Bila shaka mhalifu alikuwa anatafuta huruma ya magaidi wenzake
Kipuyo,
Tufanye hoja kwa utulivu na kuheshimiana mjadala huu utakuwa na faida kubwa.
Zahaki haki alikuwa ofisa wa polisi baada ya kushuhudia yale yote yaliyotokea kama ulivyosoma na alikuwa anatafuta mahali aeleze anayoyajua ili ukweli ufahamike.
Hapo alikuwa kafukuzwa kazi kwa kuonewa tu.
Wahariri wote wa magazeti aliowaendea walikataa kuchapisha stori yake ndipo watu wakamshauri aje kwangu.
Mimi sikuwa naishi Dar es Salaam nilikuwa Tanga na wala sikukuwa namjua.
Akanipigia simu tukaweka miadi nikaja Dar es Salaam nilifanyanae mahojiano na nikamrekodi na kupiga picha.
Maelezo yake yaliniathir sana nikafanya nakala ya ile cassette nikawapa baadhi ya viongozi wa Kiislam wasikilize na kutoa ushauri nini kifanyike.
Hadi kufikia hapo ukweli wa Mwembechai ulikuwa umeshafahamika kuwa hapakuwa na silaha msikitini kama alivyosema Yusuf Makamba wala hapakuwa na mhadhara Mtambani.
Serikali imechukua hatua na kuua Waislam kutokana na taarifa zisizokuwa kweli.
Hili lilikuwa jambo zito.
Serikali haikuzubaa ilipowadhihirikia kuwa imefanya kosa kubwa sana ikawa nayo inafanya juhudi hili jambo limalizike kimya kimya na kwa salama ili kupunguza uhasama katika jamii.
Hii ndiyo sababu hata Inquest haikufanyika kama sheria inavyotaka.
Mimi si gaidi nafahamika, Zahaki si gaidi wala halikadhalika Prof. Njozi si gaidi na ni watu tuna heshima zetu katika taifa hili.
Ndipo nikasema tufanye mjadala wa heshima.