​
Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.

Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.

Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.

Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania’ .

Zahaki atajwa katika ujambazi

Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.

Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.

“Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu,” alisema Zahaki.

Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.

“Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu”, alisema Zahaki.

Zahaki aliongeza: “Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake”.

“Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit’ - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge’. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi”. Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.

Ujumbe kwa Waislamu

Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.

“Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri” alisema Zahaki.

Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.

Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa

Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.

Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.

Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.
Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.

Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
uchunguzi
duh!
hatari hii
 
Aslamwalekhum

Serikali ni kichwa dini ni masikio na sio kinyume chake. Masikio yanapotaka kuzidi kichwa haitaleta picha nzuri,
Dini ibaki kuwa dini, na hakuna sababu ya kuleta uwiano sawa wa serikali katika watu wa dini.

Yaliotokea yameyokea lakini tujifunze mipaka yetu mashekh wenzangu, ya kaisari yabaki kwa kaisari na ya mungu tumuachie mungu

Mimi kama muislam swafi hadhia ya mwembe chai chanzo kilikua sis wenyewe waislam ukweli ambao hatuutaki kuusikia (mtanisamehe kwa hili)

Tunatumia nguvu katika kuaminisha uislam ni dini ya kweli na haki, mihadhara isiyo na tija na tunajisahau kwa maneno ya kashfa katika dini za wenzetu tunafika mbali hadi kuingiza itikadi zetu kitaifa (hili taifa haliamini katika dini )

Mafunzo ya karate na Kong fu tunajilinda na nani? Kwani jeshi la kulinda nchi halipo? Hayo mafunzo yapo katika misingi gani? Mafunzo ya karate katika nyumba za ibada tunaabudu mungu au tunaandaa jeshi? Kwanini mafunzo ya karate yanakua kama ya lazima kuna ajenda gani? (Hapa kuna maswali mengi yasiokua na majibu)

Takbil..
hoja fikirishi hii
 
RPC alikuwa Alfred Gewe,hata mimi ningependa Kufahamu ukweli,Serikali ilidai Kuna baadhi ya nchi zilikuwa zinawapa mafunzo wahuni wa chama fulani,wengine wakidai kuna viongozi wa dini na serikali wanachochea chinichini kwa manufaa ya kisiasa,ukweli usiopingika ni kwamba walikula shaba live ndani ya msikiti na idadi ya wafu kufichwa,muhenga yeyote mwenye details zaidi aziteme.
🤣🤣🤣🤣🤣 ile situation ilikuwa kama movie ya kivita,,,sitakaa nisahau
 
nakumbuka Sheikh Ponds kipindi hicho alikuwa anacheza karate...aliwadhibiti wale mapoti Kwa kung-fu

walipozidiwa Kwa kung-fu za wale maustazi, wakakimbia na kwenda kuita Kaka zao..

eee bhanaa wee.! acha kabisa..

hadi sisimizi walikuwa hawakatishi Eneo hilo nao walikuwa wanapigwa;ndege WA angani nao walikuwa wanapigwa risasi live wakikatisha..

kile kikosi kilikuwa hatari Kama Barcelona ya Guardiola.! Hakuna huruma
🤣🤣🤣🤣🤣
 
Hapa Ponda kasingiziwa. Shida ilianzia pale kwenye kile kikundi cha "Yesu sio mwana wa Mungu" mahubiri/mihadhara yao ilichukua muda mrefu sana bila reaction yoyote kutoka kwa Wakristo, kilipokuja kile kikundi cha bwana Simbaulanga cha "Biblia ni JIBU" ndipo sasa ikaanza kuonekana eti serikali ina mfumo "Kristo" Kina "askofu" Mwaipopo walitukana Ukristo weee na Wakristo wakawa kimya tu, Kina Simbuulanga wakaaanza kuonesha jinsi mtume Mohamadi alivyo pewa utume na kuonesha idadi ya kina mama aliokula nao URODA, weee, watu wakakosa uvumilivu, yaliotokea ni historia tu. Nilikuwepo Dar mwaka huo, nakumbuka vizuri sana
dooh!!!
hatari
 
hili ndilo tatizo la mambo yanayohusu Imani kila mtu anavutia upande wake...
 
Nilishakwambia siku nyingi kuwa wewe ni 'con artist' aliyekubuhu, labda hukumbuki tu.
Unayoyaweka hapa ni 'ngonjera' zisizokuwa na miguu wala kichwa, lakini kazi ya 'con artist' siku zote ni kuwanasa wenye akili zilizolala.

Sasa, wewe kuitegemea aina hii ya watu kuwa siku moja utafanikiwa kuleta mapinduzi unayoyatafuta ni kujipa matumaini yasiyokuwepo.
ndugu unavyomjibu bila kuleta hoja stahiki juu ya utetezi wako unaonekana una chuki tu na huyo mzee...
 
Sina chuki na huyo mzee, ila nina chuki na "u-con-artist' wake. Kama wewe huuoni, basi endelea kusherehekea.
 
Kalamu 1,
Unazungumza kuhusu ''con artist?'

Kukusaidia kuelewa unachosema nakushauri usome kitabu hiki: ''Count Victor Lustig: The Man Who Sold the Eiffel Tower.''

View attachment 1211033
Nyuma yangu ni Eiffel Tower, Paris​

Unazungumza kuhusu mapinduzi?
Kitabu cha Abdulwahid Sykes kimepindua historia nzima ya TANU na uhuru wa Tanganyika.

Kiko ndani ya Cambridge Journal of African History na kinasomeshwa kote Marekani na Ulaya na kwengineko kama rejea katika political history ya Tanzania.
​
Ninayoyasoma mimi wewe huwezi kabisa kuyasoma na kuyaelewa. Kwa hiyo sina muda kabisa wa kupoteza na ngojera hizi za kudhani kuweka "Cambridge' na majina ya watu unajiona kuwa wewe ni msomi.
 
Sina chuki na huyo mzee, ila nina chuki na "u-con-artist' wake. Kama wewe huuoni, basi endelea kusherehekea.
waweza nifafanulia huo 'u-con-artist' wake ili niweze kuelewa upande wako?
 
waislam ni watu wa kulalamika popote pale walipo duniani,mecca tu wanalalamika itakuwa kwa warabu weusi wakina ponda,mohamed said etc wanaona wanajua dini kuliko warabu wenyewe waliyeletewa marehemu mudi.
Wakuu wa jukwaa,

Leo ningeomba tukumbushane, ni nini hasa kilisababisha vurugu za mwembechai mwaka 1998? Wakina nani walikuwa nyuma ya tukio lile? Wangapi walipoteza maisha? Je kuna askari ambao walichukuliwa hatua yoyote kutokana na vurugu zile?

Ahsanteni.

MAONI YA WADAU

Pia Soma
 
Ukimya wao sio sababu ya uoga wa kuuawa kama mwembechai..... Huwezi jua next time wakaja kwa style gani kujibu mapigo!! Yataweza jitokeza ya kibiti ama Al Shabaab unafikiri utapata kiburi cha kuja kuwakejeli humu??
Violence sio suluhisho zaidi imeongeza chuki na visasi siku watu wakisema inatosha kama wahutu 1957 ama walendu 2000 huko DRC basi hutopata hata wasaa wakuandika humu JF

Time will tell!

Sina uhakika kama Waislam mnapoandika na ku-post baadhi ya maneno kama huwa mnatumia hata sehemu ndogo ya akili zenu sawa sawa,hivi unadhani kama yakatokea hayo makundi hata wewe utapona?dada yako atapona?even mwanao/wanao kama unao unadhani watakuwa salama?

Hakuna mtu anaekiogopa kifo but kije kwa njia ambayo hata marehemu mwenyewe anaona ni haki yake siyo vifo vya kupokana uhai kama wafanyavyo hao jamaa,kingine msipende kuwatisha watu hata hao unaodhani mtapambana nao nao watakuwa wanawatamani nyie chunga mdomo wako omba haya yasitokee.
 
Wewe mzee wa anabu sana unatetea majambazi?unatamani hata nchi hii iangamie ubaki wewe na waislamu wenzio tu.wewe ni mtu hatari sana,hupaswi kumaliza maisha yako uraiani kwa ajenda zako la kuligawa Taifa.

Vijana kwa wazee huyu ni mtu wa kumuepuka na kumuogopa kama UKOMA.
View attachment 1207828
Zahaki Rashidi
​
Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.

Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.

Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.

Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania’ .

Zahaki atajwa katika ujambazi

Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.

Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.

Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.

“Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu,” alisema Zahaki.

Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.

“Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu”, alisema Zahaki.

Zahaki aliongeza: “Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake”.

“Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit’ - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge’. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi”. Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.

Ujumbe kwa Waislamu

Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.

“Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri” alisema Zahaki.

Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.

Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa

Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.

Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.

Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.

Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.
Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.

Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.

(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
uchunguzi
 
Tunahitaji kusikia pande zote mbili, za Serikali na Waislam, ila serikali huwa haitaki kabisa huu mjadala uwepo
Mkuu!!!

Hivi ukishamfundisha mwanao adabu kwa kumchapa kisawasawa unadhani kuna haja ya kukaa nae mezani na kuanza kufanya mjadala mkijadiliana kwamba ilikuwaje,na kwanini?

Personally,serikali iko sawa na tuitunze amani kidogo tuliyo nayo haya mambo watu wanakaa hawafanyi kazi wanalalamika lalamika hovyo pasi na sababu za msingi wakiendelea kuchekewa chekewa tutashindwa kuwaona wajukuu zetu,ni kuwashugulikia tu plan A {negotiations} ikishindikana serikali i-skeep to Plan C even D ili tukae sawa.

Nazungumzia mtu au kikundi chochote,hapana kuchezea amani ya taifa.
 
Wale walikuwa waislamu wewe na mohamed said mnapotosha mpate huruma ya Umma.
Kweli Komba Mboga Nikombe Ugali.. Na polisi walipoona wengi ni wakristo ili kuaminisha umma walikua wanadeal na Waislam, wakawapa majina ya kiislam... unaweza ukacheka ujue!
 
Sina uhakika kama Waislam mnapoandika na ku-post baadhi ya maneno kama huwa mnatumia hata sehemu ndogo ya akili zenu sawa sawa,hivi unadhani kama yakatokea hayo makundi hata wewe utapona?dada yako atapona?even mwanao/wanao kama unao unadhani watakuwa salama?

Hakuna mtu anaekiogopa kifo but kije kwa njia ambayo hata marehemu mwenyewe anaona ni haki yake siyo vifo vya kupokana uhai kama wafanyavyo hao jamaa,kingine msipende kuwatisha watu hata hao unaodhani mtapambana nao nao watakuwa wanawatamani nyie chunga mdomo wako omba haya yasitokee.
Wapi nimetetea ugaidi?? Umesoma mpaka mwisho kabla hujaquote?? Nani kasema mimi muislam??
Nachopinga ni watu humu kusema mauaji yale yamemaliza kelele za waislam!! Ndio ninawahoji ni lini violence imekua suluhisho la watu kulalamika??
Wahutu walibyamazishwa kwa manguvu kwa miaka mingi ila walipoamua kujibu 1994 ikawa fundisho!!

Nachosema ni hiki..... Mauaji sio suluhisho la malalamiko ya waislam, mki compromise nao hasira zitaisha automatically

Jifunzeni kwa kenyatta uliona kaua mjaluo yeyote uchaguzi uliopita kisa odinga kujiapisha?? Alijua angechochea vita hivyo akaona ni bora apatanishwe na odinga na kusikiliza Madai yake na leo hii kenya amani tupu.

Narudia tena mabavu sio suluhisho la MALALAMIKO YA WAISLAM
 
Back
Top Bottom