Ngoja nikuitie Mkuu Maalim Mohammed Said
P
Ulijuaje dini za waliokamatwa?Sikumbuki exactly but kilichoshangaza waliokamatwa walikutwa wakristo wengi sana
So mostly inaonesha kulikuwa na kilio tu cha watu kudai uhuru wa kuandamana
na uhuru wa kupinga hiki au kile...
Msikiti wa mwembechai ulitumika tu kwa raia wengine kujiunga kwenye madai hayo
Chanzo kilikuwa Paroko Lwambano kwenda Sehemu Nyeti kusema kuwa ndani ya Msikiti wa Mwembe chai Yesu alikuwa anatukanwa
Enzi hizo kusema Muhammad sio Mtume haiku warm kosa
Kusema Ng’ombe sio mungu haikuwa kosa
Kusema mizimu sio Mungu pia haikuwa kosa
Kosa lilikuwa kusema Yesu sio Mungu ni kosa kubwa kuliko kukutwa na Kete za Bhange
Baada ya watu kukubali kufa, kujeruhiwa na kufungwa hatimae baadae Mahakama Kuu ikatangaza rasmi kuwa sio kosa na aliefungwa kwa kosa hilo aachiwe huru na Ndugu Hamis Dibagula akaachiwa huru
Kuna baadhi ya haki hazipatikan kwa kutoa press release wala kuitisha Makongamano ya kudai bali lazima uumie kuipata
Kwani ni lazima kuchokonoa imani za wengine?
Huo ni upuuzi.
Kuna wahuni kama ninyi mlikuwa mnamjaribu Ben Yamini
Unaambiwa ukitoka nje ya nyumba yako ya ibada wewe unakuwa mtanzania.Mfano hili la mwembechai watu wanasema yao tu mmewasikiliza waislam
Shushia milungi basi we chapombe.Daah kweli bangi sio mchicha
Watu wameshasema aliyelianzisha ni Askofu Lwambano. Ukitaka kujuwa zaidi kitabu cha Hamza Njozi kimetajwa juu huko, kitafute, kipo cha bure kwenye mtandao.
Kaka tushajua baba yako alikua waziri hakuna haja ya kurudia mara kwa maraAisee!!! Kitambo sana, na hii hairuhusiwi kujadiliwa popote na haitakiwai uujue ukweli, kulikuwa na kitabu kinacho zungumzia hii kadhia lakini naskia hakiruhusiwi nchini...
Nakumbuka Waziri wa Mambo ya Ndani, alikuwa Bw. Ali Ameir, na waziri mkuu mkuu alikuwa F.Sumaye..
Hhaah!! Mzee kipindi hicho alikuwa Waziri, dah maisha yapo fasta.....
Sio kweli,waliendeleza hadi kwenye viwanja vya wazi.Maneno hayo yaliongelewa Msikitini sio mitaani
Zahaki Rashidi Ngai si jina geni katika masikio ya Waislamu wengi hapa nchini. Yeye ni mmoja kati ya wanaharakati wachache ambao wametajwa sana na masheikh, vyombo vya habari na hata katika vitabu maarufu vilivyoandikwa na waataaluma wa Kiislamu.
Umaarufu wa Zahaki umetokana na kutajwa shuhuda muhimu wa tukio la mauaji ya Mwembe Chai na dhuluma mbalimbali ambazo Serikali imewatendea Waislamu.
Kwa mara ya kwanza, Zahaki alitoa ushuhuda wake kwa mwanahistoria maarufu Muhammedi Saidi. Alifanyiwa mahojiano maalum kuhusu ukweli wa mauaji ya Mwembe Chai. Hapo aliyasema yote aliyoyaiona na aliyoyaamini.
Baada ya hapo, ushuhuda huo ulichapishwa katika kitabu maarufu cha Prof. Hamza Njozi, kilichoitwa, ‘Muslim and state in Tanzania’ .
Zahaki atajwa katika ujambazi
Akizungumza na gazeti la Imaan kabla ya kwenda polisi kuhoji kutajwa kwa jina lake katika taarifa zilizozagaa katika mitandao ya kijamii akitajwa kama miongoni mwa wahumiwa wa mauaji yaliyotokea kituo cha polisi Stakishari.
Alisema baada ya kupokea taarifa hizo za kuhusishwa na uhalifu huo, hatua ya kwanza aliyofanya ni kutaka kukutana na waandishi wa habari ili Waislamu wenzake wajue ukweli juu ya dhuluma ambayo jeshi la polisi linajaribu kumfanyia akiamini inatokana na historia yake ya kusema kweli kuhusu tukio la mauaji ya Mwembe Chai.
Alisema kinachotokea sasa ni matokeo ya chuki na kisasi cha muda mrefu kilichotokana na uamuzi wake ya kusema kweli katika tukio lile la mwaka 1998 ambalo lilipelekea kufukuzwa kazi ya polisi na kufedheheshwa baada ya kulikosoa jeshi hilo.
“Najua mtuhumiwa akishafika katika mikono ya polisi ni vigumu kukutana na waandishi wa habari na kuzungumza ukweli. Baada ya kuliona hilo nimeamua kukutana nanyi ili kuwaambia ukweli Waislamu wenzangu kuwa katika tukio hili mimi sihusiki hata kidogo na hata huyo anayetajwa kuwa kiongozi wa kundi simfahamu,” alisema Zahaki.
Alisema kutokana na matukio ya Mwembe Chai, Jeshi la Polisi lilikasirishwa na limekuwa likimfuatilia kila hatua ili ipatikane nafasi ya kumpa kesi ili wampoteze ulimwenguni.
“Ndugu waandishi wa habari, mimi miaka yote nipo hapa nchini, nina wake wawili ambao naishi nao. Ajabu ni kwamba Jeshi la Polisi linadai mimi nimerejea kutoka Ethiopia. Huo ni uzushi ambao wanajaribu kuutumia ili nionekane muhalifu wakati ni uongo mtupu”, alisema Zahaki.
Zahaki aliongeza: “Jeshi la polisi wawe wa kweli. Wafanye utafiti wao kwa makini badala ya kuvamia watu kwa kuwa shuku kwani hatua hiyo itafanya kukamatwa kwa watu ambao hawana hatia jambo ambalo halitamuathiri mtuhumiwa peke yake bali litaathiri maisha ya watoto, wake na wazazi wake”.
“Mimi nilikuwa Sajenti katika kitengo cha ‘Crime Stoppers Unit’ - Central Police. Tukio la Mwembe Chai lilivyotokea mimi nilikuwa ndio ‘in charge’. Nilitoa maelezo yangu kuhusu taarifa za tukio hilo lakini jeshi halikuridhika. Wamenifukuzwa kwa aibu na sasa wananishughulikia nje ya Jeshi la Polisi”. Alilalamika Zahaki huku machozi yakimlenga lenga.
Ujumbe kwa Waislamu
Zahaki amewataka Waislamu wenzake kumuombea dua kwa mtihani huo ambao ameupata huku akiwahakikishia kuwa hajahusika katika uhalifu huo uliotekelezwa katika kituo cha Stakishari.
“Wa Llaah wa Billaahi sijahusika na uhalifu wa Stakishari, Mwenyezi Mungu anajua zaidi. Nitakwenda kuwahoji kwa nini wametaja jina langu na kulihusisha na mauaji yale, na pia kwa nini wanadanganya umma wa Watanzania kuwa mimi nimerejea kutoka Ethiopia wakati nipo hapa nchini? Wana ajenda gani ya siri” alisema Zahaki.
Aidha, Zahaki alisema anataka Waislamu wajue ukweli wote hata akiwa ameshikwa na Jeshi la Polisi ama kuuliwa katika mazingira ya kutatanisha, wajue kilichomuua ni chuki kutokana na kusema kweli katika kadhia ya Mwembe Chai.
Aibukia Jeshi la Polisi, akamatwa
Kama alivyoahidi kwa waandishi wa habari kuwa angekwenda kuhoji Jeshi la Polisi juu ya jina lake kuhusishwa na mauaji ya Stakishari, Zahaki kweli alifanya hivyo . Lakini taarifa ambayo Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam ilIitoa kwa waandishi wa habari ilisema mtuhumiwa huyo alijisalimisha.
Akizungumza na waandishi wa habari, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova alisema Mtuhumiwa Zahaki Ngai amejisalimisha kwa Jeshi la Polisi akiwa na wake zake wawili na kusema kuwa wale ambao bado hawajapatikana msako bado unaendelea.
Maneno hayo ya Kamishna Kova ni kama mwiba kwa Zahaki ambaye alishatangaza kuwa anaenda kuhoji kwa nini jina lake limetajwa na sio kujisalimisha. Kama alivyotabiri, inaonekana kama polisi wameendelea kupotosha umma.
Akizungumza na gazeti Imaan, Mwanasheria wa mtuhumiwa huyo alisema wanashangazwa na upotoshaji wa Kamanda Kova kwa umma wa Tanzania kwani Zahaki hakwenda kujisalimisha bali alikwenda kuuliza ukweli wa tetesi anazozisikia katika vyombo vya habari.
Kilindo alisema upotoshaji huo unakera na unaudhi kwani matamshi ya Kamishna wa polisi ni sawa na kuthibitisha kuwa ana uhakika Zahaki ni mhalifu na hivyo kupewa kesi hiyo wakati yeye hakuhusika na kadhia hiyo.
Katika tukio ambalo polisi wanadai Zahaki alihusika, majambazi kadhaa yalivamia kituo cha polisi cha Stakshari na kuua watu saba majira ya saa 5 usiku, Julai 12, 2015. Mpaka sasa tayari watuhumiwa tisa wanahojiwa kuhusiana na tukio hilo.
(Makala kwa hisani ya gazeti la Imaan Agosti 31 - Septemba 6, 2015)
uchunguzi
Serikali si jinga hadi kutumia silaha ya moto. Wacha kulialia humu. Ilikuwa ni sahihi kutuliza ile ghasia kwa mtindo ule.
Spirit ile ile ndo ilikuwa ikiunda kikundi chenye mwelekeo wa uamsho (Tanzania), alshabab (pembe ya africa), Tuareq (central africa) na bokoharam (west africa). Tanzania ikashindikana kwa sababu serikali ilikataa kulea uhuni, ingawa walitaka kuchomoza tena kupitia Amboni Tanga na Mkiru. Hawa watu si wa kucheka nao hata kidogo.
Katika Jambo nawapongeza TISS ni hiliSerikali si jinga hadi kutumia silaha ya moto. Wacha kulialia humu. Ilikuwa ni sahihi kutuliza ile ghasia kwa mtindo ule.
Spirit ile ile ndo ilikuwa ikiunda kikundi chenye mwelekeo wa uamsho (Tanzania), alshabab (pembe ya africa), Tuareq (central africa) na bokoharam (west africa). Tanzania ikashindikana kwa sababu serikali ilikataa kulea uhuni, ingawa walitaka kuchomoza tena kupitia Amboni Tanga na Mkiru. Hawa watu si wa kucheka nao hata kidogo.
Bado hujaeleza yenye uzito wa kutufanya sie wengine ambao tulikuwa bado wadogo kipindi hicho tuweze kuelewa uhalali wa mauwaji ya mwembechai. Miaka ishapita na watu wanataka kujua nini hasa kilitokea hakuna haja ya kuficha kama fujo za waislamu hujulikana ila yale mauwaji ndio ndio kitu ambacho watu wanataka kujua ni nini hasa kilichosababisha.Kilichosababisha mwembechai kinuke mwaka 1998.
Ingawa nilikuwa mdogo, lakn kiasi nilikuwa na uelewa wa kuangalia taarifa ya habari na kusimulia kwa ufupi nini kimeelezwa.
Ikumbukwe kuwa mwaka 1998 vuguvugu la vurugu la udini lilitaka kuitawala Tanzania na Afrika mashariki na dunia kwa ujumla kwa kujithibishia kuwa dini IPI ni bora na ina nguvu kiasi gani.
Ni kipindi ambacho dini moja ilikuwa inamikutano ya kutafuta waumini kwa kuita mihadhara ya hoja na kualika msemaji kutoka dini nyingine kubishana kwa hoja. Mihadhara hii ilifanyika sana karibu kila kiwanja cha wazi kilichopo karibu na nyumba ya ibada maeneo km mwananyamala...magomeni...manzese ...kigogo...kinondoni mtambani nk n jambo LA kawaida kukuta mihadhara ya dini na kina Dr sule wakihutubia kipindi hicho.
Ikumbukwe pia ni kipindi hikihiki cha mwaka 1998 ndicho kulizuga propaganda nyingi sana za udini hata ikafika mahali ndani ya sehemu ya nyumba ya ibada kunakuwa na mawaidha ya kuhubiriana kuwa dini Fulani INA viongozi wengi serikalini kuliko sisi kwahyo wanatutawala na hatuna maamuzi katika nchi yetu.
Mwaka 1998 kama ulikuwa na akili timamu ndio kipindi ambacho kila nyumba ya ibada nilikuwa na mafunzo ya karate kwa vijana wa dini kwa lengo LA kujilinda. Self defence ukiniuliza walikuwa wanajilinda nini ? Sina jibu.
Na ndio mwaka huo kulikuwa waliibuka viongozi wa dini wenye ushawishi mkubwa kwenye mimbari..kwa Tanzania na Afrika mashariki. Watu km shekh Rogo kule Mombasa...kulikuwa na connection na shekh mmoja alikuwa Mwanza kwa Tanzania na wengne walikuwa visiwani.
Serikali kwakuona hatari ya mbele ikapiga BAN mihadhara yoyote ya dini. Hapo ajenda za ajabuajabu zukapita kupitia nyumba za ibada kuwa wanatunyanyasa umma.
Na mengne meng ambayo huwezi kuandika hapa kwa usalama wa nchi na kuibua tena hasira za wafia dini na kuchafua nchi. Naishia hapa kwa machache baada ya upande mmoja kushindana serikali ya Ben kipindi hicho.
Akili yako imeganda wewe mwarabu mweusi!Unisema Muamini Yesu kama Mkombozi wa Maisha yako hujui tayar umechokonoa Imani ya Wengine?
Shule yako hafifu sana
Ukisema Achana na Mambo ya Mizimu muamini Yesu tayari umeingilia Imani ya mwingine
Mkuu, Dibagula aliachiwa na Mahakama ya Rufani...hukumu iliandikwa na Jaji Mkuu Samatta.Chanzo kilikuwa Paroko Lwambano kwenda Sehemu Nyeti kusema kuwa ndani ya Msikiti wa Mwembe chai Yesu alikuwa anatukanwa
Enzi hizo kusema Muhammad sio Mtume haiku warm kosa
Kusema Ng’ombe sio mungu haikuwa kosa
Kusema mizimu sio Mungu pia haikuwa kosa
Kosa lilikuwa kusema Yesu sio Mungu ni kosa kubwa kuliko kukutwa na Kete za Bhange
Baada ya watu kukubali kufa, kujeruhiwa na kufungwa hatimae baadae Mahakama Kuu ikatangaza rasmi kuwa sio kosa na aliefungwa kwa kosa hilo aachiwe huru na Ndugu Hamis Dibagula akaachiwa huru
Kuna baadhi ya haki hazipatikan kwa kutoa press release wala kuitisha Makongamano ya kudai bali lazima uumie kuipata
Tatizo watu hawataki kujua ukweli wa mambo,ukweli ni kuwa waislam wanapakaziwa mambo mengi ya uongo,mtu anakwambia kuna rumours wakati kuna kitabu kinaelezea kila kitu,hata sheikh ponda aliitwa gaidi kwa kusema ukweli,masheikh wa uamsho wanaonewa bila sababu ukiuliza wanasema ugaidi,kuna chuki dhidi ya waislam kubwa sanaSio rumours mambo mengi yalikuwa yanaendelea
Viashiria vya ugaidi misikutini ikiwa bi pamoja na mafunzo ya karate na siraha kama visu so selikal ikaona izuie haya hasa misikitini na ndio sababu wahanga wa kubwa walikuwa masheheChanzo cha vurugu na mauaji kilikuwa ni nini kulingana na DTV?